Kenya Election 2007: Outcomes

na je wanatumia systema gani?wengi wape ama lazma mtu avuke nusu??

Kwa Kenya hakuna kuvuka nusu. wanatumia wengi wape, yaani aliyewashinda wenzake, ili mradi awe na at least 25% kwenye majimbo angalau matano kati ya nane na pia yeye mwenyewe ashinde ubunge kwenye jimbo lake.

Ukiangalia hapo utaona kati ya Kibaki na Raila, wote wawili watafikisha hizo 25% katika majimbo matano na pia most likely wote watashinda ubunge kwahiyo kinachobaki ni nani kapata kura zaidi.
 
Kazi ipo. Jamani tukiendelea kufuatilia haya matokeo tuwe tunajiuliza sisi watanzania tutafikia lini hatua ya ushindani kama ya hawa wenzetu? tufanyeje ili nasi tufike hapo? Nafikiri wazo moja ni sisi "elites" tunaoweza angalau kushika keyboard kushiriki kikamilifu katika kujenga upinzani badala ya kukaa kuwalalamikia na/au kuwasifia akina Wangwe na Zitto tu design ya football fans! Ndivyo walivyofanya wenzetu Kenya.
 
Kenya ushindani wa kisiasa umepanda juu na demokrasia yao kukomaa zaidi baada ya kuiondoa KANU madarakani. Kiwango cha demokrasia na ushindani wa kisiasa hapa Tanzania hakitapanda mpaka pale CCM itakapoondolewa madarakani; kwa bahati mbaya huo ndio ukweli wenyewe.

Kwa mfumo wa sasa hivi CCM imekuwa kama ni idara moja ya serikali kiasi kuwa tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi (na hata Jeshi la Ulinzi - TPDF), TVT, Radio Tanzania, Idara ya kuendesha mashtaka, Taasisi ya kuzuia rushwa, benki kuu na vyombo vinginevyo kama hivyo vinailinda CCM kwa namna mja au nyingine. Baada ya CCM kuwa out ndipo vyombo hivyo vitakapoanza kujifunza kuwa independent na hivyo kusaidia kukomaza demokrasia.
 
Kazi ipo. Jamani tukiendelea kufuatilia haya matokeo tuwe tunajiuliza sisi watanzania tutafikia lini hatua ya ushindani kama ya hawa wenzetu? tufanyeje ili nasi tufike hapo? Nafikiri wazo moja ni sisi "elites" tunaoweza angalau kushika keyboard kushiriki kikamilifu katika kujenga upinzani badala ya kukaa kuwalalamikia na/au kuwasifia akina Wangwe na Zitto tu design ya football fans! Ndivyo walivyofanya wenzetu Kenya.

Kitila,

Matatizo yetu ni makubwa zaidi na yanatokana na katiba mbovu.

Pia sio kila mtu ataweza kushiriki moja kwa moja kwenye vyama, sio wote ni wachezaji, wengine ni watangazaji, na wengine washangiliaji.
 
....wewe mwenewe umefanya nini zaidi ya kelele tuu za hapa na pale ambazo ni za kujitafutia ulaji wako binafsi,ungeandika hata kitabu tungekuona serious
 
10.00 PM KTN News alert

CURRENT UNOFFICIAL TOTALS:

RAILA 39,538

KIBAKI 25,760

KALONZO 3,022

++++++++++++++++++++++++

Duru zakuaminika zinasema vigogo wa serikali wanaanguka kama miti msituni

Kwa mfano: Makamu wa Rais Mood Awori, Minista wa Mambo Ya Nje, Mwanake Moi aitwaye Gideon wote wanazidi kufifia huku kura zilizohesabiwa huko zikisema wapinzani wao ambao ni wa timu ya Raila watapata ushindi wa kishindo.,,,

Msilale...
 
Kenyan-Tanzania

Tupe two sides- please dont bias the results- or your presentation to Raila!

Mzalendohalisi,

Umesema kweli maana tusije tukaanza kunywa wine kumbe ni yale mambo ya Kerry na Bush ambayo mimi nililewa na kulala nikijua
kale kajinga kameenda na maji lakini kuamka asubuhi nikakuta Bush anatamba.
 
Huyo Mkenya-Mtanzania lazima awe biased kwa kuwa yeye ni pro-Raila na hivyo atakuwa anatuwekea news ambazo zinaonyesha Raila kashinda na asubuhi unasikia BBC wanasema Kibaki arudi Ikulu kwa kishindo!
 
....wewe mwenewe umefanya nini zaidi ya kelele tuu za hapa na pale ambazo ni za kujitafutia ulaji wako binafsi,ungeandika hata kitabu tungekuona serious

Of course, mimi sijajitoa, mimi pia ni sehemu ya tatizo! Ndio maana nimesema tufanyeje, sote, mimi, wewe, wao na yule!
 
Huyo Mkenya-Mtanzania lazima awe biased kwa kuwa yeye ni pro-Raila na hivyo atakuwa anatuwekea news ambazo zinaonyesha Raila kashinda na asubuhi unasikia BBC wanasema Kibaki arudi Ikulu kwa kishindo!

Lakini mbona amekuwa akitoa kutoka pande zote mbili. Soma hapo juu mwanzoni kabisa. Hata hivyo swala sio kumlaumu huyu ndugu ambaye ameamua kutupa haya manews bure kabisa, vinginevyo leteni basi source zenu ambazo ziko unbiased, kama hamuwezi mnyamaze tuendelee kupata haya mavituz ya huyu kijana mzalendo wa Kenya!
 
Kitila, Kichuguu,
Pole pole na sisi Tanzania tutafika. Tumeshatambua kuwa tatizo ni CCM na wamefanya uchaguzi kuwa mojawapo ya taasisi ya chama. Wananchi wameanza kulitambua hilo. Nimeangalia kwenye TV ya Kenya wananchi wakilalamika kuwa majina yao hayapo kwenye orodha ya wapiga kura na wakasema hawaondoki mpaka kieleweke. Tunayo kazi ya kuwaamsha wananchi, na nina hakika awamu ya 4 itatusaidia sana kuleta mwamko huo.
 
Kitila,

Matatizo yetu ni makubwa zaidi na yanatokana na katiba mbovu.

Pia sio kila mtu ataweza kushiriki moja kwa moja kwenye vyama, sio wote ni wachezaji, wengine ni watangazaji, na wengine washangiliaji.

Nafikiri tutajadili zaidi baada ya matokeo ya Kenya, ngoja nisiharibu mtiririko wa haya matokeo. Yatosha tu kusema kuwa matatizo uliyoyasema wewe na Kichuguu yalikuwepo Kenya tena makubwa zaidi wakati wa KANU. Pamoja na hayo wapinzani waliweza kuung'oa utawala wa Moi, na kusema kweli kilichobadilika katika utawala wa sasa ni mioyo na attitude za watendaji, social-structures ni zilezile! The issue is how do we mobilise the forces (voters) against CCM as they did in Kenya.
 
Kenyan-Tanzania

Tupe two sides- please dont bias the results- or your presentation to Raila!

Waheshimiwa msiwe na wasi wasi. Nawaheshimu na naheshimu JF siwezi waongopea ingawaje na support Raila. Nimuhim kuwa objective.

Ukichunguza hio grafu hapo juu mtaona Kibaki anaongoza kwa hapo.

Mambo bado MCHAKAMCHAKA ila kama nimevyokuwa nikiwaeleza Raila atashinda kwa margin kubwa.

Sasa mkiona nyingi ni za Raila juu ndivyo hali halisi ilivyo. So far anaongoza kwa mikoa ya Coast, Rift Valley, North Eastern na Nyanza. Kibaki anaongoza tuu Central huko kwao, Kalonzo Eastern atotako na Nairobi na Western Kibaki na Raila wanamenyana kiume.

Haya hii hapa news update mpya tena:

Latest: from polling station za constituencies mbali mbali nchini zikiwekwa kwa jumla:

Raila 53911
Kibaki 41 266
Kalonzo 4362

MUHIMU: Bado kuna mamilioni ya kura huko nje hazijamalizwa kuhesabiwa. Kwa sasa huwezi bashiri sana

elcfrntque271207.jpg
 
Waheshimiwa pia kuna site ambaye inatangaza kwa lugha ya Kikalenjin lakini pia na kiswahili. Mna

http://www.johnnniewalker.blogspot.com/

Click "ONLINE DRIVE" hapo chini ya huyo dubu anayekata kiuno. Matokeo namba moja hadi nne zipo kwenye lugha ya mama lakini tano hadi nane na zitakazozidi kutufikia zitakuwa kwa lugha ya Kiswahili
 
Wakuu

Nitawaleteeni matokeo zinazotolewa na KTN sabab wako na higher numbers (more people in the field) na more updates baada ya kila mda usiokuwa mrefu sana:

MUHIMU: Haya ni matokeo ya vituo fulani ambazo zimemaliza kwenye maeneo mbali mbali nchini. Kuna vituo vingi ndani ya kila eneo bunge. Halaf kuna maeneo bunge 210 nchi nzima zimezogawanika ndani ya mikoa nane: Central (kwa kina Kibaki), Nyanza (kwa kina Raila), Eastern ( kwa kina Kalonzo), Rift Valley (Kwa Moi), Western, Coast, Nairobi na North Eastern. Vituo vyote vikishatuma hesabu zao katika eneo bunge fulani basi hesabu za jumla zitapigwa chapchap na mshindi wa eneo hilo anatangazwa. Basi msiwe na shaka hili likitokea mimi hapa chap kwafahamisha sitachelewa

Nchi nzima:

K - 55,373
R - 66,383
Ka - 7,894

Zote hapo chini zimefuata taratibu ifuatayo:

Kibaki
Raila
Kalonzo

Central
23,576
378
68

Nyanza
545
18,614
10

Rift Valley
6,793
21,052
311

Nairobi
9,577
9,245
2,440

Eastern
5,527
396
2,276

Western
5,404
9,971
851

Coast
1465
3814
221

North Eastern
1,085
2,377
219
 
Back
Top Bottom