Kenani Kihongosi na ripoti ya TWAWEZA ya mwaka 2017

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
Neno ushiriki wa kisiasa kwa ujumla katika maana ni tabia yoyote ya kibinadamu au ushiriki ambao unachangia au unashawishi mchakato wowote wa kisiasa au matokeo.

Ushiriki wa kisiasa unaweza kuwa wa mtu binafsi kujihusisha moja kwa moja kwenye siasa kama mwanachama wa chama au mgombea wa chama kuingia madarakani kwa kuchaguliwa.

Inaweza kuwa kwa mtindo wa mwanachama muaminifu kushawishi wanachama wengi zaidi (watu zaidi) kujiunga na chama chake au kumpigia kampeni mgombea wa chama fulani au chama cha kisiasa mtu anachokipenda.

Ripoti ya utafiti wa Twaweza ya 2017 kwenye mradi wa sauti za wananchi uliyataja mambo kadhaa kuhusu CCM na kupendwa kwake.

Ripoti ile ilisema idadi ya wananchi wanaosema wapo karibu na CCM au Chadema imeshuka tangu mwaka 2015, CCM ikishuka kwa asilimia nne kutoka 62 hadi 58.

Ripoti hiyo ya "Demokrasia yetu" katika maelezo yake ilisema wanawake, Watu wa mashambani (Vijijini) na vijana wengi wasiokuwa na elimu ndiyo wenye kuikubali CCM zaidi kwa asilimia zinazofikia 64.

Ripoti hiyo ilisema kama makundi hayo yangebadilishwa mawazo huenda CCM ingepoteza kabisa wafuasi kwa asilimia kubwa sana.

Leo, Miaka mitano baadae mambo yamebadilika. Kinachoonekana ni Kubadilika kwa mtazamo wa vijana juu ya siasa za Tanzania na ushiriki wao kikamilifu katika kujengewa uwezo wa kiuongozi na masuala yahusuyo siasa pamoja na uongozi.

Hakuna ripoti iliyofanyika baada ya ile ya 2017 lakini picha, video na sisi tuliobahatika kuhudhuria baadhi ya matukio ya kisiasa tunaweza kuwa mashuhuda.

Kuna kazi kubwa inayofanyika chini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM) Ndg. Kenani Kihongosi na jumuiya anayoiongoza kwa mwaka huu mmoja.

Ni Kawaida kwenye Kila kona ya nchi ya Tanzania kufanikiwa kuwakutanisha mamia ya vijana katika shughuli zake. Ni Vijana ambao hushirikishwa mambo kadhaa ya kisiasa, Itikadi na Uongozi.

Ni vijana wa sifa na tabia tofauti tofauti,wenye elimu kubwa,ya kati,ndogo na wasiokuwa na elimu kabisa.Ni wanawake kwa wanaume

Huu ndo ushiriki wa vijana katika siasa uliozungumzwa miaka mitano iliyopita na utafiti wa Twaweza.Ni dalili nzuri na mtaji mkubwa kwa CCM katika chaguzi za mbeleni.

Leo Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi alikuwa Kishapu Shinyanga, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji vijana kujitokeza kwenye sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi ujao,jumanne ya August 23.

Mtindo wake wa uongozi,maisha aliyoamua kuyaishi na Unyenyekevu wake kwa anaokutana nao ama kuwaongoza ni miongoni mwa yanayovutia wengi kujitokeza kwenye shughuli zake wakijihisi utulivu na kwamba wapo sehemu sahihi kupitia yeye.

Ni kijana na anauishi Ujana hasa. Kupendelea kwake Muziki na kuucheza kama sio kuuimba katika majukwaa ya kisiasa kunawasisimua vijana wengi.

Kufikika kwake kirahisi na kuingilika na kila mmoja anayetaka kumfikia imekuwa ni chachu nyingine inayomkusanyia wafuasi wanaokuja kuwa watu muhimu kwenye siasa za Chama Tawala.

Malezi ya watu hawa wanaoletwa karibu na siasa na harakati za CCM ni muhimu sana yakaendelezwa na kustawishwa kwa Faida ya baadae ya Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

Mimi nipo tayari kuhesabiwa. Tujitokeze kuhesabiwa Ifikapo August 23, 2022.
 
Back
Top Bottom