Kelvin Carter Pixel [emoji328]

Kelvin Carter Pixel [emoji328]

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
906
KAMERA YA KEVIN YASABABISHA GUMZO LA DUNIA.

Na Bahati Samwel
Friday 16/6/2019
Namanga, Longido, Arusha-Tanzania

Sudan yaingia gizani miaka ya 90.

Sudan ni taifa la tatu kwa ukubwa Afrika na linashika nafasi ya kumi na sita duniani,eneo lake lina ukubwa wa kilometa za mraba 1,886,068, idadi ya watu ikiwa ni 40,235,000 kwa makadirio ya 2017 yatokanayo na sensa ya 2008 nchini humo, likijumuisha makabila 200, na sarafu yake inaitwa paund.

Sudan inaundwa na wilaya 18 zilizogawanywa katika Kata 133. Sehemu kubwa ya ardhi yake ni kiwira, mwangaza, mikuranga,na hupata mvua miezi ya April na Oktoba peke yake. Hivyo, uharibifu wa mazingira ni mkubwa utokanao na mmomonyoko wa udongo kwasababu ya jangwa. mji mkuu wake ni Khartoum.

Kijiografia Sudani ni nchi inayopatikana kaskazini mwa bara la Afrika, ikipakana na Misri upande wa kaskazini, bahari ya shamu upande wa kaskazini mashariki, Ertria na Ethiopia upande wa mashariki, Chad na Afrika ya kati upande wa magharibi na kaskazini magharibi imepakana na Libya.

Sudan ilipata uhuru wake kamili kutoka kwa Waingireza na Misri, 1.1.1956 ikawa Jamhuri ya Sudan, huku kauli mbiu ya nchi ikiwa ni Ushindi ni wetu yaani "al-nasr Lana" kwa kiarabu.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha duniani(IMF) ya 3.6.2018, jamuhuri ya Sudan pamoja na Sudan kusin ni miongoni mwa nchi maskini zaidai duniani, Sudan ikishika nafasi ya 28 kati ya mataifa 193 duniani huku Sudan kusini ikishika nafasi ya kwanza kwa umaskini duniani.

Historia ya Sudan ni kongwe ilianza tangu milenia ya 8 kabla ya kuzaliwa kristo mpaka kufikia kuitawala Misri kwa karne nzima ya nne baada ya kristo, lakini badae 1899 Misri ikisaidiwa na Waingereza ikitumia jeshi la watu 400 na meli za mvuke waliupiga ufalme wa Khalfa na Sudan ikatawaliwa mpaka ilipokuja kupata uhuru wake 1956.

Baada ya uhuru, Sudan ilipitia misukosuko ya kiusalama na kisiasa kwa miaka mingi katika vipindi vyote vya uongozi wake, serikali zote kuanzia ile ya Ibrahim abboud 1958 hadi 1964,Gaafar Nimeiry 1969 had 1985, Sadiq al-Mahdi 1986 hadi 1988 na Omar Hasaan al-Bashir 1989 hadi 2019 zilikumbwa na mapinduzi ya Mara kwa Mara.

Linapotajwa taifa la Sudan popote pale, jina la Luteni jenerali Omar Hassn al-Bashir linakuja kwa haraka kwasbabu, ndiye kiongozi pekee wa Sudan aliyejitangazia urais na akaitawala Sudan kwa miaka 30, lakini pia mtiririko wa matukio wakati wa utawala wake yanachangia kuibua hisia Kali na kujenga kumbukumbu ya kudumu kwa walimwengu.

Miaka ya 90 chini ya utawala wake Bashir, Sudan ilikumbwa na matukio hatari zaidi kwa usalama wa binadamu ambayo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu, ukame, na baa kubwa la njaa kuwahi kutokea duniani.

Matukio hayo yalisababisha giza nene kwa mamilioni ya waSudan, zaidi ya watu milioni mbili na nusu walikufa na wengine milioni tano kukosa makazi. Wakati vita, njaa, na jua kali yakiwatesa waSudan hadi kufikia hatua ya kupaza sauti wakisema Yu-wapi njaa, vifo na mafaa yatokeapo wakidai misaada kutoka jumuiya za kimataifa bila mafanikio, kwa kisingizio kuwa mashirika ya kimataifa yasingeweza kuisaidia Sudan kwasababu ya hali mbaya ya kisiasa.

Kwa zaidi ya miaka minne ya mateso ya njaa,vita na ukame wasudan walilazimika kula mizizi ya miti, magome ya miti, nyasi na kunywa mikojo ya wanyama ili kuyanusuru maisha yao, lakini yote hayo hayakuwa majibu ya kudumu dhidi ya uhai wao.

Jicho la Umoja wa mataifa nchini Sudan.

Hali ilivyozidi kuwa mbaya Sudan, Umoja wa mataifa uliridhia kuingia Sudan kuokoa maisha ya raia waliohitaji chakula, maji na matibabu. Ikaweka kambi za kutolea misaada katika maeneo mbalimbali kama vile Ayod, waat na Kongor. Ni wakati huo huduma za dharura za uokozi zilihitajika sana, hivyo Umoja wa mataifa ulilazimika kuanzisha "operesheni Lifeline" iliyoruhusu wapiga picha na wanahabari kutoka mataifa mbalimbali kuingia Sudan kusaidia kuripoti matukio ya maafa duniani kote ili mashirika na jumuiya za kimatifa zione haja ya kutoa msaada zaidi.

Robert Hadley amwalika Kevin Carter Sudan
Robert Hadley alikuwa afisaa mpiga picha wa umoja wa mataifa nchini Sudan,baada ya kuanzishwa kwa opersheni Lifeline iliyoruhusu wapiga picha kuingia Sudan, alimwalika Kevin Carter na rafiki yake Joao Silva kutoka Afrika kusini wakasaidie kuripoti maafa ya Sudan. Mwaliko huo uliipa sifa kubwa club ya habari ya Bang Bang waliyokuwa wakifanyia kazi Kevin na Siva huko Afrika kusini. Hata hivyo furaha ya Kevin iliongezeka maradufu kwani aliutafsri mwaliko wa Robert kama fursa ya kumfanya kufikia ndoto yake ya kuwa mpiga picha bora zaidi duniani.

Kevin Carter in nani?

Kevin Carter alikuwa mwandishi mpiga picha katika gazeti la The Star Newspaper na mwanachama wa Bang Bang club nchini Afrika kusini.

Alizaliwa na kukulia katika familia ya kikatoliki yenye msimamo dhidi ya ubaguzi wa rangi, iliyoishi daraja la pili Johannesburg nchini Afrika kusini septemba 13, 1960. Wazazi wake ni Jimmy Carter na Roma Carter waliishi maisha ya kawaida ya kubaguliwa yaliyozungukwa na mauaji ya kutisha.

Tangu akiwa mdogo, Kevin alikerwa sana na vitendo vya ubaguzi na ukatili uliokuwa ukifanywa haswa dhidi ya watu weusi na serikali ya makaburu pamoja na kuwa yeye hakuwa mtu mweusi.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita miaka ya 1980, Kevin Carter alichagua kuwa mfamasia, na badae kujiunga na jeshi akalitumikia kwa zaidi ya miaka mitatu. Akiwa jeshini, alitumia fursa hiyo kupambana kuzuia ukatili na ubaguzi uliofanywa na makaburu enzi hizo. Siku moja alishuhudia mtumishi mweusi katika bwalo la chakula la jeshi akitukanwa hadharani, alipoingilia kati kumtetea aliambulia kipigo na kuumizwa vibaya sana.

Kevin aliwahi kukamatwa na kufungwa mara kadhaa kutokana na harakati zake za kupinga ubaguzi na ukatili dhidi binadamu wenzake.

1983 akiwa jeshini alishuhudia tena shambulio la kanisa moja mjini Pretoria lililosababisha mauaji na uharibifu mkubwa, hali hiyo ilimsukuma kuamua kufanya kazi ya upiga picha. Na alianza kama mpiga picha za michezo lakini haraka haraka alitumia fursa hiyo kuanika ukatili mkubwa wa makaburu, jambo ambalo kwake lilizidisha haja ya kupambana kuleta usawa. Ni kipindi hiki pia Kevin alijiunga na gazeti la The Star Newspaper na Bang Bang club.

Kevin Carter akwama Nairobi.

Kutokana na shauku kubwa ya kukuza uwezo wake kwenye upiga picha, baada ya mwaliko wa Robert, Kevin Carter alianza safari mara moja bila kupoteza muda akiwa na rafiki yake Silva.Wakiwa njiani Kevin na Silva walilazimika kubaki Nairobi kwa muda usiojulikana wakingoja hali ya usalama Sudan irejee kutokana na kupamba moto kwa mapigano.

Lakini badae kundi la waasi lilitoa ruhusa kwa Umoja wa mataifa kuingia kupeleka misaada Ayod. Hivyo Robert Hadley, Kevin Carter na Joao Silva waliingia rasmi Ayod Sudan 12 march 1993 wakiwa kwenye ndege maalum za Umoja wa mataifa, moja ilwabeba wao na nyingine ilibeba chakula.

Hali ilivyokuwa Ayod.

1993 Ayod ilikuwa ni miongoni mwa vijiji huko kusini mwa Sudan, kwasasa ni kata na eneo la kiutawala lililoko jimbo la Fangak Sudan kusini, Ayod inawakazi 192,937 kwa mujibu wa makadirio ya 2017 yatokanayo na sensa ya 2008 nchini Sudan, huku wanaume wakiwa ni 56.6% na wanawake 43.4%. Kata hii ina ukubwa wa eneo la mraba 13,449.

Siku iliyofuata baada ya kubaki Nairobi kwa muda usiojulikana, Kevin na wenzake waliingia Ayod na kukuta wankijiji wamejipanga barabarani wakisubiri misaada. Wamama wengi waliwaacha watoto wao maporini wakilazimika kutafuta misaada kunusuru maisha ya watoto na wao wenyewe.

Katika kutimiza wajibu wao, Kevin na Silva walitengana kila mmoja akelekea upande wake kupiga picha za matukio wakati huo ndege ikiendelea kutoa chakula maeneo hayo.

Kazi ya kupiga picha ilikuwa gumu na hatari sana hasa kwa Kevin, Kwasababu kwanza Kevin alikuwa mtu wa hisia sana, hivyo kuna wakati alikuwa akiingiwa na huruma sana aliposhuhudia maafa na mateso waliyopata watoto, wamama na wababa. Pili kwasababu UN walipewa ruhusa na Kundi la waasi, walipangiwa muda wa kukaa mahali kutoa misaada. Pia wapiga picha wasingeweza kupiga picha badhi ya maeneo bila ruhusa na usimamizi wa kamanda wa Waasi na bahati mbaya zaidi lugha waliyotumia Waasi ni kiarabu na Kevin na mwenzie Silva walizungumza kiingereza.

Kamera ya Kevin yasababisha gumzo la duniani.

Wakati akipiga picha hapo Ayod, Kevin alifanikiwa kumuona mtoto mdogo aliyepewa jina Ken, umbali wa mita hamsini kutoka alipokuwa amesimama. Ken alishindwa kuendelea na safari yake ya kuwafuata walezi wake waliokuwa wameenda kupokea chakula katika kituo cha karibu cha misaada umbali wa kilometa moja na nusu.

Ken alianguka porini kutokana na njaa Kali, jua Kali liliowaka kwa nyuzi joto 40°c, kiu ya maji na mwili kukosa nguvu. Akijaribu kuficha kichwa chake ardhini ili asiungue na jua maana hapakuwa na miti eneo hilo, miti yote iliisha kwa ukame na kuliwa na binadamu kama chakula. Ken hakujua kuwa nyuma yake kulikuwa na ndege aina ya tai(vulture) mla mizoga akimunyemelea afe ili amle nyama kama alavyo mizoga.

Ni wakati huo Kevin Carter aliseti kamera yake vizuri ili aweze kuchukua picha ya mtoto Ken akinyemelewa na tai. Baada ya kupiga picha hiyo tai akiwa umbali wa mita kumi hadi ishirini kutoka alipokuwa ameanguka Ken. Kevin alilazimika kukaa dakika ishirini zaidi ili aone kama tai huyo angeweza kurusha mbawa zake kumsogelea mtoto, lakini tai hakusogea.

Baada ya muda kidogo, kwasababu ndege za UN ziilipangiwa muda wa dakika thelathini tu za kuhudumia Ayod, ndege hizo maalum zililazimika kuicha Ayod na kwenda kituo kingine cha Kongor, hapo Kevin hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kumfukuza yule tai na kuondoka na akamwacha Ken bila msaada zaidi. Toka hapo picha ile ikawa inaisuta nafsi yake na hatimaye aliamua kumshirikisha rafiki yake Silva.

Kwa mara ya kwanza 26 march 1993, gazeti la The NewYork Times lilichapisha picha ya mtoto akiwa amesogelewa na tai mla mizoga iliyopigwa na Kevin Carter. Picha hiyo iliibua hisia kubwa duniani kote, na kupelekea gazeti hilo kupokea simu na barua pepe nyingi za malalamiko yakimlenga mpiga picha kwa kushindwa kuokoa maisha ya mtoto badala yake akajali kazi yake na kumuacha mtoto akiuwawa na tai porini.

Alipoulizwa Kevin kuhusu kutomsaidia mtoto, alisema hakujua kuwa tai huyo angemshambulia mtoto Ken. Katika utetezi alisema alipoona tai ametua nyuma ya mtoto umabali wa kama zaidi ya mita kumi alilazimika kusbiri kwa dakika ishirini kuona kama tai angemsogelea Ken, lakini haikutokea hivo, na alipolazimika kuondoka eneo hilo aliamua kumfukuza tai akaondoka akimwacha Ken chini.

Japokuwa chini ya kapeti ni kwamba Kevin alitekeleza kazi aliyotumwa na mwajiri wake, aliambiwa akifika Sudan apige picha asifanye kazi ya kuokoa watu, maana haikuwa kazi yake.

Mjadala huu uliwaibua wataalam na wachambuzi wa mambo ya picha za habari wakidai kuwa, Kevin alikuwa sahihi kutomsaidia mtoto kwani kitaalamu picha isingeleta uhalisia kama mpiga picha angeamua kuacha kazi yake na kuwa sehemu ya tukio.

Kwa mujibu wa Silva mpiga picha aliyeambatana na Kevin Sudan, anasema aina ya uchukuaji wa picha pia ilichangia watu kuona kama tai alikuwa karibu sana na mtoto, kumbe sio kweli, kwani umbali kutoka alipokuwa mtoto na mpiga picha ilikadiriwa kuwa na mita zaidi ya kumi, kwahiyo ilimlazimu mpiga picha kusogeza lens ili picha ionekane vizuri. Na alifanya hivyo kwa kuogopa kuwa angesogea karibu zaidi tai angepaa na kuondoka. Hivyo asingeweza kuripoti uhalisia wa tukio.

Kazi ya mikono yamuweka kileleni Kevin
Pamoja na gumzo kubwa kuhusu picha aliyopiga Kevin, Gazeti la The New York Times lilimuzawadia Kevin kitita cha pesa kwa kupiga picha bora zaidi ya habari iliyosomwa na watu wengi duniani.

Na ilipofika 12 April 1994 katika mwezi na mwaka ambao baba wa taifa la Afrika kusini aliingia madarakani baada ya kuipatia Afrika kusini uhuru wake kutoka kwa Makaburu. Kevin Carter alitambuliwa rasmi na kupewa tuzo ya upiga picha bora zaidi duniani na taasisi kongwe na maarufu ya Pulitzer.

Majuto ni mjukuu.

Tofauti na matarajio ya wengi hasa inapokuja fursa ya kutambuliwa kwa kazi tunazozifanya kwa kupokea pongezi na tuzo kwa mbwembwe, kwa Kevin tuzo ile ilimfanya ajute na kukosa amani badala ya kufurahi.

Kevin alizidi kuishi kwa sonona na kujilaumu kila mara kwa kushindwa kuokoa maisha ya mtoto Ken aliyedhaniwa kuuwawa na tai bila msaada wake. Katika kuonesha majuto yake pamoja na kuwa yeye mwenyewe hakuthibitisha habari ya kifo cha mtoto Ken, Kevin alilazimika kuiomba radhi dunia akisema, "kwa kweli ninaomba msamaha kwa kushindwa kuokoa maisha ya mtoto Ken"( iam really really sorry, I didn't pick the child up)

Hatimaye sumu yaamua hatima ya Kevin
Akiwa na umri wa miaka 33 tu, Kevin Carter alifanya maamuzi magumu, alirudi Jijini Johannesburg, mkoani Gauteng katika kitongoji cha Parkmore alikozaliwa, kukulia, kucheza, kusomea na kufanya kazi akiwa mdogo.

Akiwa huko 27.7.1994 miezi minne tu baada ya kutunukiwa tuzo ya upiga picha bora zaidi duniani, aliingia ndani ya gari akafunga madirisha yote, akachukua Mpira wa maji akauchomeka kwenye eksosi ya kutolea moshi wa gari na upande mwingine wa mpira akaupitisha kwenye upenyo wa dirisha la dereva, akawasha gari akiwa ndani, moshi wenye sumu ya kaboni monokisaidi ukamuuwa Kevin kwa utulivu kabisa.

Kabla ya kujiua Kevin, aliandika na kuacha ujumbe kwenye kipande cha karatasi uliosomeka hivi. Maumivu ya moyo yanazidi furaha ya pesa, najisikia vibaya sana.... Kumbukumbu za mauaji,njaa na mateso ya mtoto Ken zinanijia kila mara. Naenda kumfuata na kumuomba msamaha kama nitapata bahati ya kufanya hivyo.(The pain of heart overweigh the joy of money, iam so depressed... iam haunted by the vivid memories of killing, hunger and pain of starving child Ken. I have gone to join him and ask for forgiveness if that opportunity arise.)

Je huyu Ken ni nani?

Ken ni mtoto mgonjwa wa utapiamulo na mhanga wa maafa ya baa la njaa Sudan miako ya 90, alyeishi katika eneo la Ayod Sudan kwa kula nyasi, mizizi ya miti, magome ya miti na alikunywa mikojo ya wanyama ili kulinda uhai wake. Ni katika harakati hizo pia Ken alipoteza wazazi wake wote kwa njaa, na yeye akalelewa na ndugu na jamaa.

Ken alipata umaarufu mkubwa duniani kutokana na mazingira ya maisha yake yaliyomlazimisha abadilishiwe jinsia, jina na kubwa zaidi alibambikiwa kifo akiwa hai.

Ken akutwa akiwa hai.

The NewYork Times, gazeti maarufu marekani na dunia nzima, liliamua kutuma timu ya wataalamu kwenda kuusaka ukweli kuhusu kifo cha kusitaajabisha cha mtoto Ken nchini Sudan. Aliyedaiwa kufa porini kwa kudonolewa na tai utosini wakati akijikokota kuwafuata walezi wake kwenye kituo cha msaada.

Akisimilia kwa hisia kali kuhusu Ken, Frolence Mourin aliyekuwa mratibu wa kituo cha msaada wa tiba kutoka taasisi binafsi ya Ufaransa iliyoitwa Travail dans ce dispensaire(makeshift dispensary) Alikiri kumtambua Ken na alisajiriwa kwa namba T3 hapo kupata matibabu ya utapiamlo na alipopona alichukuliwa na kituo cha msaada ya chakula cha Umoja wa mataifa na kulelewa huko.

Timu ya wataalamu hao ilibidi ipige hatua mpaka Ayod mahali alipolelewa Ken, huko walifanya mahojiano na wanakijiji wengi akiwemo mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mary Nyaluak aliyetumika kugawa chakula enzi hizo za baa la njaa kwenye kituo cha Ayod. Mary alimtambua mtoto Ken na kusema kuwa Ken alikuwa mvulana na sio msichana kama ilivyodhaniwa, jina lake halisi aliitwa Kong Nyong wakati huo aliishi nje ya kijiji kile kwa walezi wake.

Baada ya Siku mbili timu ya wataalamu ilibahatika kukutana na mlezi wa Kong Nyong(Ken) alithibitisha kumtambua Ken na alisema jina lake ni Kong Nyong pamoja na Mungu kumuepushia kifo wakati wa dhiki kuu ya njaa, jua kali, kiu ya maji, vita, na utapiamlo akaendelea kuishi na kulelewa katika kituo cha msaada cha Umoja wa mataifa kwa miaka 14 baade, Kong alikuja kufariki mwaka 2007 kwa homa.

Wahenga walinena: harakaharaka haina baraka
Ubinadamu ni wakati dhamiri/nafsi inaendesha mwili, mwili hauwezi kuendesha dhamiri/nafsi ila hushawishi maamuzi na matendo kupitia mifumo yake ya fahamu. Na uwepo wa mwandamu katika maamuzi na matendo upo wa aina mbili, yaani mantiki na hisia/mhemko.

Hivyo uchaguzi wa kuamua vema au vibaya unategemea na nini kitakutawala wakati unachukua hatua juu ya jambo lolote lile unalokumbana nalo. Hisia inaweza kukunyima nafasi na muda wa kujua maana na matokeo ya utakachokifanya lakini mantiki itakupa subra na tahadhari ya kuona nini kitakuja baada ya unachopanga kukifanya.

Kevin aliruhusu hisia zikatawala maamuzi yake badala ya kujipa muda wa kuthibitisha kifo cha Ken(Kong Nyong). Akaihukumu nafsi yake bila kuipa muda wa kujitetea. Ikazima nafsi yake ghafla, mwili nao ukapoa ghafla, Kevin akafa kwa kafara asilolijua, akiahidi kwenda kukutana na kumuomba msamaha Ken peponi akidhani ametangulia kumbe alimwacha duniani.

Ama Hakika kesho ya mwanadamu ni giza, laiti kama ingeweza kuonekana kila mmoja wetu asingekubali kupita njia hiyo asiyoijua kabla ya kifo chake.Asante Mungu kwa kutupa KevinCarter, asante pia kwa kutung'anya Kevin akiwa bado kijana mdogo. Ameen.

Ukinakili kazi yangu kumbuka kufanya acknowledgement.

Copy rights of this article reserved
Written by Bahati Samwel
Kwa mawasiliano zaidi:
0674533881
0759043332.
FB_IMG_1560933428064.jpeg
 
0759043332.View attachment 1131447
Download Image
INA SISIMUA AMAKWELI TUSIJIHUKUMU
 
Back
Top Bottom