Nas Mapesa
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 5,286
- 5,423
Kubwa likifanya uaminifu ukafa ni ishu ya ruzuku nothing else
kiukwl cjaelewa point yako mpak ss? jaribu kwnd mojakomoja kwny point ueleweke!Zitto Kabwe, Mwanasiasa makini kama alivyo, mwenye upeo kama alivyo, mjenga hoja kama alivyo. Wengi walitamani aendelee kuwepo CHADEMA lakini baadae ilishindikana.
CHADEMA hawakuwahi kumuamini. Chanzo cha ugomvi wao ni kwamba Zitto alikuwa anawauza. Waliamini kuwa alikuwa na urafiki wa karibu na Rais aliyepita.
Inawezekana ndio maana Zitto hakuwahi kutoa post nyingi mfululizo za kumchapa Rais aliyepita moja kwa moja kama anavyofanya katika utawala huu.
Alideal zaidi na skendo za Bunge ambazo hazikuwa na athari kubwa kwa Rais moja kwa moja zaidi ya zile ambazo zilikuwa zinamtaka Rais afanye mabadiliko. Hata alipoondoka CHADEMA wenye Chama kile Waliamini kuwa Zitto angekuwa mpinzani wa wapinzani.
Ilianza kuonekana alipobaki bungeni wakati wenzake walipotoka nje siku Rais wa sasa alipokuwa akifungua bunge. Na Rais huyu alimsifia kuwa alikuwa mpinzani wa kweli.
Hata hivyo dakika moja baada Rais wa sasa kutoa mguu wake bungeni na kuanza kazi ya Urais ni wazi kwamba amejitofautisha sana na Rais aliyepita kimisimamo na kifikra. Kabla safari haijafika mbali, Zitto amekuwa mpinzani hasa wa moja kwa moja dhidi ya Rais wa sasa.
Anapost mara nyingi zaidi. Na kama ilivyo kawaida yake, Anapost mantiki sana. Hata kihisia anaonekana kuwa mpinzani halisi na ameonja machungu ya utawala huu. Kafungiwa vikao vya bunge. Kasakwa na polisi usiku na mchana.
Dakika za mwisho za utawala uliopita mambo haya yasingemtokea Zitto. Mantiki ya kijinga ya makala hii ni kuwaza tu kama Rais wa sasa angeingia madarakani baada ya kuondoka tu kwa Rais Ben Mkapa huenda Zitto angekuwa bado CHADEMA. Mapambano anayopitia sasa Zitto ndio ambayo CHADEMA wamepitia utawala uliopita na watapitia utawala huu. Wasingeishi kwa hofu ya kutoaminiana, kuonana wasaliti kwa system, mpaka wakafukuzana mahakamani.
Adui yao angekuwa mmoja. Lakini katika utawala uliopita Zitto na CHADEMA waligeuzana maadui badala ya kumtazama adui. It's too late. Unavyodhani, Zitto wa leo Ukawa wakitoka nje ya bunge yeye atabakia ndani?.....
CHANZO: UKurasa wa FB: Edo Kumwembe.
Hebu tuambie Zitto alinufaika na nini utawala uliopita?Zito mwanasisa anayependa anufaike kwa njia moja au nyingine utuwala wa jk zito alikua swahiba yake na alikua akinufaika sana na serikali iliyopita sasa huu utawala wa magu hauna hayo lazima watalalama saana
Edo ni mtu makini sana. Natamani wanaume wote wa JF wangekuwa kama yeye.
Wiki iliyopita nilinukuu maneno ya Condolezza Rice "We need a Common enemy to Unite Us". Udikteta na Ufashisti umekuja kama Zawadi.
Next time edo azungumze kuhusu lowassa na chadema abalance
Hata wenyewe wanajuaZitto amewaacha mbali sana Chadema kwa hoja...
Chadema hawana hoja yoyote zaidi ya kususia bunge na maandamanoHata wenyewe wanajua
Agenda ya Zito ni kujipambanua kama mwanasiasa wa upinzani, chama chake kina taswira hasi kwa jamii ya wanaharakati na kinatanabaishwa kama CCM kuna fursa ya kukua kaiona anataka upesi atumie nafas iliyijitokeza kuipiku CUF. kumbukeni mgogoro wa kutoeleweka kwa EL si jambo lililokwisha lipo na linanyata. huwenda Mzee akashinda vita kwan kampeni zinaendelea za kuunda mtandao na hapo ndipo palipovuka soksi kiatu kikabaki.
EDO ni mchache sana. anajua alichojulishwa tu! haya mambo yapo above the pay grade ya wengi humu.
. Mada ni jambo jingine usemayo jambo jingine.Chadema hawana hoja yoyote zaidi ya kususia bunge na maandamano
mi naic sabab kubwa iliyomfukuza zzk ndan ya cdm ni kuutaka uenyekit wa mkubwa kutangaza kugombea urais na kufuatilia mianya ya mkubwa ya kupigia pesa zingine ni figisu tuPengine Zito angekuwa bado yupo chadema kama angelitoka mkapa na kimuachia magufuli
Wachache watamuelewa eddo hapa
Eddo is really genius
Thibitisha kama kumwembe ni mtu makini, na thibitisha kama wanaume wote wa jf si makini!Edo ni mtu makini sana. Natamani wanaume wote wa JF wangekuwa kama yeye.
Hilo unaweza ukalifanya hata wewe, yeye ameshafanya aliwezalo.Next time edo azungumze kuhusu lowassa na chadema abalance