mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Zitto Kabwe, Mwanasiasa makini kama alivyo, mwenye upeo kama alivyo, mjenga hoja kama alivyo. Wengi walitamani aendelee kuwepo CHADEMA lakini baadae ilishindikana.
CHADEMA hawakuwahi kumuamini. Chanzo cha ugomvi wao ni kwamba Zitto alikuwa anawauza. Waliamini kuwa alikuwa na urafiki wa karibu na Rais aliyepita.
Inawezekana ndio maana Zitto hakuwahi kutoa post nyingi mfululizo za kumchapa Rais aliyepita moja kwa moja kama anavyofanya katika utawala huu.
Alideal zaidi na skendo za Bunge ambazo hazikuwa na athari kubwa kwa Rais moja kwa moja zaidi ya zile ambazo zilikuwa zinamtaka Rais afanye mabadiliko. Hata alipoondoka CHADEMA wenye Chama kile Waliamini kuwa Zitto angekuwa mpinzani wa wapinzani.
Ilianza kuonekana alipobaki bungeni wakati wenzake walipotoka nje siku Rais wa sasa alipokuwa akifungua bunge. Na Rais huyu alimsifia kuwa alikuwa mpinzani wa kweli.
Hata hivyo dakika moja baada Rais wa sasa kutoa mguu wake bungeni na kuanza kazi ya Urais ni wazi kwamba amejitofautisha sana na Rais aliyepita kimisimamo na kifikra. Kabla safari haijafika mbali, Zitto amekuwa mpinzani hasa wa moja kwa moja dhidi ya Rais wa sasa.
Anapost mara nyingi zaidi. Na kama ilivyo kawaida yake, Anapost mantiki sana. Hata kihisia anaonekana kuwa mpinzani halisi na ameonja machungu ya utawala huu. Kafungiwa vikao vya bunge. Kasakwa na polisi usiku na mchana.
Dakika za mwisho za utawala uliopita mambo haya yasingemtokea Zitto. Mantiki ya kijinga ya makala hii ni kuwaza tu kama Rais wa sasa angeingia madarakani baada ya kuondoka tu kwa Rais Ben Mkapa huenda Zitto angekuwa bado CHADEMA. Mapambano anayopitia sasa Zitto ndio ambayo CHADEMA wamepitia utawala uliopita na watapitia utawala huu. Wasingeishi kwa hofu ya kutoaminiana, kuonana wasaliti kwa system, mpaka wakafukuzana mahakamani.
Adui yao angekuwa mmoja. Lakini katika utawala uliopita Zitto na CHADEMA waligeuzana maadui badala ya kumtazama adui. It's too late. Unavyodhani, Zitto wa leo Ukawa wakitoka nje ya bunge yeye atabakia ndani?.....
CHANZO: UKurasa wa FB: Edo Kumwembe.