Keissy alianzisha tena bungeni

sijakuelewa hapa. unataka tena muendelee kubebwa hata kwa baraza lenu la mawaziri lije huku bara kula posho? hivi hamtosheki na hawa akina nahodha vuai, dr.hatib, dr. mwinyi, dr. bilal na wengineo wengi wanaokula ruzuku za wabara bila ya kuzitolea jasho? maajabu haya.
masikini tanganyika yangu.

 
haswaaaaaaaaaa! kapiga mule muleeee.. watu wala mifedha ya bureeee...

eti kisa wazanjibaliiii
 
Kwangu mimi huyu MHs.Kessy ni MTANGANYIKA wa kweli....hakuna kumung'unya...mwizi aitwe mwizi.......!

Iti izi veri anifotuneti ukisema ukweli ndani ya CCM utaundiwa mizengwe. Tayari walishaanza kumbagua kwa ngozi yake ndani ya jengo la bunge kwa kumuita mwarabu. Sasa ina maana ni jana ndiyo wamegundua kuwa Kessy ni mwarabu? Ina maana hata kama ni mwarabu, je hakukidhi requirements za kuwa mbunge? Ifu dhati izi e kes, samuani slepti on dhe swichi kupitisha jina la Kessy kuwa mgombe ubunge, na mamlaka inatakiwa kuhojiwa kwa hilo. CCM inatumia resi kadi kutugawa watanzania eti kwa sababu tu umehoji mamlaka au kusema kile ambacho utawala haupendi kusikiliza.
 
Watanganyika tumezidi kujipendekeza! Hata deni la Taifa la hizo Trilion 30+ ni zigo lako ewe Mtanganyika!
 
Asante Mh. KEISSY kwa kutufungua sisi wa Tanganyika. Tafadhali endelea kutuamsha. Nilikuwa sifahamu ya kuwa Zanzubar ambayo ni ndogo kuliko DSM na ina watu wachache kuliko vDSM ina wabengu 83 kwenye bunge la jamhuri. Wakati DSM inawabunge 5 wa kuchaguliwa. Sina uhakika kama wa viti maalumu wanafika 10. Sasabu wao hawalipi gharama za bunge la jamhuri ndio maana kila siku wanazid kuongeza majimbo. Ukweli mchungu ila ujumbe umefika
 
Mawazo kama ya KESSY hamuwezi kuyamaliza kwa kupigana naye nje ya Bunge yeye ndivyo anavyoamini hata upande mwingine mwa shilingi wanasema Tanganyika imevaa koti la muungano.Rasmu ya katiba ya Mzee Warioba iliweka misigi mizuri ya kumaliza dukuduku kama hizo.Mambo yote ni serikali tatu kama ilivyoainishwa na kamati ya Mzee Warioba hata ukisoma kitabu cha Dr Mwakyembe kinafafanua vizuri dukuduku za akina Kessy na Duni suala ni serikali tatu.Mwl OLUOCHI amewambia hata katiba yetu ikipinda haitashi zaidi ya miaka 10.Tunahitaji Zanzibar na Tanganyika zenye serikali kamili si ujaja ujanja wa akina LUKUVI na WASIRA.Malikia miaka mingi alikuwa na mawazo mgando lakini kabla mwezi huu haujaisha tegemea kupata SCOTLAND huru.SITTA,LUKUVI,WASIRA mpo hapo
 
Hapa ndo naona ujanja wa Wazanzibari kila siku wanataka Zanzibar huru kumbe wazushi tu wanataka kutufunga macho ili tuendelee kuwabeba.Ukiwapa makavu kama kessy wanakuja juu.Nilitegemea Wazanzibar wangetumia ule mwanya wa wao kudai wa kinachoitwa Zanzibar huru.Badala yake wanaleta hadithi za udugu.Mi naona wazanzibar wametuzidi janja na kila tukistua janja yao wanakuja juu.Big up Kessy
 
Kessy ana akili sn. Anajua watanganyika hawajui namna wanavoilisha na kuihudumia km nguruwe mijitu mizima hii kutoka zenji. Watngnyk wanaendelea kuelewa wanavyohadaiwa na viongozi/wapigadebe wa ccm/mafisadi.
TUTAWAHUKUMU KWA MANENO NA MATENDO YAO. ACHA WAENDELEE KUTEKETEZA MABILIONI YA WATANVANYIKA
 
Salaam Mh Keissy

Mh tunakusikia na ahsante kwa kuongelea Watanganyika wasio na kipaza sauti wala nchi yao.

Hao wznz wapo Dodoma ni watalii tu, tofauti na wale wa Ngorongoro hao wanachukua dola tu

Mh Znz haichangii gharama za JMT ambazo kwa mbunge ni sh 15,000 kwa mwezi kwa kila mmoja kwa wabunge 84 wanaokuja kuwakilisha nchi yao lakini wanalipwa na nchi ya Tanganyika. Jumla kwa wanakula Bilioni 126.

Kila mmoja anakula milioni 30 za mfuko wa jimbo. Pesa hizo ni za Watanganyika.
Ukichanganya wabunge 84 kutoka nchi ya znz wanachukua na kupora zaidi ya bilioni 200

Ukiona wanataka kumpiga Keissy ni waoga, siri ya kupora na wizi imetambulika.

Mbunge wa znz anapokuja kuchukua pesa za kwenda kutibiwa London kutoka Tanganyika ni wizi na uhuni.

Wao wana SMZ ndio iwahudumie kwenda kutoa chunusi za wake zao India, si pesa za Mtanganyika.

Hawachangii muungano, wanapora, tuwaambie ukweli
 
Hoja hujibiwa kwa hoja sio ugomvi,wazanzibari walipaswa kumjibu Bw. Kessy!Yaani watanganyika wote waliokuwepo walishindwa kuona hoja yake au ni kujitoa akili tu.
 
miaka 50 ya kudanganyana ifike mahali tuwe wakweli ccm wamezoea vya dhuluma hawawezi kuishi ktk ukweli ..huyu mzee Nkasi namuunga mkono hatuwezi kubeba mzigo uliobebeka tena kila mtu ababe mzigo wake hawa wanzazibar tunalisha kwa pesa zetu hawana faida yoyote kwetu... back tanganyika
 
Huwezi kuamini mimi inaniuma nikiona Mzanzibar anakunywa pombe zetu raha mstarehe, wanasababisha hata ongezeko la bei ya bia hawa
 
Nawaambieni in case ameukwaa urais, haikosi tutagombana na mataifa ya magharibi yanayotudhulumu rasilimali zetu kwa rushwa wanazowapa viongozi wetu na kujibebea madini,pembe za wanyama,n.k.
 

tatizo wewe ni mr.zero ni sawa na mtoto mchanga
 

Usimsingizie Mwenyezi MUNGU kwenye hili Mkuu! Alitupatia uwezo wa KUTAMBUA MABAYA NA MEMA.....Tafakari!
 

kwani huyo babu yako kambarage hakuliona hilo au ndio yeye hana akili mwenye akili ni wewe na huyo mshihiri mbovu anataka kuolewa wa wanaume waloshiba. karume ndio aliyekuwa makamu wa rais huu muungano ulipoasisiwa sasa kama tunachangia hatuchangii maswala hayo akamuulize babu yake nyenyere kule butiama mshamba mkubwa huyu. na ndio maana huitwa wangese watu kama nyie
 
Hivi naulizia huyu CCM aliyekurupuka wakati jua linakuchwa ni kweli anauchungu na Tanganyika na zaidi kuwa gharama nyingi zinatumika kuibeba Zanzibar na kama haitoshi alidai hata hela ya mishahara ya Wazenji inatoka Tanganyika ,inawezekana wamo wengi wenye hisia kama zake kuwa Zanzibar ni mzigo.

Okay ,waheshimiwa wa sampuli ya Ali Kesi bila ya shaka wapo wengi ,Je kura zao zinaweza kuikwamisha Katiba ,Je inawezekana wakaingia mitini siku za kupiga kura ili kuonyesha Uzalendo wao wa kutokubaliana na Katiba inayoibeba Zanzibar ?

Au hizi ni sanaa na utamaduni unaoonyweshwa na ccm wahindi wanaita DRAMA ,mchezo umekuwa arranged pengine bila ya vibaraka kutoka Zanzibar kuelewa kinachochezeshwa ,jambo ambalo limewafanya vibaraka hao nao kuwa eti wakali na wamekasirika kweli kiasi ya kwamba wapo tayari kumpiga au kupigana na Ali ,ni sanaa na uigizaji mtupu ,uzalendowa kweli tumeuona kwa akina Ukawa ,hawa akina Ali kama kweli wanaionea huruma Tanganyika basi kinachohitajika ni kuachana na bunge hilo mara moja au wakati muafaka ukifika basi hapo tutawakubali ila kwa michezo hii ya kuigiza itakuwa wanajitekenya wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…