KCMC ikaangoni

Hii ndio tunaita Ethical dillema. Unamtoa ndio uokoe uhai wake ila hajaridhia na hakuna ushahidi kuwa ingemletea hatari kwenye uhai wake. Ni ngumu kweli kweli.
Hii ndio tofauti ya fani ya upasuaji na fani za kungojea miongozo. Unajua kabisa, bila upasuaji hapa, huyu mgonjwa haponi, lakini fani za taralila wanaanza kupinga pinga.​
 
Hii ndio tofauti ya fani ya upasuaji na fani za kungojea miongozo. Unajua kabisa, bila upasuaji hapa, huyu mgonjwa haponi, lakini fani za taralila wanaanza kupinga pinga.​

Nadhani hao mabingwa wa upasuaji wana miongozo yao kwamba ikitokea umekutana na emergency kwenye procedure ambayo ni life threatening inawapa ruhusa ya kuondoa kumuokoa mgonjwa.
 
Wamrudishie kizazi chake au wamekitupa?!
 
Kuna kitu nimejifunza hususani Kwa wazungu hasa kwenye mahakama zao usimfanyie mtu wema bila ridhaa yake, ni bora umwache afe au lolote limkute sababu akipata tu kupona anakushitaki na unamlipa fidia.
 
Binadamu ni kigeugeu
Just imagine kuna mtu alimsaidia mdada kwenye ajali kabla ya gari kuwaka moto yule dada alivyopona alimshtaki kuwa alikuwa na poor handling imemsababishia kupata tatizo la mguu na anataka kulipwa dollar laki nane! Wakati kama jamaa asingemuokoa yule dada alikuwa anakufa kwenye gari.
 
Watu wengine katika dunia, wanatumika kama case study, kwa wengine kujifunza na kutokurudia hayo makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…