Kazi zipo ila ajira hakuna

Kazi zipo ila ajira hakuna

Mkuu umesema kweli, hii fursa inaniweka mjini Sasa. Ila wa Kenya wapo mbali sana. Pia Tanzania naona internet Ni changamoto hasa Kama unatumia Skype.
Tupeane maujuzi mkuu.mi natamani sana kuuza kozi zangu huko pia
 
Hii nimeikuta sehemu.

WANAOPIGIA UPATU KUJIAJIRI WAPO TAYARI KUACHIA AJIRA ZAO?

Hivi karibuni kumeibuka wimbi la mashirika mbali mbali, taasisis binafsi na hata watu waliopo serikalini kusisitiza kijana kujiajiri. Kuna maswali mengi ya kujiuliza, Je, wanataka vijana waliohitimu shule mwaka huu wakajiajiri, wao wamejiajiri? Mashirika binafsi na wanaharakati mbali mbali shughuri zao nyingi kwa nini zinategemea wahisani na wafadhili? Watumishi wa serikali na wanasiasa kwa nini wao wameajiriwa na hawako tayari kuachia nafasi zao na kwenda kujiajiri? Hili ni suala linalohitaji mjadala mpana sana ili kuyabaini mazingira yanayopelekea uhitaji na au utegemezi wa kuajiriwa. Hizi elimu za watu kujiajiri natamani sana kuona zikitolewa na watu ambao wamejiajiri kweli. Maana hawa watakua mfano sahihi wa kuigwa. Pia tungekuwa na mfumo wa kubadilishana ajira miaka mitatu unakaa benchi unajiajiri unampisha yule alioko benchi ili tupime uhalisia. Lakni Utakuta wanaozungumza haya wameanzisha NGO zinadai fedha kwa wafadhiri, zinapeleka asilimia mbili kwa jamii asilimia 98 utaambiwa ni matumizi ya kawaida halafu zinapigia upatu kujiajiri wakati hizo NGO watu wake wameajiriwa.
Lakini pia wanasiasa wanalipwa posho mzigo wameajiriwa na wananchi kwa kodi za walala pu halafu wao wanataka kijana aliyetoka SAUT au MZUMBE jana ajiajiri. Wanaharakati wana NGO, ni waajiriwa halafu wanataka kijana aliyemaliza chekenya sekondari ajiajiri.
Sio mbaya lakni inahitaji mjadala mpana na maandalizi makubwa sana ya kimfumo. Mfumo wa kielimu, mfumo wa kibenki na mfumo wa kijamii. Mfumo wa kielimu kwa sababu tunapaswa kuitazama elimu yetu kama ina kidhi haja ya kijana kujiajiri mara tu anapohitimu elimu yake. Mfumo ya kibenki kwa sababu kujiajiri kunahitaji mtaji. Kijana aliyehitimu leo hii shule ni dhahiri hatakuwa na uwezo wa kuendesha hata Kilimo chenye tiba. Hivyo lazima kuwepo mfumo sahihi ya kibenki itakayomuwezesha kijana kuweza kupata mtaji. Kwa upande wa jamii, jamii ina fikra kuwa njia sahihi ya kufurahia matunda ya elimu ni kuajiriwa. Sasa Je, jamii ina ufahamu na uwezo kiasi gani wa kuyatengeneza mazingira ya kijana kujiajiri?
Hakuna taifa lolote duniani linalopigia upatu mfumo wa kujiajiri wakati ambapo halijaweka mazingira sahihi ya watu kujiajiri ikiwemo utoaji wa vocational trainings yani elimu ya stadi za maisha na ufundi, mazingira ya utafiti na ugunduzi pia hapo chini. Lakni pia inaangaliwa secta binafsi katika kuchangia ongezeko la ajira na namna gani inatoa mwanya wa watu kuweza kujiajiri.
Cha kustaajabisha watu wamegeuka kuwa wateule na kuwatupia lawama kijana kuwa eti hawafanyi kazi kwa maana ya kujiajiri na hivyo kulalamikia suala la ajira. Lakini mtu huyo huyo ukimwambia aachie nafasi aliyoajiriwa nayo halafu tumtathmini baada ya mwaka mmoja tuaweza kushuhudia akiwa ameathirika kwa maradhi ya sonona. Wako viongozi wasomi wakubwa walipovuliwa nyadhifa zao walisikika wakiomba radhi kwa wateule kuwa familia zao zinawategemea. Wako wanasiasa waliosikika wakishukuru wametolewa matopeni. Kwa nini washukuru au waombe radhi kutetea ajira zao hali ya kuwa wao ni wasomi wabobezi. Bila shaka kuna tatizo katika mfumo wa ajira usio rasmi. Hivyo, vijana wa taifa hili wanahitaji kusaidiwa ili kuzifikia fursa na sio kutupiwa mzigo wa kujiajiri wakati mazingira ni magumu.

Sure Mkuu...Kujiajiri ndio mpango mzima katika dhama hizi.
 
Naomba niwajibu wote kwa pamoja mnaofikiri kwamba mimi nimeajiriwa ...
Nikiwa mdogo (chini ya miaka 14) nilikuwa na uwezo wa kutengeneza vikapu - entukuru na kupeleka minadani. Haikutosha, nikawa nafuga kuku wa kienyeji, nauza mayai na kuku pia. Shughuli hiyo niliendelea nayo hadi nilipomaliza elimu ya msingi na kulazimika kwenda sekondari - bweni.

Wakati nikiwa sekondari, likizo zangu zote nilirudi kijijini kuendelea na mchakato huo huo. Hivyo kwenye kukua kwangu nilizoea mzingira ya kujitafutia pesa za kwangu binafsi kwa ajili ya matumizi yangu. Wazazi waliwajibika kulipa karo (japo ilikuwa kidogo) pamoja na matumizi mengine ya lazima pindi niwapo shuleni.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, nilijiunga moja kwa moja DarTech (kwa sasa inaitwa DIT); nikiwa hapo nilikuwa nachukua bidhaa toka mipakani Tunduma na Mtukura na kuwauzia wamachinga kwa bei ya jumla; wao wanaingiza mtaani na kupata faida. Baadaye nikapata mchongo wa kwamba chuma chakavu kina soko nchini Kenya - mnunuzi mzuri alikuwa anaitwa Mkole (sijui kama bado yupo). Niliporudi nyumani nilinunua mzani kwa ajili ya kupima chuma - hivyo vijana wa pale mtaani walikusanya masufuria mabovu, nyaya n.k na kuleta kupima; nilimwajiri kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kupima na kutunza kumbukumbu. Akifikisha mzigo unaozidi kilo 100 nilisafiri toka Dar kurudi home ili nisafirishe mzigo kupeleka Kenya. Huko nilirudi na bidhaa za urembo ambazo niliendelea kuwauzia wamachinga.

Baada ya kumaliza chuo; sikuwa na wazo la kuajiriwa kwa kuwa tayari nilishakuwa mzoefu wa kutosa hela kwenye biashara na kupata faida. Kwa kuwa nilikuwa huru, nilifanikiwa kupata watu wenye mali ambazo zina spidi ndogo (hazitoki sana) hivyo walinipatia ili niwe na mlango wa biashara hapa Tanzania. NIliendelea na shughuli hizo na baadaye niliona kuwa shughuli za matumizi ya computer zinalipa; hivyo nilijiandikisha kufanya mitihani kwa kuwa ujuzi wa kutumia computer nilikuwa nao tayari (Nilisoma computer DarTech kama somo la ziada ambalo tulikuwa hatufanyi mtihani - miaka ya 90 hiyo).

Hadi sasa ninapoandika hivi; huwa nafanya kazi za muda; nalipwa kilicho changu naendelea na shughuli zangu. Ajira inafunga ufahamu; sio kwamba nawadanganya - hii ndiyo kweli yangu. Kwa sasa ni muelimishaji wa vikundi vya wajasiriamali; nafuga, nafanya kazi na NGO ambayo mimi ni mwanzilishi - MAISHA YANAENDA.

Ukipata ajira fanya ila usikae tu nyumbani eti unasubiri ajira wakati benk una pesa kama laki 500,000/= inaendelea kupungua kila iitwayo leo.
Mkuu naomba niunganishe na mini kwenye hayo magroup ya ujasiriamali na kama kuna whatsapp group naomba nifahamishe uniunge
 
1. Unajiajiri kwanza ili upate mtaji ....

2. Mtaji namba moja ni hiyo elimu uliyo nayo; elimu hiyo unaibadili inakuwa maarifa ... maarifa hayo unayatoa kwa wengine .. hapa kuna tatizo kidogo jinsi ya kuyatoa.
Wengi wanahitaji ku-deliver walicho nacho kichwani kwa njia iliyozoeleka .. kufundisha madarasani. Ukiandika vitabu je?
Hizi zinaitwa points za kufikirika
 
1. Unajiajiri kwanza ili upate mtaji ....

2. Mtaji namba moja ni hiyo elimu uliyo nayo; elimu hiyo unaibadili inakuwa maarifa ... maarifa hayo unayatoa kwa wengine .. hapa kuna tatizo kidogo jinsi ya kuyatoa.
Wengi wanahitaji ku-deliver walicho nacho kichwani kwa njia iliyozoeleka .. kufundisha madarasani. Ukiandika vitabu je?
1. Jiajiri kwanza ndo upate mtaji...How come mkuu, binafsi nimejiajiri na kabiashara kangu kadogo lakini sikuweza kuifanya bila mtaji, sasa unaposema jiajiri kwanza ndo upate mtaji inakuaje....??

Maana nina idea nyingi kichwani lakini bado sijafika katika nafasi ya kuziweka katika vitendo....

Hata Dr. Reginald Mengi alifanya Kazi BOT kabla ya kujiajiri vijana Acheni Majungu, Vijana tumeni maombi ya kazi kama una sifa ipo siku utatoboa!
@Troll JF Umesema vizuri sana kaka mkubwa, nimeanza kwa kujiajili lakini nisingeweza hili bila kuwa na income, sasa mtu anaposema "jiajili kwanza ndo upate mtaji"???

Mfano mtu atasema mfano wa IT atengeneze programs ambayo itampa ajira, tukumbuke iyo program yenyewe kuna software zinauzwa mtu huyu ambae hana ajira yupo tu mtaani anawezaje kununua hizo software..!!!??
 
Naomba niwajibu wote kwa pamoja mnaofikiri kwamba mimi nimeajiriwa ...
Nikiwa mdogo (chini ya miaka 14) nilikuwa na uwezo wa kutengeneza vikapu - entukuru na kupeleka minadani. Haikutosha, nikawa nafuga kuku wa kienyeji, nauza mayai na kuku pia. Shughuli hiyo niliendelea nayo hadi nilipomaliza elimu ya msingi na kulazimika kwenda sekondari - bweni.

Wakati nikiwa sekondari, likizo zangu zote nilirudi kijijini kuendelea na mchakato huo huo. Hivyo kwenye kukua kwangu nilizoea mzingira ya kujitafutia pesa za kwangu binafsi kwa ajili ya matumizi yangu. Wazazi waliwajibika kulipa karo (japo ilikuwa kidogo) pamoja na matumizi mengine ya lazima pindi niwapo shuleni.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, nilijiunga moja kwa moja DarTech (kwa sasa inaitwa DIT); nikiwa hapo nilikuwa nachukua bidhaa toka mipakani Tunduma na Mtukura na kuwauzia wamachinga kwa bei ya jumla; wao wanaingiza mtaani na kupata faida. Baadaye nikapata mchongo wa kwamba chuma chakavu kina soko nchini Kenya - mnunuzi mzuri alikuwa anaitwa Mkole (sijui kama bado yupo). Niliporudi nyumani nilinunua mzani kwa ajili ya kupima chuma - hivyo vijana wa pale mtaani walikusanya masufuria mabovu, nyaya n.k na kuleta kupima; nilimwajiri kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kupima na kutunza kumbukumbu. Akifikisha mzigo unaozidi kilo 100 nilisafiri toka Dar kurudi home ili nisafirishe mzigo kupeleka Kenya. Huko nilirudi na bidhaa za urembo ambazo niliendelea kuwauzia wamachinga.

Baada ya kumaliza chuo; sikuwa na wazo la kuajiriwa kwa kuwa tayari nilishakuwa mzoefu wa kutosa hela kwenye biashara na kupata faida. Kwa kuwa nilikuwa huru, nilifanikiwa kupata watu wenye mali ambazo zina spidi ndogo (hazitoki sana) hivyo walinipatia ili niwe na mlango wa biashara hapa Tanzania. NIliendelea na shughuli hizo na baadaye niliona kuwa shughuli za matumizi ya computer zinalipa; hivyo nilijiandikisha kufanya mitihani kwa kuwa ujuzi wa kutumia computer nilikuwa nao tayari (Nilisoma computer DarTech kama somo la ziada ambalo tulikuwa hatufanyi mtihani - miaka ya 90 hiyo).

Hadi sasa ninapoandika hivi; huwa nafanya kazi za muda; nalipwa kilicho changu naendelea na shughuli zangu. Ajira inafunga ufahamu; sio kwamba nawadanganya - hii ndiyo kweli yangu. Kwa sasa ni muelimishaji wa vikundi vya wajasiriamali; nafuga, nafanya kazi na NGO ambayo mimi ni mwanzilishi - MAISHA YANAENDA.

Ukipata ajira fanya ila usikae tu nyumbani eti unasubiri ajira wakati benk una pesa kama laki 500,000/= inaendelea kupungua kila iitwayo leo.
Kaka Tutor B nakuelewa unachojaribu kuzungumza lakini kwa historia yako tu napata kujua yakuwa wewe ulikuwa unapata support home tangia upo mdogo na ndiyo maana hata ulipofika chuo uliweza kuendelea na biashara....

Zaidi nafikiri pengine hata mtaji ulipokuwa unakata ulikuwa unapewa support toka nyumbani...

Nizungumzie mimi binafsi, nimekuwa katika mazingira ambayo sina hata uwezo wa kumuomba ndugu hata elfu 10,000/= yakununua huyo kuku wa kienyeji, kwa hiyo famili tunazotoka pia ni shida....

Back
Top Bottom