Kazi zipo ila ajira hakuna

Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,734
Likes
4,589
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,734 4,589 280
Habari za leo waungwana!
Leo nakushirikisha katika hili .... hapa Tanzania tuna wasomi wetu wengi ambao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view. Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution. Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.
Fikiria: Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze.
Halafu treni za umeme ziko
Halafu self driving cars
Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)
Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini?
Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.
Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira.
Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI". Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding... Ukimpa idea nyingine HATAKI.
Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in bness.
Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.
Ukitazama #DiamondPlutnumz na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye. Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira?
Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!
So sad!
Sikiliza kijana msomi:
Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa.
Mungu awabariki sana.

Jifunze Kuthubutu tusiwe na kikomo cha kufikiri.
Fikiri hata mara 1000 usiochoke unapoanguka ndo inakuongezea uwezo wa kutatua Changamoto zinazokukakabili.
KUMBUKA AJIRA HAZIPO LAKINI KAZI ZIPO

UNAWEZA WAKATI NI SASA.
 
SMART PASSENGER

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Messages
556
Likes
371
Points
80
SMART PASSENGER

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2018
556 371 80
Umewaza mbali hakika lakini nikuulize swali dogo sana ivi unawezaje kujiajiri bila mtaji au ndo ile twende saccos tukakope tulime matikiti.

Swali la pili wewe umejiajiri basi tupatie walau mbinu mkuu sababu naamini mali inapatikana darasani

Assume nimemaliza bachelor ya ualimu wa sanaa.
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,734
Likes
4,589
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,734 4,589 280
Umewaza mbali hakika lakini nikuulize swali dogo sana ivi unawezaje kujiajiri bila mtaji au ndo ile twende saccos tukakope tulime matikiti.

Swali la pili wewe umejiajiri basi tupatie walau mbinu mkuu sababu naamini mali inapatikana darasani

Assume nimemaliza bachelor ya ualimu wa sanaa.
1. Unajiajiri kwanza ili upate mtaji ....

2. Mtaji namba moja ni hiyo elimu uliyo nayo; elimu hiyo unaibadili inakuwa maarifa ... maarifa hayo unayatoa kwa wengine .. hapa kuna tatizo kidogo jinsi ya kuyatoa.
Wengi wanahitaji ku-deliver walicho nacho kichwani kwa njia iliyozoeleka .. kufundisha madarasani. Ukiandika vitabu je?
 
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
4,785
Likes
8,626
Points
280
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
4,785 8,626 280
huu ujinga wa kujiajiri huwa siungi mkono, unakuta mtu ni mkurugenzi asha chota pesa za kutosha ila anapigana mwanae aajiliwe na sio kumpa mtaji ajiajili

kuna watu wako ofisini 20+yrs kama ni mitaji wameshapata ila kujiajiri hawataki wao wamekazana kutuhamasisha sisi ndo tujiajili

wabunge na mafao ya 200mill. badala wajiajili ila wanazitumia kuhonga ili warudi kuajiliwa na wananchi.

huwezi kujiajili mazingira ni mabovu, mtaji huna, taasisi za fedha hazitoi mkwanja

labda tujiajili ku-beti
 
L

lordchimkwese

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2015
Messages
286
Likes
304
Points
80
L

lordchimkwese

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2015
286 304 80
Kujiajiri sio rahisi kama hauna pesa tusidanganyane....
Ukiwa kitaa huku mtaji unatafuta kwa mbinde kwa kuunga unga kiasi kwamba hasara haitakiwi..
Ukipata hasara umeumia mana unakuta wafadhili wako wote ndio walikuchangia first time..
Usione watu wanajazana DUCE pale
 
thesym

thesym

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Messages
3,081
Likes
2,906
Points
280
thesym

thesym

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2012
3,081 2,906 280
Umewaza mbali hakika lakini nikuulize swali dogo sana ivi unawezaje kujiajiri bila mtaji au ndo ile twende saccos tukakope tulime matikiti.

Swali la pili wewe umejiajiri basi tupatie walau mbinu mkuu sababu naamini mali inapatikana darasani

Assume nimemaliza bachelor ya ualimu wa sanaa.
Swala sio si kumaliza bachelor ya ualimu wa sanaa issue unachakata vipi kichwa kuweza kutumia ulichokisoma kikuingizie pesa.

Ambacho huwezi amini kuna mtandao maarufu unafahamika kwa jina udemy, upo kwa ajili ya kuuza kozi, kuna walimu na watu wengine wanatengeneza pesa kwa kufundisha na kuuza kozi za kiswahili kwenye huo mtandao wa udemy.

Kwa bahati mbaya watu wanaouza kozi za kiswahili wengi ni Wakenya na sikuona mtanzania hata mmoja, kwa nini?

Mfano mzuri tuchukulie huyu jamaa kutoka mombasa kenya.

kiswahili-udemy-png.943971

Ukicheki mshikaji ameweza ku-enroll wanafunzi 290 wanaojifunza na kununua kozi yake ya kiswahili, unajua kila mwanafunzi alilipia kiasi gani?, angalia ww mwenyewe hapa.

kiswahili-course-price-png.943974

Ukiangalia kabla alikuwa anatoza $29.99 kwa kichwa na baadae kupunguza na kuwa ni $9.9 kwa kuwa kozi ni ya zamani, now piga mahesabu mwenyewe jamaa ametengeneza kiasi gani.

Sasa nikijiuliza swali inakuwaje mwalimu wa kiswahili wa Tanzania ambapo ndio lugha imebobea anshindwa kurekodi kozi zake vizuri na kuuza kwenye teaching platforms mbalimbali, ila kulia ajira huku tukijiuliza eti mwalimu wa sanaa atajiajiri vp?

Kwa kenya sioni ikitumia kiswahili kulinganisha na TZ inakuwaje ww muhitimu BAED kiswahili una kompyuta na internet hujui namna kuuza ujuzi wako.

swahili-course-2-png.943973

Ukiangalia hilo jina la anayefundisha kiswahili ni mchina na hii ni kozi nyingine na bei ambayo ameiweka ni kama inavyoonekana kulia.

Hii image inaonyesha mkenya mwingine mwenye wanafunzi zaidi ya 100 akiuwauzia kozi ya kiswahili yenye urefu wa masaa mawili.

mwalimu-wa-kenya-udemy-png.943972

Kiufupi kila ulicho nacho na unachokijua kuna ambao hawakijui na wanahitaji kukijua hata kwa kulipia, uzuri ni kwamba wazungu ni watu wanaopenda kujifunza, kama ww ni mwalimu wa kiswahili fanya tafiti na uanze kufundisha mtandaoni hasa udemy achana na youtube.

Au tumia youtube kupromote kozi unayouza.
 
jwhizzy

jwhizzy

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
519
Likes
158
Points
60
Age
27
jwhizzy

jwhizzy

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
519 158 60
Swala sio si kumaliza bachelor ya ualimu wa sanaa issue unachakata vipi kichwa kuweza kutumia ulichokisoma kikuingizie pesa.

Ambacho huwezi amini kuna mtandao maarufu unafahamika kwa jina udemy, upo kwa ajili ya kuuza kozi, kuna walimu na watu wengine wanatengeneza pesa kwa kufundisha na kuuza kozi za kiswahili kwenye huo mtandao wa udemy.

Kwa bahati mbaya watu wanaouza kozi za kiswahili wengi ni Wakenya na sikuona mtanzania hata mmoja, kwa nini?

Mfano mzuri tuchukulie huyu jamaa kutoka mombasa kenya.

View attachment 943971
Ukicheki mshikaji ameweza ku-enroll wanafunzi 290 wanaojifunza na kununua kozi yake ya kiswahili, unajua kila mwanafunzi alilipia kiasi gani?, angalia ww mwenyewe hapa.

View attachment 943974
Ukiangalia kabla alikuwa anatoza $29.99 kwa kichwa na baadae kupunguza na kuwa ni $9.9 kwa kuwa kozi ni ya zamani, now piga mahesabu mwenyewe jamaa ametengeneza kiasi gani.

Sasa nikijiuliza swali inakuwaje mwalimu wa kiswahili wa Tanzania ambapo ndio lugha imebobea anshindwa kurekodi kozi zake vizuri na kuuza kwenye teaching platforms mbalimbali, ila kulia ajira huku tukijiuliza eti mwalimu wa sanaa atajiajiri vp?

Kwa kenya sioni ikitumia kiswahili kulinganisha na TZ inakuwaje ww muhitimu BAED kiswahili una kompyuta na internet hujui namna kuuza ujuzi wako.

View attachment 943973
Ukiangalia hilo jina la anayefundisha kiswahili ni mchina na hii ni kozi nyingine na bei ambayo ameiweka ni kama inavyoonekana kulia.

Hii image inaonyesha mkenya mwingine mwenye wanafunzi zaidi ya 100 akiuwauzia kozi ya kiswahili yenye urefu wa masaa mawili.

View attachment 943972

Kiufupi kila ulicho nacho na unachokijua kuna ambao hawakijui na wanahitaji kukijua hata kwa kulipia, uzuri ni kwamba wazungu ni watu wanaopenda kujifunza, kama ww ni mwalimu wa kiswahili fanya tafiti na uanze kufundisha mtandaoni hasa udemy achana na youtube.

Au tumia youtube kupromote kozi unayouza.
Mkuu umesema kweli, hii fursa inaniweka mjini Sasa. Ila wa Kenya wapo mbali sana. Pia Tanzania naona internet Ni changamoto hasa Kama unatumia Skype.
 
thesym

thesym

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Messages
3,081
Likes
2,906
Points
280
thesym

thesym

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2012
3,081 2,906 280
Mkuu umesema kweli, hii fursa inaniweka mjini Sasa. Ila wa Kenya wapo mbali sana. Pia Tanzania naona internet Ni changamoto hasa Kama unatumia Skype.
Unaweza kukomaa hata na bando usiku, mambo yakiwa fresh unaunga broadband kabisa kama rahanet.
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,734
Likes
4,589
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,734 4,589 280
Naomba niwajibu wote kwa pamoja mnaofikiri kwamba mimi nimeajiriwa ...
Nikiwa mdogo (chini ya miaka 14) nilikuwa na uwezo wa kutengeneza vikapu - entukuru na kupeleka minadani. Haikutosha, nikawa nafuga kuku wa kienyeji, nauza mayai na kuku pia. Shughuli hiyo niliendelea nayo hadi nilipomaliza elimu ya msingi na kulazimika kwenda sekondari - bweni.

Wakati nikiwa sekondari, likizo zangu zote nilirudi kijijini kuendelea na mchakato huo huo. Hivyo kwenye kukua kwangu nilizoea mzingira ya kujitafutia pesa za kwangu binafsi kwa ajili ya matumizi yangu. Wazazi waliwajibika kulipa karo (japo ilikuwa kidogo) pamoja na matumizi mengine ya lazima pindi niwapo shuleni.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, nilijiunga moja kwa moja DarTech (kwa sasa inaitwa DIT); nikiwa hapo nilikuwa nachukua bidhaa toka mipakani Tunduma na Mtukura na kuwauzia wamachinga kwa bei ya jumla; wao wanaingiza mtaani na kupata faida. Baadaye nikapata mchongo wa kwamba chuma chakavu kina soko nchini Kenya - mnunuzi mzuri alikuwa anaitwa Mkole (sijui kama bado yupo). Niliporudi nyumani nilinunua mzani kwa ajili ya kupima chuma - hivyo vijana wa pale mtaani walikusanya masufuria mabovu, nyaya n.k na kuleta kupima; nilimwajiri kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kupima na kutunza kumbukumbu. Akifikisha mzigo unaozidi kilo 100 nilisafiri toka Dar kurudi home ili nisafirishe mzigo kupeleka Kenya. Huko nilirudi na bidhaa za urembo ambazo niliendelea kuwauzia wamachinga.

Baada ya kumaliza chuo; sikuwa na wazo la kuajiriwa kwa kuwa tayari nilishakuwa mzoefu wa kutosa hela kwenye biashara na kupata faida. Kwa kuwa nilikuwa huru, nilifanikiwa kupata watu wenye mali ambazo zina spidi ndogo (hazitoki sana) hivyo walinipatia ili niwe na mlango wa biashara hapa Tanzania. NIliendelea na shughuli hizo na baadaye niliona kuwa shughuli za matumizi ya computer zinalipa; hivyo nilijiandikisha kufanya mitihani kwa kuwa ujuzi wa kutumia computer nilikuwa nao tayari (Nilisoma computer DarTech kama somo la ziada ambalo tulikuwa hatufanyi mtihani - miaka ya 90 hiyo).

Hadi sasa ninapoandika hivi; huwa nafanya kazi za muda; nalipwa kilicho changu naendelea na shughuli zangu. Ajira inafunga ufahamu; sio kwamba nawadanganya - hii ndiyo kweli yangu. Kwa sasa ni muelimishaji wa vikundi vya wajasiriamali; nafuga, nafanya kazi na NGO ambayo mimi ni mwanzilishi - MAISHA YANAENDA.

Ukipata ajira fanya ila usikae tu nyumbani eti unasubiri ajira wakati benk una pesa kama laki 500,000/= inaendelea kupungua kila iitwayo leo.
 
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
23,249
Likes
11,647
Points
280
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
23,249 11,647 280
Habari za leo waungwana!
Leo nakushirikisha katika hili .... hapa Tanzania tuna wasomi wetu wengi ambao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view. Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution. Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.
Fikiria: Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze.
Halafu treni za umeme ziko
Halafu self driving cars
Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)
Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini?
Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.
Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira.
Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI". Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding... Ukimpa idea nyingine HATAKI.
Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in bness.
Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.
Ukitazama #DiamondPlutnumz na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye. Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira?
Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!
So sad!
Sikiliza kijana msomi:
Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa.
Mungu awabariki sana.

Jifunze Kuthubutu tusiwe na kikomo cha kufikiri.
Fikiri hata mara 1000 usiochoke unapoanguka ndo inakuongezea uwezo wa kutatua Changamoto zinazokukakabili.
KUMBUKA AJIRA HAZIPO LAKINI KAZI ZIPO

UNAWEZA WAKATI NI SASA.
1543031715791-jpeg.944122
 
Mbokigwe Mwambungu

Mbokigwe Mwambungu

Member
Joined
Feb 28, 2018
Messages
29
Likes
22
Points
5
Mbokigwe Mwambungu

Mbokigwe Mwambungu

Member
Joined Feb 28, 2018
29 22 5
Education is a key of life but Skills is a master key of life. big up Tutor b!!
 
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
1,291
Likes
1,032
Points
280
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
1,291 1,032 280
Umeongea points sana Tutor B. Ni kweli kabisa suala la ajira, ndilo linalozidi kutafuna bongo za watanzania wengi sana.

Na numejaribu kupitia comments zote hapo juu. Nimeona taklibani 85% ya watu, wameshindwa kukuelewa haswa. Sababu sio kwamba ulichokiandika hakieleweki, bali sababu ni kwamba WAMEKOSA ELIMU YA NJE YA BOX LA AJIRA(nontraditional education), hivyo sio rahisi kukuelewa kirahisi rahisi, hasa pale unapoongelea suala la KUJIAJIRI. Ama hakika jitiada za makusudi kabisa zinahitajika, ili kuzikomboa jamii....

Asante sana mheshimiwa Tutor B
 
Si lazima ufanye kazi ya kile ulichokisomea. Mimi nimesoma Mechanical Engineering - ni fundi mchundu (FTC); lakini hata siku moja sikuwahi kufanya kazi hiyo (workshop) ila nikikutana na mafundi nafanya nao kazi za kuandika kwa sababu tunaongea lugha moja. Hivyo FTC yangu sio kwamba hainisaidii - inanisaidia pale ninapokutana na mafundi wakataka kunishirikisha kwenye maandalizi ya kazi zao kama michoro n.k.

Kuna rafiki yangu mwingine kwa sasa ni mzee sana - aligraduate mwaka 1982; naye hakuwahi kuajiriwa na kwa sasa ana SACCOS; ni baada ya kuona ajira zinazengua ndo akarudi MUCOBS kusoma mambo ya SACCOS management; nasisitiza hajawahi kuajiriwa .. analima, anafuga, alishaanzisha centre za VETA kibao sehemu tofauti na zinaendelea kumlipa kwenye uzee wake; na zitaendelea kumilikiwa na watoto wake.

Kwenye ajira huna cha kummilikisha mtoto wako!
 
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Messages
1,286
Likes
1,321
Points
280
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2010
1,286 1,321 280
Naomba niwajibu wote kwa pamoja mnaofikiri kwamba mimi nimeajiriwa ...
Nikiwa mdogo (chini ya miaka 14) nilikuwa na uwezo wa kutengeneza vikapu - entukuru na kupeleka minadani. Haikutosha, nikawa nafuga kuku wa kienyeji, nauza mayai na kuku pia. Shughuli hiyo niliendelea nayo hadi nilipomaliza elimu ya msingi na kulazimika kwenda sekondari - bweni.

Wakati nikiwa sekondari, likizo zangu zote nilirudi kijijini kuendelea na mchakato huo huo. Hivyo kwenye kukua kwangu nilizoea mzingira ya kujitafutia pesa za kwangu binafsi kwa ajili ya matumizi yangu. Wazazi waliwajibika kulipa karo (japo ilikuwa kidogo) pamoja na matumizi mengine ya lazima pindi niwapo shuleni.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, nilijiunga moja kwa moja DarTech (kwa sasa inaitwa DIT); nikiwa hapo nilikuwa nachukua bidhaa toka mipakani Tunduma na Mtukura na kuwauzia wamachinga kwa bei ya jumla; wao wanaingiza mtaani na kupata faida. Baadaye nikapata mchongo wa kwamba chuma chakavu kina soko nchini Kenya - mnunuzi mzuri alikuwa anaitwa Mkole (sijui kama bado yupo). Niliporudi nyumani nilinunua mzani kwa ajili ya kupima chuma - hivyo vijana wa pale mtaani walikusanya masufuria mabovu, nyaya n.k na kuleta kupima; nilimwajiri kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kupima na kutunza kumbukumbu. Akifikisha mzigo unaozidi kilo 100 nilisafiri toka Dar kurudi home ili nisafirishe mzigo kupeleka Kenya. Huko nilirudi na bidhaa za urembo ambazo niliendelea kuwauzia wamachinga.

Baada ya kumaliza chuo; sikuwa na wazo la kuajiriwa kwa kuwa tayari nilishakuwa mzoefu wa kutosa hela kwenye biashara na kupata faida. Kwa kuwa nilikuwa huru, nilifanikiwa kupata watu wenye mali ambazo zina spidi ndogo (hazitoki sana) hivyo walinipatia ili niwe na mlango wa biashara hapa Tanzania. NIliendelea na shughuli hizo na baadaye niliona kuwa shughuli za matumizi ya computer zinalipa; hivyo nilijiandikisha kufanya mitihani kwa kuwa ujuzi wa kutumia computer nilikuwa nao tayari (Nilisoma computer DarTech kama somo la ziada ambalo tulikuwa hatufanyi mtihani - miaka ya 90 hiyo).

Hadi sasa ninapoandika hivi; huwa nafanya kazi za muda; nalipwa kilicho changu naendelea na shughuli zangu. Ajira inafunga ufahamu; sio kwamba nawadanganya - hii ndiyo kweli yangu. Kwa sasa ni muelimishaji wa vikundi vya wajasiriamali; nafuga, nafanya kazi na NGO ambayo mimi ni mwanzilishi - MAISHA YANAENDA.

Ukipata ajira fanya ila usikae tu nyumbani eti unasubiri ajira wakati benk una pesa kama laki 500,000/= inaendelea kupungua kila iitwayo leo.
Ukweli mchungu,Mimi nimekuelewa Mkulu
 
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
1,291
Likes
1,032
Points
280
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
1,291 1,032 280
Sure Mkuu...Kujiajiri ndio mpango mzima katika dhama hizi.
Si lazima ufanye kazi ya kile ulichokisomea. Mimi nimesoma Mechanical Engineering - ni fundi mchundu (FTC); lakini hata siku moja sikuwahi kufanya kazi hiyo (workshop) ila nikikutana na mafundi nafanya nao kazi za kuandika kwa sababu tunaongea lugha moja. Hivyo FTC yangu sio kwamba hainisaidii - inanisaidia pale ninapokutana na mafundi wakataka kunishirikisha kwenye maandalizi ya kazi zao kama michoro n.k.

Kuna rafiki yangu mwingine kwa sasa ni mzee sana - aligraduate mwaka 1982; naye hakuwahi kuajiriwa na kwa sasa ana SACCOS; ni baada ya kuona ajira zinazengua ndo akarudi MUCOBS kusoma mambo ya SACCOS management; nasisitiza hajawahi kuajiriwa .. analima, anafuga, alishaanzisha centre za VETA kibao sehemu tofauti na zinaendelea kumlipa kwenye uzee wake; na zitaendelea kumilikiwa na watoto wake.

Kwenye ajira huna cha kummilikisha mtoto wako!
 
Forum statistics

Threads 1,262,368
Members 485,562
Posts 30,121,318