Ni kweli, kazi zipo kibao. Nchi hii ina changamoto chungu nzima, nchi hii bado changa haina maendeleo. Inahitajika kufanya kazi kubwa sana kutatua changamoto na kufanya nchi yetu iendelee kama nchi zingine zilizoendelea.
Sema, kikwazo kikubwa kwa sasa ni 'mentality' ya kikoloni kuwa maisha ya msomi ama maisha ya kipato ni kuwa na ajira ya kupata mshahara mwisho wa mwezi.
Siku hii mentality ikifa akilini na moyoni mwa mtu ndipo atakaposhangaa ni namna gani alivyo na uwezo mkubwa wa kujipatia kipato kikubwa nje ya ajira.
Kazi zipo nyingi sana, sema tu sio za lelema unapaswa kujituma si kawaida tofauti na watu waliopo kwenye ajira. Na hapa ndipo penye shida sana watu hawataki kujituma sana, wanataka kujituma kidogo tu kama wafanyavyo wenye ajira.
Mimi nasisitiza tujitume sana maisha yatakuwa mazuri mara kumi zaidi ya walio kwenye ajira. Hii nchi ina kazi nyingi mno ila ajira ni chache sana kama sio hakuna kabisa.
Hata hivyo ieleweke tu wazi kuwa kadri muda unavyosonga mbele ndivyo hali inavyozidi kuwa complicated wala tusitarajie eti mambo yatakuwa ahueni kidogo.
Hali ya maisha ya sasa ina provide kile kitu kinaitwa 'SURVIVAL FOR THE FITTEST'. Hata waliopo kwenye ajira wanalalamika kipato kidogo, hawana future nzuri na walio nje ya ajira wanalalamika maisha magumu. Hii contradiction ndio haswa inatengeneza mazingira 'survival for the fittest, and the weak will perish'. Let's be fit.
Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, kwa nyakati hizi the strongest and luckiest people are going to shine above the weak people, yaani hizi ndio nyakati bora kabisa za watu strong and lucky. Prove yourself how strong and lucky you are, or else how weak you are!
Kwa hisani ya
Tutor B