Kazi ya Wassira ni ipi?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,208
1,749
tunaambiwa wassira ni waziri wa mahusiano ya umma. Labda tupate ufafanuzi wa mahusiano ya umma. Lakini tunaambiwa kuwa yeye ndiye aliyesababisha lile sakata la vijana watatu wa cdm kukamatwa na kuwekwa ndani. Kosa lao ni kuhudhuria mkutano wa ccm? Mabona ni yeye wassira aliwachokoza?
Sakata hilo likapelekea hadi vijana wa ccm kwenda kuomba msamaha kwa katibu wa cdm. Nako kukazuka tafrani nyingine. Yule bangebange nae akajipeleka na vijana wa cdm wakamkwida, na kwa busara ya katibu mkuu ndo ikawa pona yake. Kudhihirisha ukuda wake, badaala ya kushukuru kuwa yameisha anapeleka tena lawama kwa vijana wa cdm kuwa wameonyesha utovu wa nidhamu.
Kama sio kauli za kukurupuka za wassira tungefika huko hadi kwenda kuombana misamaha? Kwanza aliyetakiwa kwenda kuomba msamaha ni yeye wassira, ila kwa kuwa anaeleweka kuwa nae ni bange, vijana waliomzidi busara wakaenda kumuombea radhi.
kauli za wassira ni hizi; aliwataka vijana wa cdm waliokuwa kwenye mkutano wake wanyooshe mikono. Then...? Baada ya kuona hakuna eti akashukuru kuwa hawapo. Kwani nchi ya ccm hii? Ndipo ziliposikika kelele na miruzi toka kila kona ya uwanja huo, huku umati uliokuwepo hapo ukinyoosha vidole viwili na kusema ile kauli maarufu ya cdm-piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiipoooooooooooooooooooooooz..............!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kazi ya wassira ni ipi?
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,529
55,390
Muulize muhifadhi mkuu Gombe National park atakueleza kwa ufasaha maana kule ndipo ulipo ukoo wake.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164

Kazi ya Wasira ni mahusiano ya umma yaani kuunganisha ikulu na umma, nadhani nimekujibu. Haya funga thread mara moja.
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,208
1,749
Kazi ya Wasira ni mahusiano ya umma yaani kuunganisha ikulu na umma, nadhani nimekujibu. Haya funga thread mara moja.

pamoja na majibu ya mashaka ya ndugu mwita, ningependa kuuliza swali la nyongea. Je, umma ni nini na ikulu ni kitu gani. Na je, umma na ikulu vinaingilianaje?
 
Ikulu ni taasisi inayojumuisha kazi na majukumu ya Rais wakati umma ni mkusanyiko wa raia kwa umoja wao. Haya funga thread mara moja.
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,208
1,749
Ikulu ni taasisi inayojumuisha kazi na majukumu ya Rais wakati umma ni mkusanyiko wa raia kwa umoja wao. Haya funga thread mara moja.

report post if u can. Sasa mbona huyu jamaa anachafua hali ya hewa kati ya umma na ikulu?
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,891
1,190
Mimi kazi kubwa ya Wassira ninayoifahamu ni "kusinzia ovyo". Huyu jamaa wakati mwingine huwa anasinzia hata akiwa anakula na familia yake!
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
Ikulu ni taasisi inayojumuisha kazi na majukumu ya Rais wakati umma ni mkusanyiko wa raia kwa umoja wao. Haya funga thread mara moja.
Ndugu haya majibu yako unarefer wapi??katiba, Sheria na kanuni, circular za serikali au unajibu kama unavyofahamu wewe???Napata mashaka sana na majibu yako, halafu nakuelewa kwa shida mno ndugu yangu.
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,392
14,010
Kazi ya Wasira ni mahusiano ya umma yaani kuunganisha ikulu na umma, nadhani nimekujibu. Haya funga thread mara moja.
Ilihitaji wizara hii? Na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu (Salva et all) ina kazi ipi?
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Pakitakiwa hoja ya nguvu lazima utamkuta Wassira. Yeye hana habari na nguvu ya hoja. Jana alikiri rasmi kuwa yeye ni Tyson. JK alitaka kumpa Ukatibu Mkuu wa CCM akazuiwa na wazee.
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
report post if u can. Sasa mbona huyu jamaa anachafua hali ya hewa kati ya umma na ikulu?
Huyu bwana anapenda kujipambanua kama msemaji wa serikali humu ndani, kimsingi kazi yake kubwa humu ni uchafuzi wa hali ya hewa. We twende tu utaona, hapo anatafuta platform ya kutujazia siku.
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,208
1,749
Amechafuaje hewa

kazi uliyotumwa humu jukwaani hakika imeshakushinda. Soma uzi unasemaje kisha nyumbulisha. Kiufupi wassira alipata hiyo post kwa bahati mbaya sana. Ilibidi arudishwa Tarime kukabiliana na wezi wa mifugo toka nchi jirani. Lakini kazi sophisticated kama mahusiano ya umma hazitaki kusinzia, jazba wala papara. Anachafua hali ya hewa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom