Kazi ya Vice Prezdaa ni nini?

Mlitika

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
457
260
Ikiwa kama jambo lolote hata linalohusu utendaji wa wizara moja basi lazima rais ndo atoe jibu; ivi job description ya makamu wa rais inasemaje? Kimsing mbona kama hahitajiki?
 
Makamu wa rais majukumu yake ni kama ya waziri wa mazingira.

Nadhiriki kusema tuna mawaziri wa mazingira wawili
 
Ikiwa kama jambo lolote hata linalohusu utendaji wa wizara moja basi lazima rais ndo atoe jibu; ivi job description ya makamu wa rais inasemaje? Kimsing mbona kama hahitajiki?

47
.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya
Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku
hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
au yuko nje ya nchi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa
Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa
pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake
wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na
watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais
akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.
(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa
kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano
atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais
atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
40
(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi;
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.
(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote
kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu
kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa
Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.
(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar
anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti
cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.
(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya
uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa
Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na
Rais.
Wakati wa
Makamu wa
Rais kushika
madaraka
Sheria ya 1994
Na.34 ibara 11
48
.-(1) Makamu wa Rais atashika madaraka ya Makamu wa
Rais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.
(2) Makamu wa Rais aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara ya
50(3) ataapa na kushika madaraka yake baada ya uteuzi wake
kuthibitishwa na Bunge.
Kiapo cha
Makamu wa
Rais.
Sheria
Na.34 ya 1994
ib.11
49
. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake
ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo
cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na
utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
 
Mzee wa mikasi sio mzugaji, akiona tu ribon anatoa mkasi kutoka kwenye mfuko wa kushoto wa koti lake
Ikiwa kama jambo lolote hata linalohusu utendaji wa wizara moja basi lazima rais ndo atoe jibu; ivi job description ya makamu wa rais inasemaje? Kimsing mbona kama hahitajiki?
 
Wakuu niambieni huyu jamaa yeye mbona haeleweki? Au kazi za makamu wa raisi ni zipi? Nijuzeni wakuu.
 
kutembea na mkasi mfukoni tayari kwa kuzindua...pia na kitambaa cha kupiga goti wakati wa kupanda miti..hizi nafasi nyingine ni kupoteza fedha za watanzania
 
kutembea na mkasi mfukoni tayari kwa kuzindua...pia na kitambaa cha kupiga goti wakati wa kupanda miti..hizi nafasi nyingine ni kupoteza fedha za watanzania

Ha ha haaa! Kazi kweli kweli.
 
Ikiwa kama jambo lolote hata linalohusu utendaji wa wizara moja basi lazima rais ndo atoe jibu; ivi job description ya makamu wa rais inasemaje? Kimsing mbona kama hahitajiki?

jamani kaacheni kapumzike maana ni kazee sana ila kali badili miaka kipindi kana kwenda marekani kusudi kasikose scholarship cozo kamezaliwa 1936 na kanasema eti 1942.Maana mie babu yangu anamiaka 80..mawazo yake ni primitive afu siunakumbuka enzi hizo wazungu ndio walikuwa wanakata utepe sasa analipizia kabla hajafa.
 
tatizo liko kwa Rais mwenyewe kung'ang'ania majukumu yote yeye na wkt mengine anakuwa mzto kutoa maamuz. Me namkubali sana vice ni BRIGHT kuliko mkubwa
 
Back
Top Bottom