Kazi ya kutafsiri kitabu, msaada jamani

Kazi ya kutafsiri kitabu, msaada jamani

Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
3,422
Reaction score
5,595
Niko kwenye maandalizi ya project ya kwenda kufundisha wakulima mkoani Lindi juu ya kuongeza thamani ya mazao yao.

Nimeanza kuandaa teaching guide toka kwenye kitabu kimoja cha kiingereza cha Entrepreneurship ila ningependelea kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.

Nahitaji mnisaidie kunipa tafsiri ya baadhi ya maneno kwa lugha ya kiswahili wandugu, Tuanze na haya yafuatayo:

1.Market and Margin Related issues
2.Competitive advantage
3.Gross margin
4.Barriers to entry
5.Proprietary advantage
6.Lead time advantage
7.Service chain
8.Timing
9.Overall Potential
10.Fixed and variable costs
 
Ningeweza kufasiri kama yanavyoonekana, lakini nadhani ni msamiati wa kitaalamu ambao una maneno yake tayari. Mtafute mwalimu ambaye ni mzoefu, cc; KOKUTONA..
 
Last edited by a moderator:
Deeboyfrexh

Mimi sio mtaalamu wa lugha na pengine watu watakuja hapa na kunisahihisha lakini ifuatayo ni jitihada yangu kukupa tafsiri ya hizo terminologies unazotaka kuzitumia.

Tupilia mbali chochote kile kisichokufaa - I won't be offended.



1.Market and Margin Related issues ......................Masuala yanayohusu masoko na tijara

2.Competitive advantage ......................................Unafuu (ubora) wako katika ushindani

3.Gross margin ...................................................Tijara jumla

4.Barriers to entry ...............................................Vikwazo vya kujiunga

5.Proprietary advantage .......................................Unafuu (au uzuri) wa umiliki

6.Lead time advantage .........................................Uzuri (ubora) wa kudamka

7.Service chain ....................................................Mfumo (mtiririko) wa huduma

8.Timing .............................................................Uwahishaji muafaka

9.Overall Potential ...............................................Jumla ya uwezo

10.Fixed and variable costs ...................................Gharama za awali na badilishi
 
2. faida za ushindani
4. vikwazo/ changamoto za kuingia/kuanza
5. faida za mmiliki
7. mtiririko wa huduma
8. Mipango madhubuti
9. faida kwa ujumla
 
fixed cost =gharama zisizobadilika uzalishaji/huduma ukipanda au kushuka
varialecost= kinyume cha hapo juu
 
Niko kwenye maandalizi ya project ya kwenda kufundisha wakulima mkoani Lindi juu ya kuongeza thamani ya mazao yao.Nimeanza kuandaa teaching guide toka kwenye kitabu kimoja cha kiingereza cha Entrepreneurship ila ningependelea kuitafsiri kwa lugha ya kiswahili...
Nahitaji mnisaidie kunipa tafsiri ya baadhi ya maneno kwa lugha ya kiswahili wandugu,
Tuanze na haya yafuatayo:
1.Market and Margin Related issues
2.Competitive advantage
3.Gross margin
4.Barriers to entry
5.Proprietary advantage
6.Lead time advantage
7.Service chain
8.Timing
9.Overall Potential
10.Fixed and variable costs

Kuna malipo? Au ndo michosho?
 
Ningeweza kufasiri kama yanavyoonekana, lakini nadhani ni msamiati wa kitaalamu ambao una maneno yake tayari. Mtafute mwalimu ambaye ni mzoefu, cc; KOKUTONA..

Nadhani atakuwa ameshapata wa kumtafiria.
Sisi walimu wa Fizikia hatunaga vingereza vingi atiii
 
Back
Top Bottom