Kazi ya kuandikisha BVR Ilala

Kazi ya kuandikisha BVR Ilala

shemweta91

Senior Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
101
Reaction score
18
Habari wana JF.

Mimi ni mmoja wa waliopeleka maomba ya nafasi ya kazi ya BVR operator kwa upande wa Ilala ila mpaka sasa sijajua kinachoendelea mana wenzetu wa wilaya tofauti washapata na tumeona walipofikia mpaka sasa ila kwa ilala ni kimya. Hivyo mwenye taarifa kamili ninamuomba atupatie hapa nasi tujue kama tushakosa ama ni vipi.

Nawasilisha!
 
Duha kimya nimetoka kata kuangalia kimya

Mimi nilienda pale ilala kwa yule mama akaniambia hana taarifa na anahisi majina watatoa kulekule manispaa tulikopeleka barua sasa sikujua nini cha kufanya mana nilitoroka sehem za watu
 
Majina yanaweza kubandikwa leo pale manispaa! Keep on waiting
 
Majina yanaweza kubandikwa leo pale manispaa! Keep on waiting

Nilipita pale jana asubuhi 24/06/2015 wakanambia kua ijumaa huenda majina yakatoka na kuna uwezekano jumatatu ndo tukafanya usaili hii ni kutoka masijala japo alisema nae hana uhakika
 
Wadau mrejesho ni huu! Masjala wamedai kuwa majina yatawekwa leo jioni au kesho kwa walioomba ilala
 
Wadau mrejesho ni huu! Masjala wamedai kuwa majina yatawekwa leo jioni au kesho kwa walioomba ilala

yatawekwa wapi kuna mtu anansumbua hapa. Yatawekwa ofisi ya mkulugnz au ofisi za kata au wapi?
 
Back
Top Bottom