Kazi nzuri ITV, Said Mwema

Kipindi cha ITV kuhusu ripoti barabaran kilichorushwa kwa ustadi mkubwa kimeweka mambo wazi na SAIDI Mwema amakubali kwamba matrafiki wanakula rushwa kwa kwenda mbele utafikiri kiama imefika. Serikali sasa inaweza kuchukua mbinu hiyo kuwanasa maaskari wengine wala rushwa. Maaskari walionyeshwa wakipokea rushwa wanaweza kufukuzwa kazi, je wale waliotoa rushwa watachukuliwa hatua gani? Na Je Jerry Muro aliyerekodi maovu hayo kwa ugunduzi huo na kazi nzuri atapewa zawadi gani?
Nadhani target isiwe polisi tuu, tunaweza kufanya mengine zaidi, watuhakikishie kuwa wanahitaji msaada huo. Yani hata baadhi ya madude ya wakubwa wanaokamua rushwa kubwa zaidi kuna proof za videos ambazo watu wanashindwa nani wamwamini na kumkabidhi, na ukimkabidhi usalama wako utakuwaje!

Nice move from Jerry, ni mwanzo mzuri, asiishie huko tu!
 
Tunahitaji wanahabari wa aina ya Jerry Muro.Nilianza kumzimia huyu jamaa siku alipomkalia kooni DC wa Ilala Patric Tsere live on tv siku lilipoguka ghorofa mtaa wa Kisutu.Tsere alidai kuwa itaundwa tume ya uchunguzi kuhusu ajali hiyo,na Muro akamuuliza tume hadi lini wakati ile ya Lowassa kuhusu ghorofa la Chang'ombe imekaliwa kabatini?

Wakati tunampongeza Muro na kumtaka aendelee na uzi huohuo ni muhimu pia kukumbuka kwamba mara kadhaa wafichua maovu nchini kwetu wanaishia kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa watuhumiwa pasipo vyombo vya dola kuchukua hatua madhubuti za kukomesha kamtindo hako.Angalia ishu ya Kubenea...japo kesi iko mahakamani kwa mwendo wa kusuasua,mwandishi huyo na gazeti lake limejikuta mara kadhaa likipekuliwa na polisi kwa madai ya kipumbavu kabisa.

Ushauri wangu kwa Muro ni kwamba ushujaa wake uendelee sambamba na umakini katika usalama wake.Pongezi za akina Mwema ni geresha tu kwa vile inafahamika sana kwamba rushwa zinazopokelewa na trafiki hupelekwa pia kwa vigogo wa jeshi la polisi,just like vigofu vinavyotakiwa kupeleka pasenteji flani kwa wakubwa kila baada ya shifti.

Muhimu: Ushauri wa umakini katika usalama haumaanishi kum-discourage Muro katika vuguvugu alilolianzisha
 
Hivi ni kweli wale askari wameshughulikiwa au ni housekeeping (kujisafisha) kwa jeshi la polisi? Kama kweli walitaka jamii iwaamini wangetangaza majina ya wahalifu na adhabu walizopewa. Hivi haiwekzekani hawa jamaa wakahamishwa tu kuondolewa wanapojulikana na kupelekwa sehemu zingine au kuondolewa idara ya traffic na kupelekwa idara zingine ili kupoza mambo? Mwenye taarifa zaidi kuhusu hasa ni hatua zipi jeshi la polisi limechukua atueleze. Kuna tetesi kuwa askari wadogo huwa wanapangiwa na wakubwa kiasi cha kukabidhi kutokana na makusanyo yao ya hongo kila siku. Kama hiyo ni kweli, je, hao vumilia vumbi si watakuwa wanatolewa kafara huku mfumo ukiwa bado intact.
 
waga,

GT hajatumwa, na kama katumwa basi katumwa na wananchi. Kutofautiana mitizamo ni jambo zuri sana katika mijadala kama hii.

Nkamangi,

Hapa umeniua kabisa!
kaama kweli vile?
Sasa iakuwaje watu wanapokuwa tofauti na nyie wanafutiwa post zao? USILOGWE UKAISIFIA CCM
Sijui na hii iatafutwa kabla haijasomwa?
 
Me nadhani pongezi kwanza zingekwenda kwa mtararishaji wa kipindi na mpiga picha wao maana kazi kubwa imefanya na mpiga picha baada ya kuambiwa nini cha kufanya sio kwamba nina mbania Jerry but Jerry ni mtu wa 3 so hao wa 1 na 2 mbona wamesahaulika? Bila ya wao kurekodi hayo matukio Jerry angetangaza nini. Je huyo aliyetowa hilo wazo kuhusiana na kurekodi matukio yote hayo ya vijana wa Saidi Mwema na Mzee Kombe, watampatia zawadi gani?
Kina Jerry na wenzie watalindwa vp maana tayari kibarua cha hao vijana wa Mwema wamepoteza kibaru chao, sasa hao waliobaki si watakuwa na usongo nao.??
 
kaama kweli vile?
Sasa iakuwaje watu wanapokuwa tofauti na nyie wanafutiwa post zao? USILOGWE UKAISIFIA CCM
Sijui na hii iatafutwa kabla haijasomwa?
Mkuu kanda2 ukisema NYIE unawaunganisha wengi wasiokuwemo... Jaribu kuwa fair katika hukumu zako muzee!

BTW: Ukubwa jaa... CCM inatambua hilo ndo maana hata ikipigiwa kelele namna gani inazichuja kelele hizo na kuzifanyia kazi inazoona za muhimu...

Isikuume sana unapoitetea CCM hata pasipostahili ukabadilishiwa kibao, kwani unataka ushangiliwe tu mkulu? Hapana, penye wengi tarajia mengi... Kuna tutakaokuunga mkono na wengine tunakuponda huku tukikupa facts japo wengine kwa jazba tunaweza kukosa hata facts za upondaji wenyewe.

That's Jamii!
 
Back
Top Bottom