JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
TANGAZO LA KAZI
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anawatangazia Watanzania wenye sifa kutuma maombi ya kazi, ili kujaza nafasi za kazi zifuatazo:
MKAGUZI MSAIDIZI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (ASSISTANT INSPECTOR OF FIRE AND RESCUE) – nafasi 103
1.1 Sifa za mwombaji
Mwombaji awe na Shahada au Stashahada ya Juu katika moja ya fani zifuatazo: Uhandisi, Usanifu wa Majengo, Menejimenti ya Maafa (Disaster Management), Biashara (Bussiness Administration), Utawala, Rasilimaliwatu,
Mazingira, Ualimu,Udaktari na Sayansi ya Kompyuta kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.2 Kazi za kufanya
Kusimamia utoaji huduma ya kwanza kwa majeruhi katika matukio ya maafa;
Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga za moto kwenye maeneo mbalimbali kama vile viwanja vya ndege, miji , bandari na vijiji;
Kutoa elimu ya tahadhari ya moto kwa Umma;
Kusimamia na kuratibu shughuli za uzimaji moto na Uokoaji kwa kuchukua taarifa toka kwa wazimamoto (Firefighters) na kuziwasilisha kwa Kamanda wa tukio na kuchukua amri toka juu na kuwapelekea wa chini;
Kufanya uchunguzi wa matukio mbalimbali ya moto;
Kutoa mafunzo ya kinga ya moto, kuzima na kufanya ukaguzi wa tahadhari kwa askari waliopo kituoni;
Kukagua ubora na uimara wa zana na vifaa vya kuzimia moto vilivyo chini ya usimamizi wake;
viii.Kuandaa mpango wa ukaguzi na usalama wa ujenzi wa viwanda, vituo vya mafuta na mabomba ya gesi;
Kufanya ukaguzi wa ‘fire pumps' na ‘Fireman lifts' kwenye majengo marefu na viwandani;
Kusanifu mifumo ya kuashiria, kung'amua na kuzima moto (Fire Alarm, Fire Detection and Fire Suppression Systems);
Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri wa vifaa vya tahadhari vinavyotakiwa kufungwa kwenye majengo kabla na baada ya ujenzi na,
Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake.
SAJINI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (SERGEANT OF FIRE AND RESCUE) – Nafasi 190
2.1 Sifa za Mwombaji
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha sita.
Mwenye ujuzi katika fani zifuatazo atafikiriwa zaidi
na diploma ya kawaida ya Uuguzi; au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la I katika moja ya fani ya Umakenika, ufundi bomba, ufundi umeme, uchomeleaji, ufundi uashi na ufundi seremala.
2.2 Kazi za kufanya
Kusimamia kazi za chumba cha mawasiliano;
Kusimamia kazi za uzimaji moto na uokoaji;
Kuandaa utaratibu wa ukaguzi wa vituo vya maji vya Zimamoto (Fire Hydrants Inspection);
Kutunza kumbukumbu za kituo na
Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake wa kazi.
KONSTEBO WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (FIRE CONSTABLE) – nafasi 507
3.1 Sifa za Mwombaji
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha nne. Mwenye cheti/ujuzi katika fani zifuatazo atafikiriwa kwanza: Zimamoto, ufundi makenika, ufundi wa kuchomelea (welding) ufundi bomba, ufundi umeme, ufundi uashi, ufundi seremala, usomaji wa ramani za majengo, utunzaji wa kumbukumbu na udereva daraja C.
3.2 Kazi za kufanya
Kuzima moto;
Kuokoa Maisha na mali;
Kutoa huduma ya kwanza katika matukio ya maafa;
Kutunza na kukagua zana za zimamoto na uokoaji;
Kushiriki katika magwaride ya sherehe za jeshi au kitaifa;
Kulinda mali na zana za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji;
Kukagua vituo vya maji vya Zimamoto (Fire Hydrants);
viii.Kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto;
Kuelimisha na kushirikiana na Jamii juu ya dhana nzima ya Zimamoto ya kujitolea
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake.
MASHARTI MUHIMU YA KUZINGATIA
Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 30, mwenye afya njema na ambaye hajaoa au kuolewa.
Mwombaji awe hajatenda kosa lolote la jinai;
Mwombaji awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kwa muda usiopungua miezi 6 kabla ya kuajiriwa;
Mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote atakapopangiwa ndani ya Nchi;
Mwombaji aliyehudhuria na kufaulu mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji yanayotolewa na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, atafikiriwa kwanza;
Waombaji wenye sifa
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa;
Barua zote za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya masomo ya kidato cha nne na sita pamoja na vya taaluma/ujuzi, wasifu wa mwombaji (CV) ikiwa na majina ya wadhamini watatu na anwani zao, nakala ya cheti cha kuzaliwa na picha mbili ndogo za pasipoti;
viii.Mwombaji aandike kazi aliyoomba juu ya bahasha;
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 1 Februari, 2014
Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya Posta;
Waombaji wa kazi ya Sajini na Konstebo wa Zimamamoto na Uokoajiwatume barua za maombi kwa anuani ifuatayo:
Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
S.L.P 5821,
DAR ES SALAAM
Waombaji wa kazi ya Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto na Uokoajiwatume barua za maombi kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM