Kawambwa akanusha vya matundu 4 ya vyoo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kawambwa akanusha vya matundu 4 ya vyoo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaJambazi, Oct 29, 2010.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Leo asubuhi kupitia TBC1 Kawambwa amekanusha tuhuma za matundu 4 kwa 700m, badala yake yeye anasema yamejengwa kwa laki 7.

  Ila alikua anaonekana hayuko secure na alichokua anaongelea.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wakabadilishe kwenye ilani yao kwanza, kule ndiko ilikoandikwa!
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  What do you expect out of him. Amekuwa mbunge na hakuchukua hatua yeyote angalau hata ya kufuatilia tu. Kuna mdogo wangu alikuwa anafundisha kule Bagamoyo, Sekondari ya Miembe Saba - alilipigia kelele sana hili swala la vyoo vya shule na wizi wa hela, mwandishi wa habari alikwenda kumhoji akasema ukweli kuwa hakuna hata choo kimoja kilichojengwa hapo shuleni na manispaa - akawa amejipalia mkaa, akatumiwa majambazi kummaliza akasevu, wakataka kumshitaki wakakosa ushahidi - sasa hivi wamemkataa asifundishe wilayani Bagamoyo. Sasa hivi yuko wilaya ya Same anachapa mzigo.

  Lisemwalo lipo, kama halipo ........
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nilikuwepo MwembeYanga, pamoja na uchovu wangu wa safari , Dr Slaa alisoma kwenye Taarifa hiyo kwenye Kijitabu cha utekelezaji wa Ilani ya ccm Jimbi la Bagamoyo , taarifa ambayo Kawambwa alimsomea JK alipokua Bagamoyo.
  Dr Slaa , akasisitiza, kama JK alisomewa tarifa hiyo kisha hakuhoji , basi lipo tatizo la namna anavyoelewa mambo, na kama taarifa ilikosewa basi kuna shaka juu ya umakini wa Kawambwa kama Waziri na kama Mbunge , pamoja na Jakaya Kikwete, inaonesha wamekosa umakini, na kielelezo cha viongozi ambao kwaharaka ni sawa na chief Msovelo, niwatuambao hawawezi kutafsiri taarifa, elimu haiwasaidii.
  achukue kile kijitabu allichomsomea Kikwete asome neno kwa neno kisha akanushe, otherwise ni kielelezo cha wapuuzi katika uendeshaji waTaifa hili.
   
 5. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wapi utaweza kujenga choo cha tundu moja kwa laki saba? Makadirio ya haraka haraka kwa kurejea ujenzi huku kwetu mitaani ni kama ifuatavyo: Kuchimba shimo la kina mita 3, upana mita 2 na urefu mita 2 (12 cubic metres of soil) ni Shs 400,000. Kuweka tandiko la chini ni kama Shs laki 2, Matofali ya kujengea shimo kuanzia chini hadi juu mwisho wa shimo ni tofali 400 kila moja shs 700 inakuwa Shs 280,000 na Sementi ya kujengea ni mifuko miine jumla shs 50,000. Kupiga plasta shimo ni mifuko 6 ya shs 80,000. Tandiko la juu ya choo la mita 2.5 x 2.5 likiwa na nondo mm 12 pamoja na kokoto ni Shs 150,000. Kujenga boma ni tofali 200 kwa shs 140,000 na mifuko mminne ya sementi 50,000. Mbao za kuezekea ni 6 za shs 90,000. Bati tatu za shs 45,000, na kupiga plasta boma ni mifuko 6 ya shs 80,000. Ongeza gharama za milango mmoja na komeo (150,00) na dirisha moja (80,000), jumla ndogo tuunapata shs 1,595,000. Ongeza 25 % labour charges inapanda na kuwa shs: 1,993,750/=, na hapo gharama za usafirishaji wa vifaa sijaweka, Watalaam wengine hapa JF watanisaidia.Gharama hizi zikiingizwa kwenye kandarasi ya serikali inaweza kufikia Shs 3,000,000 kwa kila shimo, hapo hujaweka posho za Mkuu wa Idara ya Elimu Wilaya, Mhasibu Mkuu wa wilaya, Afisa Mipango wa wilaya, Mhandisi Wilaya, Mkuu wa Afya Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kuja kukagua kama ujenzi wa chjoo unaendelea vizuri (Shs 1,000,000) na cha mbele / ufisadi milioni kadhaa. Namshangaa mhandisi Kawambwa kwa kutaka kutudanganya ati 700,000 kwa kila shimo.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kawambwa anashindwa kujibu tuhuma za Slaa kwa hoja zenye mantiki, Slaa amesoma taarifa aliyoisaini yeye.
   
 7. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kazi kwelikweli..
   
 8. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Je, tutafika?
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Dokta hakubeep ila alituma message. Ahsante Kakajambazi kwa kutujulisha kwamba ujumbe umefika.
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kumbe yule ni mdogo wako..........
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kawambwa alichosoma Slaa ni kama andiko toka kwa Bible huwezi kulipinga unless uedit iyo report
   
 12. J

  Jafar JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haswa ni mdogo wangu !!!!!
   
 13. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Kawambwa amesema kuwa shule tano kule bagamoyo zilitengewa shilingi laki 7 kila moja kwa kila moja kujenga choo ya matundu manne. Kwa sababu hiyo jumla ya fedha zote zilizotengwa ni sh. milioni 3.5 NA SIYO SHILINGI BILIONI 3.5 alizozichakachua padre Slaa. Ukweli pekee ndio utakaotuweka huru na sio ghirba ama kuchakachua takwimu.!!!
   
 14. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Okay safi sana..........
   
 15. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni afadhali Mheshimiwa Kawambwa angekaa kimya kuliko kuendelea kuchochea moto kwenye jambo ambalo ufisadi wa wazi umeonekana.

  Wamejisahau mpaka wanataja figures za kifisadi mbele ya wananchi bila aibu. Hiyo ni kashfa kubwa na alitakiwa Waziri-at minimum- asimamishe kazi wahusika wote na kupitisha uchunguzi mkali kuhusiana na matumizi ya pesa hizo.
   
 16. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Choo gani hicho cha laki 7? kwa gharama za sasa za ujenzi au za 2005?

  Kama ni gharama za sasa, hivyo vyoo ni hatari kwa maisha ya wanafunzi.
   
 17. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Kaka huu uchambuzi wako nimeupenda kweli kweli na utanisaidia kujenga choo changu nje cha main house, Ndugu yangu unajua nini, wanasiasa wanatudharau kwa kupitia watu kama Prof Maghembe,Kawambwa,Chegeni na Kamala kwani analysis zao na majibu yao sio ya kitaalamu hata kidogo, mtu hata hajaenda shule kwa maisha ya sasa huwezi kumuambia unaweza jenga kujenga tundu la choo kwa laki 7 tu na maisha haya mfuko wa siment tsh 15,000/=, SHAME ON YOU KAWAMBWA,Nenda kamuone Utoh mdhibiti wa matumizi ya serikali akueleze akuzodoe sio kutuletea siasa za kifisadi hapa nyau weeee, Mwaka huu mtatafuta choo maana :rip:CCM.HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII,2010.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wenzao kwenye herufi huwa wanakosea kuongeza labda sifuri moja.. lakini kuongeza sifuri tatu, kuzitamka hivyo bila kujihoji kichwani ni dalili mbaya
   
 19. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo anamsahihisha CAG na CAG report!
   
 20. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  he! tuna wahandisi humu, si mchezo!
   
Loading...