Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,650
- 21,011
Nimesikia kuwa PM Majaliwa amewaagiza mawaziri wa kilimo, biashara na mwingine gani sijui, wakae na kuja na mpango kwaajili ya kilimo. Nawaza sijui watakuja na kaulimbiu gani. Hii ni historia fupi ya kaulimbiu za kilimo.
1.Siasa ni kilimo, azimio la Iringa.
2. Kilimo cha kufa na kupona.
3. Chakula ni uhai.
4. Ukulima wa kisasa
5.Kilimo kwanza.
Kwa kweli hizo zote zimefeli. Kwa maoni yangu, ili kilimo kifanikiwe kifanywe huria. Tuvunje hivyo vyama vya ushirika, watu wakitaka ushirika waunde wenyewe kwa hiari zao. Mtu awe huru kuuza mazao yake atakako. Mnunuzi yeyote aruhusiwe kununua. Kodi na tozo kwenye mazao zipunguzwe, ziwe za chini kabisa. Wananchi wanajua jinsi ya kulima. Wakiwa na uhakika wa kurudisha mitaji yao na kupata faida, yatatokea mapinduzi makubwa kabisa ya kilimo katika nchi hii.