Kauli za wanasiasa sawa na Jogoo na tetea

Kauli za wanasiasa sawa na Jogoo na tetea

whitehorse

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2009
Posts
2,572
Reaction score
4,455
Kauli za wanasiasa huwa zimejaa ulaghai mithili ya jogoo linapotaka kumpanda tetea. Tukio la jogoo kumpanda tetea (hawa ni wale kuku wetu wa asili ama maarufu kama kuku wa kienyeji. Sio wale yatima)

Wengi tunajua kinachotokea kabla tetea hajapandwa. Huwa anatafutiwa vyakula laini laini jogoo anatufuta ardhini wadudu walionona na vyakula vyenye mvuto kisha humuita tetea wake kwa muito wa mahaba na tetea husogea mbio kula vinono. Hizi ni kauli za wanasiasa wakiwa majukwaani ZINATAMANISHA SANA

Jogoo hushusha bawa lake moja kwa mbwembwe huku anamzunguka tetea kwa mikogo mingi. Babu yangu aliniambia zamani sana nikiwa bado mdogo kuwa anamwambia tetea "nitakununulia gauni refu mpaka chini" tetea hulaghaika na kukubali kupandwa. Kuna matetea wabishi huwa wanakula na kuahidiwa magauni marefu lakini wakitaka kupandwa huwa wanakimbia sana na kusababisha jogoo kukatiza mitaa kukimbiza huyu tetea hadi ampande.
Vivyo hivyo kauli za wanasiasa ni ULAGHAI . Wanaolaghawa wengine hukimbia lakini mwishowe huishia kupandwa vilevile.

Utafutaji wa chakula cha hongo ili tetea alainike, kuburuza bawa chini kwa mbwembwe na hata kukimbiza tetea yote haya huwa ni harakati za matayarisho ya kumpanda tetea. Hata hivyo muda wa jogoo kujinafasi juu ya tetea ni sekunde 5 tu. Jogoo humpanda tetea akimaliza sekunde zake tano anashuka na anasahau kila kitu hadi zile ahadi za magauni marefu. Vivyo hivyo kauli za wa nasiasa ni WASAHAULIFU

Baada ya sekunde tano jogoo akimaliza starehe yake hakuna gauni refu wala fupi bali huwaendea tetea wengine na kuwalaghai kwa style ile ile na kuwapanda kisha akastarehe sekunde tano akashuka na kuendelea na maisha mengine.
Vivyo hivyo Wanasiasa hutumia kauli zile zile mara zote hawana jipya.

katika hali maisha ya kawaida ahadi zisipotekelezwa hutengeneza hasira. Hata teta nae hupandwa na hasira za ahadi hewa tumeshuhudia tetea alomstarehesha jogoo kuwapiga na kuwakimbiza tetea wenzake wanaolaghaiwa na jogoo lile tapeli.
Kazi kubwa sana hii maana tetea wengi hukubali kulaghaiwa zaidi . Tetea mwenye hasira hupata ugumu wa kuoigana nao maana wakati mwingine hata jogoo lile lile humpiga na kumfukuzia mbali. Tetea huishia kupiga makelele mengi akitangaza kuwa keshalaghaiwa na sasa ana taka kutaga yale matokeo ya kulaghaiwa. Makelele haya huwa ghasia kwa jogoo na mara zote jogoo humfukuzia mbali tetea anayepiga makelele au kutoa sauti za miguno ya mshtuko na kebehi. Mwisho tetea huishia kuatamia mayai yake bandani bila magauni marefu wala kutafutiwa vyakula vinono. Huku jogoo likiendelea kulaghai na kupanda na kushuka migongoni mwa matetea wengine wengi. Na mara chache jogoo hili hufikia hatua ya kujeruhi hata kuwatoa damu majogoo mengine yanayojaribu kuingilia matetea yake . Japokuwa wote wanatumia mtindo mmoja ule ule wa kulaghai.

Kauli za wanasiasa huwa ni za muda mfupi sana na hazitoshelezi shauku ya miaka mingi kama ile shauku ya tetea kununuliwa gauni refu sana hadi miguuni.


Akili zangu zimeniletea MAJOGOO NA MATETEA WENGI SANA.

Anaandika : #mjukuuwababu#
f5115279c411de49f6ca80c1fcac05eb.jpg
 
Back
Top Bottom