Kauli za Kishujaa na zisizo na Unafiki za Mwandishi Moses Mathew, Mungu ambariki maradufu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Akizungumza asubuhi ya leo katika Kipindi pendwa cha Tuongee Asubuhi Jicho la Habari cha kila Jumamosi kinachorushwa na Kituo bora cha Runinga ( Television ) cha Star Tv Mwandishi wa Habari Mkongwe wa Magazeti ya Serikali ( Daily News ), Mtaalam wa Mawasiliano, Mwanaharakati na Mwalimu pia wa Tasnia ya Habari Moses Mathew leo ametoa Kauli za Kishujaa kabisa ambazo Mwanaharakati Cyprian Musiba na Mamlaka husika ( Serikali ) wanatakiwa wazipokee na wazifanyie Kazi kwa Afya ya Usalama na Ustawi mzima wa Mama Tanzania yetu.

Sitoandika mengi leo ila nitaweka tu hapa Nukuu za Kauli zake hapa ambazo Mwandishi huyu Mkongwe Moses Mathew amezilenga sehemu Kuu tatu ambapo ya Kwanza ni kwa Mwanaharakati Cyprian Musiba, Mamlaka husika ( Serikali ) na kwa Waandishi wa Habari ( hasa hasa akiwalenga hawa wa Mitandaoni ) ambao ndiyo wanaonekana kuwa na matatizo ya Kiuweledi mno na ya mwisho akieleza Msimamo wake kama Mwanataaluma.

Nimwombe tu huyu Mmiliki wa Tanzanite Tv ( akimaanisha Cyprian Musiba ) kwamba abadilike na aina ya Sumu yake Kubwa ya Kihabari anayoipandikiza ndani ya Vichwa vya Watanzania. Kinachonisikitisha zaidi huyu Mtu ni Mwandishi wa Habari Mwenzetu ila sijui kama hiki anachokifanya sasa ndiyo Maadili aliyoyasoma alipokuwa Chuoni. Kama unasema na unajiamini kabisa kuwa una Ushahidi wa Tuhuma kuna haja gani ya Wewe kuja Kuwadhalilisha Watu badala ya Kuupeleka huo Ushahidi wako katika Vyombo husika vya Kiusalama ili wachukuliwe hatua? Kama kuna Mtu ambaye anamtumikia na ndiyo anamtuma hivi basi ajue anajiharibia mno kwani kwa Kipindi kifupi tu tokea aanze hizi harakati zake amesababisha Hofu kubwa sana ndani ya Watanzania kitu ambacho si Kizuri

Niiombe tu Serikali husika hasa Waziri na Msemaji wa Serikali ambaye namtambua kuwa ni Mtu Mweledi na Msomi mzuri sana Abbas waingilie hili kati kwani Mimi Moses Mathew ambaye kila Siku nazunguka huku na kule katika Majukumu yangu haya ya Habari nakutana na Maswali mengi juu ya huyu Cyprian Musiba na bahati nzuri hata hao ambao wananiuliza ni Watu wazito tu katika nchi hii, wanashangaa na wanasikitika huku wakisema Tanzania inakoelekea huenda yakawa ni makubwa hata ya yale tuliyoyashuhudia huko Rwanda na Burundi. Huyu Cyprian Musiba anaweza akawa ana Hoja kweli au Madai ya Msingi ila Serikali nayo iwe inaingilia kati katika kuyapima na hata kuyaruhusu yaende Masikioni mwa Watanzania kwani yana Madhara makubwa kuliko wao wanavyodhani

Nitoe Ombi langu Kubwa sana kwa Waandishi wa Habari hasa hawa wa Mitandaoni kwamba waache Kufanya Kazi zao ( Majukumu yao ) Kinyume na Maadili na Taratibu za Tasnia kwani kama wangekuwa makini na wameiva kweli kamwe wasingekuwa wanawalisha Watanzania Taarifa zenye Chuki, Ubaguzi na Kuwagawa huku wao wakiona ndiyo wanafanya vyema. Navipongeza sana Vyombo viwili vya Habari za Mitandaoni cha Michuzi Blog na Millard Ayo ( japo nae ana Mapungufu machache ) ila angalau anajitahidi kwa sasa kwa Uandishi wao mzuri na uliojaa Uweledi mkubwa na unaofuata Maadili lakini vinginevyo vilivyobaki nashangaa kuona vipo hewani na bado TCRA wanavilea huku wakijua fika kuwa vinaharibu Ustawi wa Watanzania hasa wale ambao wanapata taarifa zao

Lazima ifike muda Watu watambue kuwa Uandishi wa Habari ni Tasnia tena Kubwa sana na inayoheshimika mno duniani kote na ndiyo maana mnaona tunaenda Shule Kuisomea kwa Miaka Mitatu na kama haitoshi wapo Watu wana Masters na hadi PhD’s za hii Tasnia hivyo hatuwezi Kuona Watu wachache wanataka Kuiharibu na Kufanya tuonekane Wapuuzi kama Wao halafu tukanyamaza hii haiwezekani na tutalipambania. Sijaumbwa kuwa Mnafiki au Muoga wa Kusema Ukweli juu ya Jambo lolote lile na wengine tunapokuwa tunayasema haya jueni kuwa Sisi ndiyo tunakutana na Sehemu kubwa ya Watanzania walio katika ngazi za huku chini ambao kiukweli wamejawa na wasiwasi mkubwa sana juu ya Tanzania yao. Ni imani yangu Ndugu Cyprian Musiba ( ambaye namheshimu mno ) atayatafakari haya kwa Kina na nimeyasema haya hapa Kiuwazi ili ajue Uchungu tulionao Sisi wana Tasnia wenzake juu ya hiki anachokifanya na naamini atabadilika

Kamarada Moses Mathew kama kuna Siku ambayo umeonyesha kuwa kweli Wewe ulipikwa vyema na Chuo Kikuu cha SAUT na uliiva vizuri Kitasnia hii ya Habari, Utangazaji na Mawasiliano basi leo. Na binafsi kama cleverbright niseme wazi kabisa Kwako kwamba nami kama kuna Mwanahabari ambaye namkubali na kila nikiona amealikwa Star Tv katika Kipindi chao hiki cha Jumamosi na hata vingine basi ni Wewe Moses Mathew. Uko tofauti na Waandishi wa Habari wengi sana hapa Tanzania na unapotumaliza wengi ni kwamba umetokea na bado unafanyia katika Gazeti la Serikali la Daily News na umekuwa Mwandishi Mwandamizi ( wa muda mrefu ) ila huwa huna Unafiki wala Uwoga hata kama ukiwa unachambua Mapungufu ya Serikali ambayo ndiyo inakulipa. Sifa yako kubwa ni kwamba huwa hufanyi mno Criticism kama wengine bali Wewe huwa unafanya Kitu Kizuri Kiitwacho Critique ambapo huwa unaanza Kukosoa Jambo lakini baadae unatoa Ushauri ( Mapendekezo ) na pale ambapo huwa unaona panastahili Sifa pia huwa unatoa tena Kiuwazi kabisa.

Kwa hizi Kauli zako za leo namuomba sana Mwenyezi Mungu akubariki, akulinde na akuzidishie Mafanikio Kamarada wangu.
 
Akizungumza asubuhi ya leo katika Kipindi pendwa cha Tuongee Asubuhi Jicho la Habari cha kila Jumamosi kinachorushwa na Kituo bora cha Runinga ( Television ) cha Star Tv Mwandishi wa Habari Mkongwe wa Magazeti ya Serikali ( Daily News ), Mtaalam wa Mawasiliano, Mwanaharakati na Mwalimu pia wa Tasnia ya Habari Moses Mathew leo ametoa Kauli za Kishujaa kabisa ambazo Mwanaharakati Cyprian Musiba na Mamlaka husika ( Serikali ) wanatakiwa wazipokee na wazifanyie Kazi kwa Afya ya Usalama na Ustawi mzima wa Mama Tanzania yetu.

Sitoandika mengi leo ila nitaweka tu hapa Nukuu za Kauli zake hapa ambazo Mwandishi huyu Mkongwe Moses Mathew amezilenga sehemu Kuu tatu ambapo ya Kwanza ni kwa Mwanaharakati Cyprian Musiba, Mamlaka husika ( Serikali ) na kwa Waandishi wa Habari ( hasa hasa akiwalenga hawa wa Mitandaoni ) ambao ndiyo wanaonekana kuwa na matatizo ya Kiuweledi mno na ya mwisho akieleza Msimamo wake kama Mwanataaluma.

“ Nimwombe tu huyu Mmiliki wa Tanzanite Tv ( akimaanisha Cyprian Musiba ) kwamba abadilike na aina ya Sumu yake Kubwa ya Kihabari anayoipandikiza ndani ya Vichwa vya Watanzania. Kinachonisikitisha zaidi huyu Mtu ni Mwandishi wa Habari Mwenzetu ila sijui kama hiki anachokifanya sasa ndiyo Maadili aliyoyasoma alipokuwa Chuoni. Kama unasema na unajiamini kabisa kuwa una Ushahidi wa Tuhuma kuna haja gani ya Wewe kuja Kuwadhalilisha Watu badala ya Kuupeleka huo Ushahidi wako katika Vyombo husika vya Kiusalama ili wachukuliwe hatua? Kama kuna Mtu ambaye anamtumikia na ndiyo anamtuma hivi basi ajue anajiharibia mno kwani kwa Kipindi kifupi tu tokea aanze hizi harakati zake amesababisha Hofu kubwa sana ndani ya Watanzania kitu ambacho si Kizuri “

“ Niiombe tu Serikali husika hasa Waziri na Msemaji wa Serikali ambaye namtambua kuwa ni Mtu Mweledi na Msomi mzuri sana Abbas waingilie hili kati kwani Mimi Moses Mathew ambaye kila Siku nazunguka huku na kule katika Majukumu yangu haya ya Habari nakutana na Maswali mengi juu ya huyu Cyprian Musiba na bahati nzuri hata hao ambao wananiuliza ni Watu wazito tu katika nchi hii, wanashangaa na wanasikitika huku wakisema Tanzania inakoelekea huenda yakawa ni makubwa hata ya yale tuliyoyashuhudia huko Rwanda na Burundi. Huyu Cyprian Musiba anaweza akawa ana Hoja kweli au Madai ya Msingi ila Serikali nayo iwe inaingilia kati katika kuyapima na hata kuyaruhusu yaende Masikioni mwa Watanzania kwani yana Madhara makubwa kuliko wao wanavyodhani “

“ Nitoe Ombi langu Kubwa sana kwa Waandishi wa Habari hasa hawa wa Mitandaoni kwamba waache Kufanya Kazi zao ( Majukumu yao ) Kinyume na Maadili na Taratibu za Tasnia kwani kama wangekuwa makini na wameiva kweli kamwe wasingekuwa wanawalisha Watanzania Taarifa zenye Chuki, Ubaguzi na Kuwagawa huku wao wakiona ndiyo wanafanya vyema. Navipongeza sana Vyombo viwili vya Habari za Mitandaoni cha Michuzi Blog na Millard Ayo ( japo nae ana Mapungufu machache ) ila angalau anajitahidi kwa sasa kwa Uandishi wao mzuri na uliojaa Uweledi mkubwa na unaofuata Maadili lakini vinginevyo vilivyobaki nashangaa kuona vipo hewani na bado TCRA wanavilea huku wakijua fika kuwa vinaharibu Ustawi wa Watanzania hasa wale ambao wanapata taarifa zao “

“ Lazima ifike muda Watu watambue kuwa Uandishi wa Habari ni Tasnia tena Kubwa sana na inayoheshimika mno duniani kote na ndiyo maana mnaona tunaenda Shule Kuisomea kwa Miaka Mitatu na kama haitoshi wapo Watu wana Masters na hadi PhD’s za hii Tasnia hivyo hatuwezi Kuona Watu wachache wanataka Kuiharibu na Kufanya tuonekane Wapuuzi kama Wao halafu tukanyamaza hii haiwezekani na tutalipambania. Sijaumbwa kuwa Mnafiki au Muoga wa Kusema Ukweli juu ya Jambo lolote lile na wengine tunapokuwa tunayasema haya jueni kuwa Sisi ndiyo tunakutana na Sehemu kubwa ya Watanzania walio katika ngazi za huku chini ambao kiukweli wamejawa na wasiwasi mkubwa sana juu ya Tanzania yao. Ni imani yangu Ndugu Cyprian Musiba ( ambaye namheshimu mno ) atayatafakari haya kwa Kina na nimeyasema haya hapa Kiuwazi ili ajue Uchungu tulionao Sisi wana Tasnia wenzake juu ya hiki anachokifanya na naamini atabadilika “
Musiba siyo mwanahabari bali anatumikia "alimentary canal" yake tu.
 
Hayo uliyosema ni kweli ila musiba akimsikia huyu jamaa alivyomchambua na vyombo vyake vya habari, huyu jamaa atakiona cha mtemakuni
 
Ooh aangalie wana weza waka muazory gwanda

Hata kama wakimuazori gwanda lakini ukweli wake huu usio na hata Chembe ya Unafiki utaendelea kubaki Mioyoni mwetu. Jamaa ninamkubali mno kwani binafsi huwa napenda Watu ambao siyo Wanafiki, hawaogopi Kufa kwa Kusema Ukweli na huwa hawapindishi Maelezo ( Maneno ) juu ya Jambo husika. Na bahati nzuri Watu kama Moses Mathew na Mimi cleverbright ( ambao kwa bahati mbaya tupo wachache mno hapa duniani ) ndiyo huwa Vipenzi wakubwa wa Mwenyezi Mungu.
 
Hayo uliyosema ni kweli ila musiba akimsikia huyu jamaa alivyomchambua na vyombo vyake vya habari, huyu jamaa atakiona cha mtemakuni

Kwani huyo Musiba akijibu Mapigo kwa Kumkomoa au Kumchafua Yeye atafaidika na nini? Ninachojua tu ni kwamba Watu wengi wanaokubaliana na Musiba na wanaomuamini kwa Upuuzi wake ni Wapumbavu wa Kiwango cha Kimataifa ila labda nikusaidie tu hizi Kauli za huyu Mwandishi wa Habari Mwandamizi Moses Mathew zimepokelewa vyema kabisa na Watanzania wachache wenye Akili nyingi, Upeo mkubwa na Wazalendo wa kweli. Ni kheri Musiba na Kundil lake ( wanaomtuma ) wakuchukie lakini kwa Mwenyezi Mungu ukajulikana kuwa ulisema Jambo jema bila Kificho wala Unafiki kama alivyofanya Moses Mathew leo. Jamaa ( Moses Mathew ) leo amekuwa ndiyo MVP wa Mchezo alipokuwa Mubashara kabisa Star Tv.
 
Back
Top Bottom