Kauli ya Waziri Nyalandu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Waziri Nyalandu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Goheki, Jul 19, 2012.

 1. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeangalia taarifa ya habari Itv,kwa kweli wamechukua muda wa kutosha kuelezea ajali ya meli iliyozama,pia wamehoji watu mbalimbali kuhusu tukio hili.Ilifikia kwa waziri Nyalandu,yeye akasema anashukuru watalii(Wazungu)wametoka salama.Hii nidhamu ya uwoga itaisha lini kwa viongozi wetu kuona wazungu ni bora zaidi.Ni juzi tu mawaziri wawili walikimbilia serengeti baada ya wazungu kuvamia.LAKINI KWA MTZ,USAFIRI HAMNA,MAFUTA HAMNA AU HAKUNA POLISI WA KUTOSHA.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Jomba, weka wazi kuwa ilitolewa helikopta ya jeshi la polisi kuwasaka wezi machakani, hadi wakawapata na vifaa vyote vilivyoibiwa. Huyu ni lazima awahanye wazungu hasa Wamarekani, maana wamemdokeza kuwa atakuwa next president wa Tz. Silly Comment.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  siku hizi hata Wakenya wanatucheka
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Sikuangalia habari ila sitaki kuamini ninachokisoma. Yaani watu over 150 uhakika wa wao kuwa wanaishi haupo lakini huyu bwana anashukuru kuwa watalii wametoka hai? Na ho wengine je?
   
 5. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Is he for real? Nimechoka...........
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nyalandu is a "Mzungu Worshiper" just like JKilaza.
   
 7. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Haya ndio matatizo ya kukalili kazi, kwa kuwa yeye ni naibu waziri wa maliasili na utalii basi kila kitu anataka kukihusisha na utalii! anafikiri ndio ataonekana mchapa kazi! Sijui lini mawaziri wa serikali ya CCM watakuwa na akili!
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Tukiweka unafiki pembeni, huyu Waziri yuko sahihi. Mmesahau Mh. Nyalandu ni Naibu Waziri wa Utalii hivyo interest kubwa kwake kuwa watalii sio ajabu. Hayo mengine wanapaswa kuzungumzia mawaziri na watendaji husika na hasa wa "upande wa pili".

  By the way alikuwa anazungumzia watalii waliotoka Tanganyika kwenda nchi nyingine na pengine wangerudi tena Tanganyika. Hao waathirika wengine ni raia wa nchi nyingine ambao nadhani hawamhusu sana Mh. Nyalandu and in fact kwanza wizara yenyewe si ya muungano. Ukielewa hili wala hutamlaumu Nyalandu - he is absolutely right!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umemaliza kila kitu!
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Dudus,
  You are dead wrong. Kwenye ajali binadamu wote ni sawa. Hakuna cha uzungu au uswahili. This statement was very unfortunate.
   
 11. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyalandu ni shallow na boot licker
   
 12. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Fikra za kutukuza wageni ni tatizo kubwa sana na lina uhusiano wa moja kwa moja na umaskini wa jamii husika. Kwa mtu mwenye kufikiria vizuri, raia wake mmoja ana thamani kuliko wageni au watalii wengi.
  Ili jamii iendelee ni lazima ithamini raia wake kuliko wageni.
  Ustaarabu ni Mwenyeji kuwa daraja la kwanza na wageni wanafuatia, vinginevyo ni sawa na kuwapa mbwa chakula cha watoto!
   
 13. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  wale wale ....walikufa watu kumi na wazungu wawili!
   
 14. b

  bdo JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  sikubaliani na kitendo/tukio la kuwateka wageni waliokuwa katika kambi huko serengeti, na mauaji ya Faru, ila napenda kusema baada ya matukio hiyo imekuwa ni neema na ulaji kwa baadhi walinda amani (vyombo vya dola)polisi na walizi wa game, na kwa upande mwingine imekuwa kero shida na taabu kwa wakazi wano zunguka eneo la Mbuga ya Serengeti. Japokuwa ilitangazwa kuwa waharifu hao walishakamatwa, lakini sasa kinachoendelea ni wananchi katika vijiji jirani na mbuga na hasa eneo la Gurumeti area (mbuga ya wanyama ndani ya mbuga ya wanyama) wanaishi kwa hofu, wanakamatwa kama panzi wanateswa, wanawekwa ndani - na kutolewa kwa hela nyingi, wanabambikiwa nyama za wanyamapori na walinzi wa hifadhi na kuambiwa kuwa ni za wanavijiji hao, vijana wamehama majumbani mwao - wanaishi kwa hofu, wamejificha...yaani ni shida tu, kwa maneno haya ya Naibu waziri basi ninahofia maisha ya wananchi hao, maana hao walinzi wa mbuga wanatumwa na mmliki wa Grumenti Reserve Area (VIP lodge) ili waweze kuwanyanyasa wananchi na kuwatisha..
   
 15. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ha haaa...hili jina inabidi tulitumie sana kuwafikishia salamu hawa watawala wetu.

  MZUNGU WORSHIPER Mh. Lazaro Nyalandu.
   
 16. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Huyu nae si ndo hizo zake unfikiri Dhaifu anampendea nini !! Ni hizo hizo sera za kujikomba. Kwanza anasemaje hivyo wakati hawajaopoa maiti zote na hata hawajui idadi kamili ya abiria ?? Nasikia anajiita mzungu wa singida....!!

   
 17. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Dah ngoja nipite tuu maana hapa unaweza kula ban ! I hope bado hujafika miaka 18 !!

   
 18. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli lakini kwa unafiki, upuuzi, na vitimbwi wanavyofanya hawa jamaa mie naona sawa tu.
   
 19. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dudus kwa hali hiyo,Membe hausiyani tena na wabongo kwa kuwa ni waziri wa Mambo ya nje?
   
 20. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Nausea?????? Na wewe ni kama huyo MZUNGU WORSHIPER ntapata ban bure.........so watalii ni wazungu tu??????
   
Loading...