Kauli ya TAFUTA PESA ni mwelekeo mwingine wa upotofu wa kizazi cha sasa

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Nawasalimu

Kauli hii ya tafuta pesa, imekua si kauli ngeni sana masikioni mwetu au pindi usomapo maandishi imekua ni kauli ya kawaida sana na inakua kwa kasi sana katika wakati wetu huu. Kauli hii kwangu mimi nimeona ikitumika sana hasa katika suala la mahusiano kwani ndio imekua kauli mbiu ya kutafuta pesa kama sehemu ya kuongeza security ya hayo mahusiano au heshima kwa ujumla.

Kutafuta pesa ni vizuri kabisa na ni muhimu kabisa. Lakini sasa kwa jinsi inavyoaminishwa na kushabikiwa hii kauli ya tafuta pesa ndipo tatizo linapoanzia. Kwa nini nasema Haya? Ni kwa sababu kama hizi:

Kwanza, Ndugu zangu nitoe mfano kwenye mahusiano, kuishi na Mwanamke ni kwa akili. Maandiko matakatifu yenyewe yameeleza wazi kabisa na hayakueleza kua ili uishi na Mwanamke ni utafute pesa. Yamesema ishini nao kwa akili 1 petro 3:7. Hivyo neno linasema Wanaume ishini na wake zenu kwa akili na kumpa Mke heshima kama chombo kisicho na NGUVU na Warithi pamoja na neema ya uzima.

Pili, Hiki kinachofanyika cha kauli za kuhamasishana kutafuta pesa kumepelekea Watu wengi kujiingiza katika njia zisizofaa ili mradi tu wapate pesa ili eti wawe na heshima katika jamii. Hali hii imepelekea ubadhirifu mkubwa kufanyika, maisha ya mkumbo, ushirikina na mambo kama hayo kuongezeka na mwisho kupelekea mauti au anguko kubwa. Ninachotaka kusema ni kua, Maisha ni mchakato Ndugu zangu, pesa sio kila kitu kwenye maisha ila ni muhimu kua nazo. Penda kukubali huo mchakato kufanyika kwa utaratibu pasipo papara hadi pale mambo yanapojiset na kumbuka pesa haitoshi, na haitokaa kutosha kamwe.

Tatu, kwa macho ya rohoni, hii kauli ya tafuta pesa ni mpango mkakati wa Shetani na wajumbe wake kuhakikisha Binadamu hapati Mda wa kumtafuta MUNGU Bali ajishughulishe na kutafuta pesa tu na kila Mara awe na mikakati mbalimbali ya kutafuta pesa na badae azitumie kwa Anasa na si kuzitumia pesa hizo kwa kusudi la MUNGU. 1 Wakorintho 10: 26 maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote Viuzajavyo. Na pia ukisoma Mathayo 6: 33 Neno linasema utafuteni kwanza Ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa. Lakini kwa kua Ibilisi amejipambanua na wamtambuwao ni wachache ndio maana kapenyeza ajenda ya tafuta pesa ili Watu wawe mbali na Mungu wao. Na matokeo yake pesa zenyewe haupati na ukipata hazikai na zikikaa zinakutesa bado kwa sababu umezipata nje ya kusudi la Mungu.

Nne, Kauli ya tafuta pesa ni kiashiria cha kushindwa kwa uwajibikaji na kutokutambua nafasi yako na hivyo kujificha kwenye kichaka cha kutafuta pesa. Nimesema Pesa ni Muhimu lakini si kila kitu. Hivyo kushamiri kwa kauli hizi kunaashiria kua pesa ndio kila kitu na ndio kama ngao ya Mwanaume/Mwanamke yeyote kitu ambacho si sahihi. Ni Mara ngapi Umewaza juu ya umuhimu wa akili? Maarifa? Busara? Na kiasi? Basi nakujulisha Pesa ni matokeo ya vitu hivyo hapo juu na bila kua na hivyo vitu hapo juu hata ukiwa na pesa kiasi gani itakua mzigo tu kwako kama mafurushi mengine ya mizigo.

Tano, Ndugu zangu fahamu zetu na akili zetu zimetekwa na shetani nyakati hizi. Na moja ya njia anazotumia kubwa kabisa ni kuteka Fahamu zetu. Na fahamu ikishikiliwa ndipo unaanza kua na fikra kama hizo za Tafuta pesa, tafuta pesa, kataaa Ndoa n.k ni muhimu utambue kua Pesa haijawahi kutosha na hata ukiipata tambua sio yako salama na pona yako ni kuitumia kwa utukufu wa Mungu. Una tafuta pesa ili uheshimike? Heshima hailetwi na pesa. Una tafuta pesa ili Mwanamke akae kwako na akuheshimu? Mwanamke Mwenye akili narudia tena alie na akili hatishwi na pesa yako anatizama akili yako. Tusome mhubiri 5:10, na Marko 4:19 unaweza kusoma ujifunze juu ya matokeo ya kauli za tafuta pesa na uhusiano wake kiimani.

Nachelea kusema kua kutafuta pesa ni vizuri kwani hata vitabu vitakatifu vimeeleza, lakini mawasilisho ya humu mengi yanawasilisha kutafuta pesa kama njia ya kupata heshima, kuthaminika na sifa. Na Mwisho pesa inayotafutwa ni inatafutwa kwa kusudi la maovu na sio wema na kwa kusudi la Mungu. Tutafute pesa lakini pesa hizo zitusaidie kuishi katika kusudi la Mungu.

Kwani pesa bila Mungu ni kazi bure na Maisha yetu hapa Duniani ni Mafupi.

N.B Najua nitaambiwa tafuta pesa yes natafuta mkuu na maarifa ya kuzitumia ni lazima tuwe nayo.

Next thread ni wazee wa Kataa Ndoa na Punyeto.

Karibuni.
 
Nawasalimu

Kauli hii ya tafuta pesa, imekua si kauli ngeni sana masikioni mwetu au pindi usomapo maandishi imekua ni kauli ya kawaida sana na inakua kwa kasi sana katika wakati wetu huu. Kauli hii kwangu mimi nimeona ikitumika sana hasa katika suala la mahusiano kwani ndio imekua kauli mbiu ya kutafuta pesa kama sehemu ya kuongeza security ya hayo

Karibuni.
Nani kapoteza pesa na wapi zilipotelea hadi atafute hizo pesa?

Nani asiyetafuta pesa?

Atafute pesa kwa kiwango gani?

Nani na lini aliacha kutafuta pesa?

Pesa kiasi gani ziliwahi kutosheleza mahitaji?

Mambo ya kidunia bila ya kumcha Mungu yote ni ubatili mtupu au ni sawa na kujilisha upepo.
 
Nawasalimu

Kauli hii ya tafuta pesa, imekua si kauli ngeni sana masikioni mwetu au pindi usomapo maandishi imekua ni kauli ya kawaida sana na inakua kwa kasi sana katika wakati wetu huu. Kauli hii kwangu mimi nimeona ikitumika sana hasa katika suala la mahusiano kwani ndio imekua kauli mbiu ya kutafuta pesa kama sehemu ya kuongeza security ya hayo mahusiano au heshima kwa ujumla.

Kutafuta pesa ni vizuri kabisa na ni muhimu kabisa. Lakini sasa kwa jinsi inavyoaminishwa na kushabikiwa hii kauli ya tafuta pesa ndipo tatizo linapoanzia. Kwa nini nasema Haya? Ni kwa sababu kama hizi:

Kwanza, Ndugu zangu nitoe mfano kwenye mahusiano, kuishi na Mwanamke ni kwa akili. Maandiko matakatifu yenyewe yameeleza wazi kabisa na hayakueleza kua ili uishi na Mwanamke ni utafute pesa. Yamesema ishini nao kwa akili 1 petro 3:7. Hivyo neno linasema Wanaume ishini na wake zenu kwa akili na kumpa Mke heshima kama chombo kisicho na NGUVU na Warithi pamoja na neema ya uzima.

Pili, Hiki kinachofanyika cha kauli za kuhamasishana kutafuta pesa kumepelekea Watu wengi kujiingiza katika njia zisizofaa ili mradi tu wapate pesa ili eti wawe na heshima katika jamii. Hali hii imepelekea ubadhirifu mkubwa kufanyika, maisha ya mkumbo, ushirikina na mambo kama hayo kuongezeka na mwisho kupelekea mauti au anguko kubwa. Ninachotaka kusema ni kua, Maisha ni mchakato Ndugu zangu, pesa sio kila kitu kwenye maisha ila ni muhimu kua nazo. Penda kukubali huo mchakato kufanyika kwa utaratibu pasipo papara hadi pale mambo yanapojiset na kumbuka pesa haitoshi, na haitokaa kutosha kamwe.

Tatu, kwa macho ya rohoni, hii kauli ya tafuta pesa ni mpango mkakati wa Shetani na wajumbe wake kuhakikisha Binadamu hapati Mda wa kumtafuta MUNGU Bali ajishughulishe na kutafuta pesa tu na kila Mara awe na mikakati mbalimbali ya kutafuta pesa na badae azitumie kwa Anasa na si kuzitumia pesa hizo kwa kusudi la MUNGU. 1 Wakorintho 10: 26 maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote Viuzajavyo. Na pia ukisoma Mathayo 6: 33 Neno linasema utafuteni kwanza Ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa. Lakini kwa kua Ibilisi amejipambanua na wamtambuwao ni wachache ndio maana kapenyeza ajenda ya tafuta pesa ili Watu wawe mbali na Mungu wao. Na matokeo yake pesa zenyewe haupati na ukipata hazikai na zikikaa zinakutesa bado kwa sababu umezipata nje ya kusudi la Mungu.

Nne, Kauli ya tafuta pesa ni kiashiria cha kushindwa kwa uwajibikaji na kutokutambua nafasi yako na hivyo kujificha kwenye kichaka cha kutafuta pesa. Nimesema Pesa ni Muhimu lakini si kila kitu. Hivyo kushamiri kwa kauli hizi kunaashiria kua pesa ndio kila kitu na ndio kama ngao ya Mwanaume/Mwanamke yeyote kitu ambacho si sahihi. Ni Mara ngapi Umewaza juu ya umuhimu wa akili? Maarifa? Busara? Na kiasi? Basi nakujulisha Pesa ni matokeo ya vitu hivyo hapo juu na bila kua na hivyo vitu hapo juu hata ukiwa na pesa kiasi gani itakua mzigo tu kwako kama mafurushi mengine ya mizigo.

Tano, Ndugu zangu fahamu zetu na akili zetu zimetekwa na shetani nyakati hizi. Na moja ya njia anazotumia kubwa kabisa ni kuteka Fahamu zetu. Na fahamu ikishikiliwa ndipo unaanza kua na fikra kama hizo za Tafuta pesa, tafuta pesa, kataaa Ndoa n.k ni muhimu utambue kua Pesa haijawahi kutosha na hata ukiipata tambua sio yako salama na pona yako ni kuitumia kwa utukufu wa Mungu. Una tafuta pesa ili uheshimike? Heshima hailetwi na pesa. Una tafuta pesa ili Mwanamke akae kwako na akuheshimu? Mwanamke Mwenye akili narudia tena alie na akili hatishwi na pesa yako anatizama akili yako. Tusome mhubiri 5:10, na Marko 4:19 unaweza kusoma ujifunze juu ya matokeo ya kauli za tafuta pesa na uhusiano wake kiimani.

Nachelea kusema kua kutafuta pesa ni vizuri kwani hata vitabu vitakatifu vimeeleza, lakini mawasilisho ya humu mengi yanawasilisha kutafuta pesa kama njia ya kupata heshima, kuthaminika na sifa. Na Mwisho pesa inayotafutwa ni inatafutwa kwa kusudi la maovu na sio wema na kwa kusudi la Mungu. Tutafute pesa lakini pesa hizo zitusaidie kuishi katika kusudi la Mungu.

Kwani pesa bila Mungu ni kazi bure na Maisha yetu hapa Duniani ni Mafupi.

N.b Najua nitaambiwa tafuta pesa yes natafuta mkuu na maarifa ya kuzitumia ni lazima tuwe nayo.

Next thread ni wazee wa Kataa Ndoa na Punyeto.

Karibuni.
Ni kamsemo ka watu maskini kujifariji.
 
Tafuta kwanza pesa na hayo mengine utazidishiwa, kauli ya tafuta pesa inatia hamasa na kupunguza maneno mengi na kujieleza sana kwa sisi ambao tumeupitia umaskini. Hakuna hekima, hakuna amani, hakuna upendo sehemu yenye njaa. Unakubali kauli ya tumtafute Mungu ila unapinga kauli tutafute pesa. Binafsi sina haja ya kumtafuta Mungu kwa sababu siamini kuwa Mungu kajificha. Nikiwa na pesa nikisaidia mwenye uhitaji nimeshampata Mungu. Mungu ni kila unachokiona: miti, mito, watu na hata wanyama.
 
Tafuta kwanza pesa na hayo mengne utazidishiwa , kauli ya tafuta pesa inatia hamasa na kupunguza maneno mengi nakujieleza sna kwa sisi ambao tumeupitia umaskin,hakuna hekima , hakuna amani ,hakuna upendo sehemu yenye njaa.unakubali kauli ya tumtafute Mungu ila unapinga kauli tutafute pesa ,Binafsi sina haja ya kumtafuta Mungu kwa sababu siamin kuwa Mungu kajificha , nikiwa na pesa nikasaidia mwenye uhitaji nmeshampata Mungu ,Mungu ni kila unachokiona miti ,mito watu na hata wanyama .
Ubaya unakuja wanayo itumia hiyo kauli haya pesa hawana hatuoni wakizitafuta😅
 
Back
Top Bottom