Kama unataka Kaptula tafuta Kaptula sio Suruali ili Uikate.....

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,466
19,496
Hizi kauli za huyu anatumia muda na pesa kujiremba, wakati ulimkuta anapendeza na unajua kupendeza huko gharama nadhani ni kupotoka kutaka kumbadilisha....; Fulani kila siku anatumia muda kuangalia mipira wakati ulimkuta kwenye mpira ulivyomsindikiza rafiki yake.....; Kwamba hajui kutafuta pesa..., Kwani ulitaka business partner?

Sijui fulani hajui kupika au mvivu; kwa dunia ya sasa kama pesa unayo tafuta mpishi, yeye aendelee kukupa kingine ambacho anacho; Kosa ni pale kudhani unaweza kumbadilisha mtu tabia, cha maana angalia vipaumbele vyako wewe na chagua kuanzia mwanzo hata kama mara chache unapenda suruali isifike chini unaweza kuikunja ila kama ni mtu wa suruali alafu unanunua kaptula sidhani kama unaweza kuigeuza kuwa Suruali....

Ni hayo tu...., To each their Own.....
 
Wanaume wa Dar wanajua kutoa vichambo.

Acha wa mkoani tukakate mkaa.
Kwa afya ya maisha yako ni bora ukapata wakata mikaa wenzako na kama ni vinginevyo usichukue muuza sura au mtu wa Dar (as you call them) ukadhani utambadilisha akawe mkata mkaa (unless unataka variety wewe uendelee na mkaa wako na yeye anachofanya mkutane kwenye kinachowaunganisha)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom