Kauli ya RPC wa Mbeya juu ya maandamano ya CHADEMA

Kauli ya RPC wa Mbeya juu ya maandamano ya CHADEMA

mhalisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
1,181
Reaction score
322
Mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi, Ahmed Msangi alisema wafuasi na viongozi Chadema watakaothubutu kuandamana atawafanyia kitu kibaya ambacho hawatakisahau maishani.

Alisema maandamano hayo ni batili na yalipigwa marufuku kwa sababu hayana maana hivyo atakayethubutu kuandamana atakutana na kitu ambacho atakijutia.


“Nasema hivi, watu wenye akili timamu za kuchanganua mambo, wamepeleka kesi mahakamani kupinga mchakato wa Katiba, sasa Chadema kwa nini waingie barabarani kama si kutaka kuleta fujo?

“Chadema wanatuchokoza na ninasema wakithubutu kuandamana … bora nifukuzwe kazi, lakini kitu nitakachowafanyia hawatanisahau maishani mwao.”

source: Mwananchi



kauli kama hii wadau tunaiongeleaje?
 
Hata mimi nikikutana na mwandamanaji nitakachomfanya hatasahau maisha yake yote.
 
Tunatak viongozi kama hawa safi sana watandikwe mpaka wapasuke kabisa chadema wajinga sana.
 
ukikaa na rpc wa mbeya ahmed msangi ni mtu poa na anaushauri mzur sana ktk maisha na shughuli mbalmbal za kijamii na anamalengo ya kuifanya mby kuwa mahala pazur kwa biashara kwa kudumisha amani na utulivu ila machizi yatakayoandamana hata mimi ntayafanya ki2 mbaya zaid ya msangi
 
Katika msafara wa mambo kenge hakosi,haya yanayosaport kauli mbovu kama hiyo ni u-zuzu,kwa sababu mtu anayeongoza na kuusimamia umma hawezi toa kauli kama hiyo!
 
Poleni saaana,hivi uwanajiuliza watu kama hawa walisoma wapi, wanafamilia, wana wazazi ,wana elewa, wanaishi, wanaishi na jamii? Hivi wanakumbuka kilichotokea wakati waafrika walipokuwa wanadai uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe? Nakumbuka Sharpvillemascre. Haya mabwanyenye wanayofanya wasidhani ni mapya.
 
Kila siku tunasikia wakisema wanatumia weledi katika kazi zao za kila siku. sasa sijui kama huu ndio weledi wenyewe wanaofundishana na mabosi wao. maana kila siku utasikia sisi tunafanya kazi kwa weledi.lakini kila kukicha utasikia raia amewekewa fuvu la kichwa na askali. Msangi ningekuelewa na kukusapoti kama ungetoa kauli hii dhidi ya majambazi na wanaoukata na kuuwa albino
 
CDM walichemka kuitisha maandamano bila kukaa na kuhusisha vyama vinavyonda ukawa .
Sasa wananchi wamewasusia wana CDM wachache.
 
Kupambana kwa nguvu zote na Upinzani ili kutafuta kupandishwa cheo, kwa kufuata mfano wa Mahita!!
 
HUYU JAMAA NAMKUMBUKA KWA KUZIMA MAANDAMANO YA SHEIHE PONDA DAR.ALITOA ONYO ASUBUHI KWENYE TBC TV.Alinikera sana wakati ule,jeshi la POLISI lilitupiga sana,lkn hawa CDM WAPIGWE TU.
 
CDM walichemka kuitisha maandamano bila kukaa na kuhusisha vyama vinavyonda ukawa .
Sasa wananchi wamewasusia wana CDM wachache.

Wala usiwalaumu chadema kwa kuitisha maandamano bila kuwashirikisha ukawa. Wamefanya hivyo ili kupata tathmini kama bado chama kina uhai au ndo kipo mochwari baada ya mgogoro na zimwi la ZITTO kuwaandama.

Yaani walichokifanya ni kama kile wao wanachokilalamikia kwenye MUUNGANO kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano.

Hao wanafiki tumeshawazoea. Wanapenda (ku)kinena kile wasichopenda kutenda.
 
Msangi mzee wa kung'oa kucha! Jamaa katili sana!
kauli yake inathibitisha hilo,mapolisi wengi walishaacha kutumia akili zao siku nyingi vyao ni vitisho na kukusanya rushwa jeshi hili lina makamanda wachache sana wanaotumia weredi km kamanda SIRO.
 
Ahmed Msangi ni yule aliyemtuma Ulimboka Mabwe Pande na alifanyizia na Mbeya wanajua aendelee kupima maji kwa kijiko , hiyo ni Mbeya na kauli yake imesikika na Kumbukumbu watu wanazo hata fukuzwa kazi bali atifika kunakostahili
 
Back
Top Bottom