Kauli ya Rais kusali siku tatu imetafsiliwa kinyume,Makanisa yanafurika na kuongeza maambukizi. Serikali ichukue hatua

Ata epicentre ya Italy kwenye Coronavirus ilikuwa Lombardy na chanzo ni champions league match ya Atlanta na Valencia. Watu kibao walienda kwenye match ilifanyikia Milan baada kuona uwanja wao usingetosha kilochofuata wataliano awawezi sahau.

Pamoja na makelele yote, athari zote lakini hakuna mtu mwenye sauti ya kuzuia haya maombi ama kweli madaraka ya raisi kwenye katiba yanatisha basi mtu anaipiga nchi kiberiti hakuna mwenye uthubutu wa kukemea.
 
Hao watumishi wa Mungu wanaoonekana kuitumia hii nafasi ya siku tatu za maombolezo kwa upande wangu siwezi kuwalaumu, kwasababu hiyo ndio kazi yao, hivyo tuwaache tu watekeleze wajibu wao.

Hapa ni vyema serikali ingeweka hata condition moja kwa waumini wanaoenda misikitini na makanisani, ni vyema kila mmoja awe na mask ili kujilinda yeye na kumlinda jirani yake wakati wa ibada.

Kusema watu wahudhurie ibada ila muda wa ibada ndio umepunguzwa hili kwangu halina maana, kwasababu sidhani kama huyo virus wa Corona anahitaji saa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, atakuwa ana -shift kwa muda mfupi zaidi, hivyo kusema tu muda wa ibada upunguzwe bado siioni kama njia nzuri ya kujikinga na maambukizi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mask kwenye kunena kwa roho. Mkuu tungebaki majumbani tukasali na kuomba jumapili ni siku mpya ya kuongezeka kwa maambukizi au hawataki uchaguzi ufanyike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa wanahangaika na watu bar huku tatixo ni mkusanyiko wakati kwenye ibada watu wamejaa siamini kama Tanzania tumefikia hatua hii ya kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwenye janga kama hili
 
Bams,
Pangekuwepo na wasaidizi wa rais, wakasoma hii kitu uliyoweka hapa, na wao wakaichukua na kumpelekea na kumsihi wayajadili yaliyomo...

Sina la zaidi ya hapo. Nitachafua uzi mzuri kabisa.

..mimi siamini kama haya aliyoandika barafu bwana mkubwa au wasaidizi wake hawayafahamu.

..pia siyo mara moja bwana mkubwa ametoa kauli halafu ikabidi kauli hizo zitafsiriwe au ziwekwe sawa/ vizuri.

..na mara zote bwana mkubwa huwa yuko sahihi, tatizo ni wananchi kushindwa kumuelewa anamaanisha nini.

..kwa kweli kinachoendelea kinashangaza.
 
..mimi siamini kama haya aliyoandika barafu bwana mkubwa au wasaidizi wake hawayafahamu.

..pia siyo mara moja bwana mkubwa ametoa kauli halafu ikabidi kauli hizo zitafsiriwe au ziwekwe sawa/ vizuri.

..na mara zote bwana mkubwa huwa yuko sahihi, tatizo ni wananchi kushindwa kumuelewa anamaanisha nini.

..kwa kweli kinachoendelea kinashangaza.
Na hiki ndio kipimo sahihi cha kujua ni maisha ya aina gani waTanzania wanayoyaishi kiutawala.

Mtawala ana haki zote za kufanya lolote, hata linalohatarisha maisha yao na hakuna yeyote anayeweza kuhoji chochote.

Hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana.

Huenda hizi ni hatua tunazopaswa kuzipitia kabla hatujafika huko pa kuwahoji wanaotutawala.

Hivi kweli tutapita hivi hivi tu katika majambo kama hili tusiweze hata kujifunza chochote cha maana kwenda mbele?
 
Nakuunga mkono Barafu, binafsi nashindwa kuelewa kwa nini serikali inafumbia macho suala la mikusanyiko ya dini, tofauti na case ya kanisani huko South Korea kuna waislam zaid ya 600 waliambukizwa huko Kuala Lumpur around march 18, na pia kulikuwa na case ya namna hiyo huko Indonesia. Wakati watu wanapokusanyika ndipo huyu virus asiyeonekana naye anasambaa bila waumini kujua. Mikusanyiko hii ya kanisa inawaleta pamoja watu wote ikiwamo hata wanafunzi, kuna mikusanyiko ya kweny masoko, baani, na kweny sherehe za usiku nk serikali ingejitahidi kupunguza haya mambo, ni agents ya kusambaza ugonjwa, pia ni vema wananchi wakashauriwa kuvaa mask,zinasaidia sana hasa kwa approach tunayoitumia ya kuendela na shughuli za kila siku (mask inazuia mgonjwa asimuambukize mwingine, au asiye mgonjwa asiambukizwe, na pia inamsaidia mtu asijishike kweny pua mahala ambapo virus anaweza kuingia kirahis kweny mifumo ya upumuaji). Na urahisi wa ugonjwa huu ni kuwahi kuchukua hatua, unaweza kuchelewa madhara yakawa makubwa lakini hatua lazima uchukue. Kwa maelezo ya Mh. waziri wa afya, mpk sasa hajui suspected ni wangapi, wako wapi maana anategemea watu wanaojisikia kuwa na hizi homa wajipeleke Amana, kwa namna hii vita tumeishindwa. Issue ingine ya kufunga miji yenye ugonjwa kama dsm ili kuepuka kusambaza ugonjwa mikoa yote itakuwa ngumu ku control. Mungu anatuasa kupitia zaburi kwamba tushike sana elimu wala tusimwache aende zake, tuishike elimu tukae nyumbani, tumtafute Mungu kweny nyumba vyetu vya kulala, sebuleni, prayer rooms nk kupunguza kasi ya kusambaa kwa ugonjwa. Kama serikali haitobadili mbinu zake za kupambana na Covid 19 basi, huu ugonjwa utaishi kwetu muda mrefu sana maana watu watakuwa wanaambukiza mara mbilimbili yaani unaugua unapona ukiingia mtaani unaambukizwa tena na kutakuwa na athari kubwa sana kiuchumi. Itakuwa kama Ebola huko Congo
 
Mkuu @barafu,kongole sana na Mungu Mwenyezi akubariki sana kwa "analysis" nzuri na halisi.
Kule kwenye kampuni,hili bandiko lilikuwa ndilo linatakiwa liwe mezani kwa mfadhili na limefanyiwa kazi siku nyingi,kama wapo kweli "analyst" wa namna ya barafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom