Kauli ya Pinda Bungeni haina utata kisheria?

Kauli ya Pinda Bungeni haina utata kisheria?

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,628
Reaction score
2,290
Kutokana na kauli ya Waziri Mkuu Pinda Bungeni kuwa watu wanaokaidi sheria wapigwe na Polisi je ina maana jeshi letu la Polisi hawana mbinu nyingine ya kuwadhibiti wahalifu ila kwa kuwapiga tuu? Kutokana na sheri ya Polisi hata mhalifu anapokimbia hawarusiwi kumuua ila kama hapambani na Polisi kwa silaha ila wanatakiwa kutafuta njia sahihi ili wamkamate. Sasa kama Waziri Mkuu anatamka anayekaidi sheria apigwe si ina maana hiyo ni hukumu tayari?
 
Ulevi wa madaraka na uvivu wa kufikiri, wakaidi na wahalifu wana namna ya kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Mi nadhani kila kiongoz akija na namna yake ya kutafuta suluhisho la matatizo bila kufuata sheria, madhara makubwa yatatokea na hata hiyo amani wanayohubiri itavurugika.
Wenye makosa ya kuua hawapigwi bali hushitakiwa, sembuse hao wanaoitwa wakaidi!
 
Ulevi wa madaraka na uvivu wa kufikiri, wakaidi na wahalifu wana namna ya kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Mi nadhani kila kiongoz akija na namna yake ya kutafuta suluhisho la matatizo bila kufuata sheria, madhara makubwa yatatokea na hata hiyo amani wanayohubiri itavurugika.
Wenye makosa ya kuua hawapigwi bali hushitakiwa, sembuse hao wanaoitwa wakaidi!
Sawa kabisa, mimi nikikumbuka yaliyompata Mwangosi na hii kauli ya Pinda naanza kupata jibu la kwanini Ulimboka alifanyiwa vile, kwanini Kibanda alifanyiwa vile na wengine wengi wameteswa kwa namna mbalimbali.
 
wanaojua sheria watuaambie sheria inasemaje juu ya hao watu wakaidi, mleta uzi alitakiwa kua wa kwanza kujiuliza swali hili na ikiwezekana kulipatia jibu
 
Watu wakiuwawa mpelekeni the hague kwa uchovhezi Na kutimia vibaya mamlaka.
 
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC BI HELLEN KIJO BISIMBA amesema waziri mkuu Mizengo Pinda amevunja katiba kwa kusema polisi wawapige raia. Amesema kiongozi mkubwa kama yeye si vema kutamka maneno kama hayo.

Dw.
 
Mbona wameshavunja Katiba wengi tu, Yaani sijui labda MUNGU aje mwenyewe kila siku wanaivunja Katiba tu Mungu atuteremshie neema
 
Bisimba usihofu, hiyo ndiyo style ya CCM kukata roho! Wako hoi na mahututi! Dawa zote walizokuwa nazo za udini, ukanda, ukabila na ugaidi hazifanyi kazi tena! Wako ICU wakipumulia mashine ya polisi na mahakama!! Tumaini lao la mwisho sasa ni mabomu!! Lakini dawa hii nayo haitafanya kazi. Kaburi linawasubiri kwa hamu!!!
 
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC BI HELLEN KIJO BISIMBA amesema waziri mkuu Mizengo Pinda amevunja katiba kwa kusema polisi wawapige raia. Amesema kiongozi mkubwa kama yeye si vema kutamka maneno kama hayo.

Dw.

ccm katiba hawaijue au wameisahau, nan policcm nao hivyohivyo. Chagonja anaulizwa swali kuhusu hatua watakazo mchukulia Mbowe kuhusu kukanusha kuwapa ushahidi eti anasema ' ...tutaangalia....na makachero wangu...'. Hawajue sheria hawa, na hata hizo wanazozijua wamekosea kuzitafsiri, wanazitumia tu, kwa sababu wao ndo wanaoonekana werevu sana. They are a time bomb!!
 
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC BI HELLEN KIJO BISIMBA amesema waziri mkuu Mizengo Pinda amevunja katiba kwa kusema polisi wawapige raia. Amesema kiongozi mkubwa kama yeye si vema kutamka maneno kama hayo.

Dw.
huyo ndo pinda..hana weledi wowote, cjui ni vigezo gani vilimpa u pm..
 
Hili la Pinda alipashwi kupuuziwa kwani linaweza kuigeuza nchi yetu "into a police state" Nashauri wanaharakati wote tuungane katika kulaani tamko hilo, mpaka Pinda awatake watanzania radhi,
 
Ana jazba kwani nani mtoto wake wa kumlipika kwa maneno ya kipuuzi namna ile eti Piga tu!

Watu wengine wanatakiwa wafungiwe hata visakramenti maana hawastahili kabisa. Nitawaambia maaskofu hili lijamaa hata kanisani litengwe tu. Yaani watu wanauawa halafu yeye anasema piga tu...waombolezaji wanakukera nini? Mambo ya ajabu sana
 
Sasa kama Mkulu alisema atawakata mapembe wananchi wa Mtwara hiyo kauli inatofautiana vipi na ya Pinda? Yeye amecopy tu kutoka kwa JK.Simply CCM imeoza kuanzia kichwani mpaka kwenye unyayo.
 
Sons and daughters
We're in choppy waters
With invalid motors
Squalid quarters
Leaders drunk
Steer in the funk
Talking like punks
We're sunk
Where's the paradigm?
Where's the escape?
Inna dissya time
My mouth agape
Black Makarios, with comprehension
Like Aquarius, in fifth dimension
So precarious, no condescension
The Lion got cancerous
I got cantankerous
This burn is sulfurous
Waiting gets sumptuous
They boot you with national security
Loot you down to impurities
And shoot you with no surety
Beyond cruelty
With more than a Caesarian swagger
Like a wild west character, cultured in "War Bus"
Wielding uninhibited words like deadly daggers
Prime Minister, what's with the blabbers?
Pulling antics more than Lady Gaga
What's that you are smoking? Sipping larger lager?
"Mtoto wa Mkulima", turning Agha
Epic failure, in this tragic saga



http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

Ukianza kusoma katiba tu naona kifungu kimekiukwa, nitaviorodhesha kimoja baada ya kingine.

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977
UTANGULIZI MISINGI YA KATIBA Sheria ya 1984 Na.15 ib.3


KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani:

NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na
Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu
wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote
, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na
kulindwa
, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:

....

Serikali na watu Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea Sheria ya 1984
Na.15 ib.6 Sheria Na.4 ya 1992 ib.6
9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-

(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa
unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia
mtu kumyonya mtu mwingine;
(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;
(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi
yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.

SEHEMU YA TATU HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa

Usawa mbele ya Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.

Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8 Sheria ya 2000 Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

...
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.

Haki ya Kuishi
Haki ya kuwa hai Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
14. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Haki ya Uhuru wa mtu binafsi
Sheria ya 1984 Na.15 ib.6

15.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini,kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.

Uhuru wa mtu kwenda atakako
Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri
ya Muungano.

Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria
ya 1984 Na.14 ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
 
tume ya haki za binadamu halina nguvu ata kidogo limebaki kutoa tamko tu by the way congrats bi bisimba for what you have comment.
 
Huyu mama nae kazidi kutoa matamko. Ningemuona wa maana sana kama angetuma wanasheria wa ofisi yake kwenda kuwasaidia wananchi waliokamatwa mtwara kwa kusingiziwa kufanya fujo za gesi. Hovyo kabisa Bibi Kijo
 
Back
Top Bottom