Kauli ya Pinda Bungeni haina utata kisheria?

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC BI HELLEN KIJO BISIMBA amesema waziri mkuu Mizengo Pinda amevunja katiba kwa kusema polisi wawapige raia. Amesema kiongozi mkubwa kama yeye si vema kutamka maneno kama hayo.

Dw.
Pinda alishaanza kuvunja katiba siku nyingi. Kumbuka alipotoa tamko bungeni kwamba wale wanaoua albino nao wauawe!Alipobanwa kuwa anatenda kosa la kisheria na amevunja katiba kwa kuhamaisha mauaji akatoa chozi la uongo na kweli na kuomba msamaha. Lakini sasa kwa kuwa muda umepita pengine amesahau au amepitiwa au ndo ulevi wa madaraka na unazi wa ccm ndiyo maana anatoa matamko yasiyotumia akili na hekima. Kibaya zaidi waziri mkuu Pinda ni mwanasheria! Hii ni aibu kubwa kwa kuweka profession yake ya sheria pembeni kumtumikia kafiri achilia mbali ubinadamu. Anaporuhusu polisi wapige to what extent (hadi kujeruhi au kuua?). Kwa vile ametoa amri hiyo basi angeweka na kipimo au kikomo cha kupiga. Hivi Pinda anatoa justification gani kwa watoto waliouwawa au kujeruhiwa na polisi katika mkutano wa chadema Arusha? Anaona ni sawa tu kwa vile walikuwa kwenye mkutano wa chadema siyo? km wangelikuwa kwenye mkutano wa ccm nadhani hapo ndo angekuwa na sympathy. Shame on you mr prime minister of Tanzania.
 
Na wewe mbona Post menopausal hormonal imbalances depression inakusumbua hatusemi??

Ndio lugha gani hiyo, ni Kichina? au ni wa maana sana ndio unatumia lugha za kiajabu?
 
Na wewe mtetezi wa Pinda unatakiwa kubwabwaja tu!!!! Haya pita lumumba ukachukue Buku 7 zako ujira wa siku nzima.

Anayelalamika ndio anapaswa kuja na kifungu anachodhani kimevunjwa ili mtetezi aje na utetezi wake, kushindwa kufanya hivyo ni tafsiri kuwa malalamiko hayo hayana mashiko.
 
Waandishi wa TZ ni pRo. WangEkuwa wenzetu wangemkomalia hadi angejitoa madarakani.
 
Kama yeye kapinda wenzake wajisokota kabisa!
 
Kwa kuwa umechafuka siku nyingi basi kila mtu unamuona mchafu. Hoja ya msingi ni kuwa WM amevunja Katiba ya Nchi,

HAYA BASI EMBU TUJILINGANISHE NA HUYU MAMA
Hii hapa historia yake japo kwa kifupi.

HELEN Kijo Bisimba, ni jina linalosikika ndani na nje ya Tanzania. Huyu ni mama shupavu, jasiri, mpambanaji na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, ambaye ameamua kujitoa kutoa mchango wake katika kuendeleza na kulinda ustawi wa taifa la Tanzania.
Tumezoea kusema kwamba ‘nabii hasifiki nyumbani’! Inawezekana ni hivyo kwa mama huyu, ambaye kazi anazozifanya zinaheshimika na kusifiwa kwenye ulingo wa kimataifa kuliko hapa nyumbani? Inawezekana ni kwa vile kazi anayoifanya mama huyu inaigusa serikali jichoni au kwa vile amejifunga kibwebwe kupambana na mfumo dume na kutaka kuutokomeza? Au labda ni kwa vile bado viongozi wengi kwenye ngazi ya maamuzi katika taifa letu ni wanaume?
Juzi, sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari Dk. Bisimba akisoma taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuamua kuiburuza Serikali ya Tanzania kwenye Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi.
Hiki ni kitendo cha ujasiri na kujitoa, maana ni wachache wanaoweza kuthubutu kufanya hivyo bila kuogopa matokeo yake.
Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kinachoongozwa na Bisimba, kimekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto, wanawake na watu wote wanaokandamizwa; kunyang’anywa ardhi yao na matuko mengine ya kifisadi yanayoendelea katika taifa letu. Kituo hiki kimekuwa sauti ya wanyonge.
Mama huyu amejitofautisha na baadhi ya watu wanaoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) mbalimbali katika taifa letu la Tanzania; hata kama NGO’s hizo zinakuwa ni za kutetea haki za binadamu, viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi kwa malengo ya kupata mshahara tu!
Au kwa lengo la kujenga majina yao na kujitafutia sifa. Ni tofauti kabisa na Bisimba, ambaye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekuwa sehemu ya maisha yake.
Bila unafiki na kujipendekeza, Bisimba anaonekana wazi kuguswa na kila aina yoyote ile ya ukiukwaji haki za binadamu katika taifa letu. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi, rushwa na uporwaji wa rasilimali katika taifa letu.
Ameshiriki kuipigania demokrasia na utawala bora na kilio cha katiba mpya katika taifa letu. Haogopi kusimama na kusema wazi msimamo wake na msimamo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.
Yuko tayari kusema hata yale yasiyopendeza kwenye masikio ya watawala.
Mama huyu aliyezaliwa mnamo mwaka wa 1954 mkoani wa Kilimanjaro, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinacholinda na kutetea haki za binadamu za kila Mtanzania na kuhakikisha kwamba kila raia anakingwa na aina zote za udhalilishaji.
Mapenzi ya kutetea haki za binadamu na moyo wa unaharakati yalionekana kwake kwenye miaka ya 1970 alipokuwa akisoma sekodari ya Korogwe kule Tanga.
Alifukuzwa shule kwa muda, baada ya kukataa shinikizo la walimu wake kuomba msamaha kwa barua ya kudhalilisha aliyoandikiwa mwalimu mkuu wa shule. Alikataa kuomba msamaha wa kosa ambalo yeye hakutenda.
Kwa vile alikuwa msaidizi wa kiranja wa shule alikubali kufukuzwa kuliko kuomba msamaha. Baba yake mzazi alikwenda kumwombea msamaha, lakini walimu walikataa. Hadi alipoamua baadaye kuzungumza na walimu na hatimaye kuomba msamaha kwa kosa ambalo hakulitenda mwenyewe.
Tukio hili lilimjengea moyo wa ujasiri ambao hadi leo hii zaidi ya miaka 40, amekuwa akitetea haki za wanyonge, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee.
Mama huyu, alikuwa kati ya watu wa kwanza kumshughulikia Dk. Stephen Ulimboka alipotekwa, kupigwa na kuteswa.
Kila mtu alishangaa jinsi mama huyu alivyopata habari haraka juu ya tukio hilo la kinyama na kufanya haraka kushiriki kutoa msaada kwa Dk. Ulimboka.
Alimsaidia kumfikisha hospitali na kuendelea kuishinikiza serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini watu waliofanya unyama huo.
Wakati wa mgomo wa madaktari, sauti ya Bisimba ilisikika kote kwenye vyombo vya habari. Yeye na wanaharakati wengine waliishinikiza serikali kufanya haraka kuumaliza ili kunusuru uhai wa raia wasiokuwa na hatia.
Na katika hali isiyokuwa ya kawaida mama huyu na wanaharakati wengine walikamatwa na polisi na kuhojiwa wakati walipofika Muhimbili, kutaka kujua kinachoendelea.
Mwaka 2001, alikuwa mwanamke mwanaharakati wa kwanza kupinga na kulaani mauaji yaliyotokea Zanzibar. Kitendo hicho kilimletea sifa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka 2008 alikuwa mwanamke wa kwanza kupokea tuzo ya Mwanamke Jasiri inayotolewa na Balozi wa Amerika nchini Tanzania.
Mama huyu amekuwa mstari wa mbele kupinga hukumu ya kifo. Siku ya Kupinga Hukumu ya Kifo inaangukia siku yake ya kuzaliwa ambayo ni Oktoba 10, hivyo mwaka huu anapoadhimisha miaka 58 ya kuzaliwa, ana imani kubwa kwamba iko siku adhabu hii ya kifo itakuja kufutwa nchini Tanzania.
Mama huyu ni kati ya watu wanaotamani kuona Tanzania inawaruhusu wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo, na elimu ya kujitambua inafundishwa shuleni.
Kwa maoni yake, wakati mwingine wasichana wanapachikwa mimba kwa kuwa na uelewa mdogo juu ya kujamiana; na kwamba wazazi wasione aibu kuongea na watoto wao juu ya suala la kujitambua na mahusiano, maana ukimya katika hili ni hatari zaidi kuliko faida.
Mama huyu yuko mstari wa mbele kupinga vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na vifo vya watoto wadogo. Ameunga mkono na kushiriki kampeni zote zinazoendelea za kupambana kupunguza vifo vya wajawazito.
Pia kwa kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu anaongoza kampeni ya kutokomeza ukeketaji, kuwarithi wajane na aina nyingine ya unyanyasaji kwa wanawake.
Mama huyu alianza kukiongoza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mwaka 1996, na ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hiki cha kutetea na kulinda haki za binadamu.
Ni mjane tangu mwaka 1994. Ana watoto wanne, wawili ni mainjinia, mmoja ni daktari na mwingine ni mhasibu. Lakini pia anatunza watoto yatima nyumbani kwake na ni mwanachama wa wanawake wajane katika kanisa anapoabudu.
Mbali na kuwatunza watoto yatima nyumbani kwake, yeye amekuwa sauti ya watoto wanaojilea na kujitunza.
Wakati kuna watafiti wanaopinga Tanzania kuwa na familia za watoto wanaojilea wenyewe na kujitunza, Bisimba anaamini kwamba Makete na Karagwe, alikofanyia utafiti wa tasinifu yake ya shahada ya uzamifu, kuna familia za watoto wanaojilea na kujitunza kutokana na janga la ugonjwa wa ukimwi.
Mwaka 2008 mpaka 2001, alichukua likizo ya masomo na kwenda Uingereza kuchukua shahada ya uzamifu kwenye sheria na haki za binadamu.
Tasinifu yake ulikuwa ni utafiti juu ya haki za watoto. Alitaka sauti ya watoto wa Afrika isikike, alitaka kujua jinsi watoto wanavyouelewa mfumo wa serikali. Anaamini kwamba kwa kuelewa mawazo ya watoto, serikali yoyote inaweza kutenda vizuri siku zinazokuja, maana watoto wa leo ndio viongozi wa kesho.
Kabla ya kujiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, mama huyu alikuwa mwalimu wa Kiingereza na Kiswahili katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima alikofanya kazi kwa kipindi cha miaka 10.
Marehemu mume wake ndiye aliyemshauri kusomea sheria. Wakati anajiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alikuwa bado anafundisha taasisi na kujitolea kwenye Shirika la WILDAF (Women in Law and Development in Africa) ambalo aliliwakilisha kwenye mkutano wa wanawake wa Beijing mwaka 1995.
Mama huyu ni kiongozi wa mfano. Hata wafanyakazi wenzake wanampenda na kumheshimu. Wengi amewaambukiza roho ya kutetea haki za binadamu na ujasiri wa kusimama kidete mbele ya haki.
Ukifika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, unakutana na mkurugenzi ambaye licha ya kuwa kiongozi wa kituo hicho, ni mama mwenye sifa zote za umama; kulea, kuelekeza, kujali, kutokuwa na uroho wa elimu, kuwashughulikia wengine, kuguswa na matatizo ya wengine na kuambukiza roho ya ujasiri kwa wafanyakazi wenzake.
Mama huyu pamoja na kazi kubwa alizonazo za kukiongoza kituo, bado ana nafasi ya kuihudumia familia yake, kuangalia mpira na watoto na wajukuu zake na pia kupata nafasi ya kuimba kwenye kwaya ya kanisa.
Huyo ndiye Bisimba, mwanamke shujaa, jasiri, msomi, mzalendo, mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu.

*nimebold kwa aliyetaka kufahamu kama ana mume
 
Yalipotokea mauaji Mtwara hakusikika, Arusha kama tulivyotegemea kaja na mtamko, tushajua ni mbabaishaji hafai kua mwanaharakati kwani ana upendeleo na ubaguzi.
 
Mkuu umeniwahi hawa wanaojiita Watetezi wa haki ni zaid ya wanafiq rena ni wadini kupindukia!
Mahita aliwahi kusema zaid ya aliyoyasema Pinda(TUTAWASAGASAGA TUTAWAKANYAGAKANYAGA)na kweli watu waliuliwa,wanawake walibakwa,wanaume walilawitiwa,magereza yalijaa moaka watu wengi wakakimbia ikimbizi Mombasa na kuna baadhi ta wazanzibari hadi leo hawajarudi!!!mbona hatujawasikia watetezi hawa!!!?au wa Pemba si Binaadamu!!!!?
Badili yake tukasikia Pongezi kwa Jeshi la Polisi wamefanya kazi nzuri na Mkapa akawaongeza vyeo!!!!

Muembe Chai vp mbona hatukuwasikia watetezi!!!?
au kwa sbb waliofanyiwa unyama ule ni waislamu!!!?
WANAHARAKATI WANASHERIA WA TZ NI WANAFIQ WADINI WAKUBWA!!
Polisi hawa hawa wakiuwa Znz ni sawa lkn wakiuwa Tanganyika ni kosa!!!?
Polisi hawa hawa wakipiga wakinyanyasa Wakidhalilisha Znz ni sawa lkn Wakifanya Tanganyika ni kosa!!!!?
Au nchi hi kuna Majeshi ya polisi mawili Tz!!!!?
TZ HAKUNA WANAHARAKATI KUNA VIKUNDI VYA KUTETEA UKIRISTO NA WAKIRISTO TUUUU!!!!
 
Na wewe mtetezi wa Pinda unatakiwa kubwabwaja tu!!!! Haya pita lumumba ukachukue Buku 7 zako ujira wa siku nzima.
Ukiona unakosa hoja kusimamia msimamo wako ujue msimamo wako ni dhaifu. Nilitegemea ungekuja na hoja za msingi kusimamia msimamo wako wa Mzee Pinda kuvunja katiba lakini cha ajabu umedhihirisha kuwa hata wewe hujui kama amevunja kifungu kipi cha katiba bali umebebwa na upepo ambao hujui unatoka wapi na unakwenda wapi. Subiria kasi ya huo upepo itakapokwisha ndipo utaanza kushangaa usijue ulitoka wapi na unatakiwa kwenda wapi.

Ukiona huna hoja ya msingi kuzungumzia jambo basi busara pekee ni kukaa kimya.
 
Wewe uliyeuliza pinda kwa kutoa kauli pumbavu amevunja ibara ipi umeshindwa kuweka ibara inayoruhusu kauli hiyo pumbavu unabaki unabwabwaja tu!!! Kama kungekuwepo na ibara kama hiyo basi kauli pumbavu kama hiyo ya janga la Taifa pinda zingetolewa na wengi tu waliomo ndani ya hii Serikali dhalimu. Pita kwenye ukoo wenu wa panya pale lumumba ukachukue Buku 7 zako kwa kuandika pumba.

Ukiona unakosa hoja kusimamia msimamo wako ujue msimamo wako ni dhaifu. Nilitegemea ungekuja na hoja za msingi kusimamia msimamo wako wa Mzee Pinda kuvunja katiba lakini cha ajabu umedhihirisha kuwa hata wewe hujui kama amevunja kifungu kipi cha katiba bali umebebwa na upepo ambao hujui unatoka wapi na unakwenda wapi. Subiria kasi ya huo upepo itakapokwisha ndipo utaanza kushangaa usijue ulitoka wapi na unatakiwa kwenda wapi.

Ukiona huna hoja ya msingi kuzungumzia jambo basi busara pekee ni kukaa kimya.
 
Na
wewe mtetezi wa Pinda unatakiwa kubwabwaja tu!!!! Haya pita lumumba
ukachukue Buku 7 zako ujira wa siku nzima.

Pinda hajavunja sheria yoyote! bali kawakumbusha wajibu wao muhimu kwa mujibu wa penal code cap 16 RE:2002, kuanzia sec 77, 78 na kuendelea kapitieni hapo ma mburula nyie!
 
Msaliti wa Watanzania kenge wee!!! Buku 7 tu zinakufanya uisaliti nchi yako!!! Acha kubwabwaja kama kichwani kwako kumejaa uozo wa pumba.

Another government official who opted not to be named said that the Article 13 (5) (6) and Article 8 of the Constitution provided good answers to Pinda's words.

The articles stresses on equality of all persons before the law and their entitlement to that right without any discrimination, to protection and equality. It further states that civic rights, duties and interests of every person and community should be protected and determined by courts or other state agencies established by or under the law.

Pinda hajavunja sheria yoyote! bali kawakumbusha wajibu wao muhimu kwa mujibu wa penal code cap 16 RE:2002, kuanzia sec 77, 78 na kuendelea kapitieni hapo ma mburula nyie!
 
Yalipotokea mauaji Mtwara hakusikika, Arusha kama tulivyotegemea kaja na mtamko, tushajua ni mbabaishaji hafai kua mwanaharakati kwani ana upendeleo na ubaguzi.
You are absolutely correct. This mama is discriminatory in her action. Sijampenda kwa ubaguzi wake kisha ana udini. Sio mwanahrakati wa kweli ni sehemu tu ya CDM kama alivyokuwa Ananilea Nkya. Lakini haimaanishi kwamba namsupport huyu Mizengwe Pinda ambaye alilia uwaziri mkuu mwaka 2008. Shame upon him kwa kauli zake mbaya
 
HAYA BASI EMBU TUJILINGANISHE NA HUYU MAMA
Hii hapa historia yake japo kwa kifupi.

HELEN Kijo Bisimba, ni jina linalosikika ndani na nje ya Tanzania. Huyu ni mama shupavu, jasiri, mpambanaji na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, ambaye ameamua kujitoa kutoa mchango wake katika kuendeleza na kulinda ustawi wa taifa la Tanzania.
Tumezoea kusema kwamba ‘nabii hasifiki nyumbani’! Inawezekana ni hivyo kwa mama huyu, ambaye kazi anazozifanya zinaheshimika na kusifiwa kwenye ulingo wa kimataifa kuliko hapa nyumbani? Inawezekana ni kwa vile kazi anayoifanya mama huyu inaigusa serikali jichoni au kwa vile amejifunga kibwebwe kupambana na mfumo dume na kutaka kuutokomeza? Au labda ni kwa vile bado viongozi wengi kwenye ngazi ya maamuzi katika taifa letu ni wanaume?
Juzi, sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari Dk. Bisimba akisoma taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuamua kuiburuza Serikali ya Tanzania kwenye Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi.
Hiki ni kitendo cha ujasiri na kujitoa, maana ni wachache wanaoweza kuthubutu kufanya hivyo bila kuogopa matokeo yake.
Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kinachoongozwa na Bisimba, kimekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto, wanawake na watu wote wanaokandamizwa; kunyang’anywa ardhi yao na matuko mengine ya kifisadi yanayoendelea katika taifa letu. Kituo hiki kimekuwa sauti ya wanyonge.
Mama huyu amejitofautisha na baadhi ya watu wanaoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) mbalimbali katika taifa letu la Tanzania; hata kama NGO’s hizo zinakuwa ni za kutetea haki za binadamu, viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi kwa malengo ya kupata mshahara tu!
Au kwa lengo la kujenga majina yao na kujitafutia sifa. Ni tofauti kabisa na Bisimba, ambaye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekuwa sehemu ya maisha yake.
Bila unafiki na kujipendekeza, Bisimba anaonekana wazi kuguswa na kila aina yoyote ile ya ukiukwaji haki za binadamu katika taifa letu. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi, rushwa na uporwaji wa rasilimali katika taifa letu.
Ameshiriki kuipigania demokrasia na utawala bora na kilio cha katiba mpya katika taifa letu. Haogopi kusimama na kusema wazi msimamo wake na msimamo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.
Yuko tayari kusema hata yale yasiyopendeza kwenye masikio ya watawala.
Mama huyu aliyezaliwa mnamo mwaka wa 1954 mkoani wa Kilimanjaro, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinacholinda na kutetea haki za binadamu za kila Mtanzania na kuhakikisha kwamba kila raia anakingwa na aina zote za udhalilishaji.
Mapenzi ya kutetea haki za binadamu na moyo wa unaharakati yalionekana kwake kwenye miaka ya 1970 alipokuwa akisoma sekodari ya Korogwe kule Tanga.
Alifukuzwa shule kwa muda, baada ya kukataa shinikizo la walimu wake kuomba msamaha kwa barua ya kudhalilisha aliyoandikiwa mwalimu mkuu wa shule. Alikataa kuomba msamaha wa kosa ambalo yeye hakutenda.
Kwa vile alikuwa msaidizi wa kiranja wa shule alikubali kufukuzwa kuliko kuomba msamaha. Baba yake mzazi alikwenda kumwombea msamaha, lakini walimu walikataa. Hadi alipoamua baadaye kuzungumza na walimu na hatimaye kuomba msamaha kwa kosa ambalo hakulitenda mwenyewe.
Tukio hili lilimjengea moyo wa ujasiri ambao hadi leo hii zaidi ya miaka 40, amekuwa akitetea haki za wanyonge, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee.
Mama huyu, alikuwa kati ya watu wa kwanza kumshughulikia Dk. Stephen Ulimboka alipotekwa, kupigwa na kuteswa.
Kila mtu alishangaa jinsi mama huyu alivyopata habari haraka juu ya tukio hilo la kinyama na kufanya haraka kushiriki kutoa msaada kwa Dk. Ulimboka.
Alimsaidia kumfikisha hospitali na kuendelea kuishinikiza serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini watu waliofanya unyama huo.
Wakati wa mgomo wa madaktari, sauti ya Bisimba ilisikika kote kwenye vyombo vya habari. Yeye na wanaharakati wengine waliishinikiza serikali kufanya haraka kuumaliza ili kunusuru uhai wa raia wasiokuwa na hatia.
Na katika hali isiyokuwa ya kawaida mama huyu na wanaharakati wengine walikamatwa na polisi na kuhojiwa wakati walipofika Muhimbili, kutaka kujua kinachoendelea.
Mwaka 2001, alikuwa mwanamke mwanaharakati wa kwanza kupinga na kulaani mauaji yaliyotokea Zanzibar. Kitendo hicho kilimletea sifa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka 2008 alikuwa mwanamke wa kwanza kupokea tuzo ya Mwanamke Jasiri inayotolewa na Balozi wa Amerika nchini Tanzania.
Mama huyu amekuwa mstari wa mbele kupinga hukumu ya kifo. Siku ya Kupinga Hukumu ya Kifo inaangukia siku yake ya kuzaliwa ambayo ni Oktoba 10, hivyo mwaka huu anapoadhimisha miaka 58 ya kuzaliwa, ana imani kubwa kwamba iko siku adhabu hii ya kifo itakuja kufutwa nchini Tanzania.
Mama huyu ni kati ya watu wanaotamani kuona Tanzania inawaruhusu wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo, na elimu ya kujitambua inafundishwa shuleni.
Kwa maoni yake, wakati mwingine wasichana wanapachikwa mimba kwa kuwa na uelewa mdogo juu ya kujamiana; na kwamba wazazi wasione aibu kuongea na watoto wao juu ya suala la kujitambua na mahusiano, maana ukimya katika hili ni hatari zaidi kuliko faida.
Mama huyu yuko mstari wa mbele kupinga vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na vifo vya watoto wadogo. Ameunga mkono na kushiriki kampeni zote zinazoendelea za kupambana kupunguza vifo vya wajawazito.
Pia kwa kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu anaongoza kampeni ya kutokomeza ukeketaji, kuwarithi wajane na aina nyingine ya unyanyasaji kwa wanawake.
Mama huyu alianza kukiongoza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mwaka 1996, na ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hiki cha kutetea na kulinda haki za binadamu.
Ni mjane tangu mwaka 1994. Ana watoto wanne, wawili ni mainjinia, mmoja ni daktari na mwingine ni mhasibu. Lakini pia anatunza watoto yatima nyumbani kwake na ni mwanachama wa wanawake wajane katika kanisa anapoabudu.
Mbali na kuwatunza watoto yatima nyumbani kwake, yeye amekuwa sauti ya watoto wanaojilea na kujitunza.
Wakati kuna watafiti wanaopinga Tanzania kuwa na familia za watoto wanaojilea wenyewe na kujitunza, Bisimba anaamini kwamba Makete na Karagwe, alikofanyia utafiti wa tasinifu yake ya shahada ya uzamifu, kuna familia za watoto wanaojilea na kujitunza kutokana na janga la ugonjwa wa ukimwi.
Mwaka 2008 mpaka 2001, alichukua likizo ya masomo na kwenda Uingereza kuchukua shahada ya uzamifu kwenye sheria na haki za binadamu.
Tasinifu yake ulikuwa ni utafiti juu ya haki za watoto. Alitaka sauti ya watoto wa Afrika isikike, alitaka kujua jinsi watoto wanavyouelewa mfumo wa serikali. Anaamini kwamba kwa kuelewa mawazo ya watoto, serikali yoyote inaweza kutenda vizuri siku zinazokuja, maana watoto wa leo ndio viongozi wa kesho.
Kabla ya kujiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, mama huyu alikuwa mwalimu wa Kiingereza na Kiswahili katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima alikofanya kazi kwa kipindi cha miaka 10.
Marehemu mume wake ndiye aliyemshauri kusomea sheria. Wakati anajiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alikuwa bado anafundisha taasisi na kujitolea kwenye Shirika la WILDAF (Women in Law and Development in Africa) ambalo aliliwakilisha kwenye mkutano wa wanawake wa Beijing mwaka 1995.
Mama huyu ni kiongozi wa mfano. Hata wafanyakazi wenzake wanampenda na kumheshimu. Wengi amewaambukiza roho ya kutetea haki za binadamu na ujasiri wa kusimama kidete mbele ya haki.
Ukifika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, unakutana na mkurugenzi ambaye licha ya kuwa kiongozi wa kituo hicho, ni mama mwenye sifa zote za umama; kulea, kuelekeza, kujali, kutokuwa na uroho wa elimu, kuwashughulikia wengine, kuguswa na matatizo ya wengine na kuambukiza roho ya ujasiri kwa wafanyakazi wenzake.
Mama huyu pamoja na kazi kubwa alizonazo za kukiongoza kituo, bado ana nafasi ya kuihudumia familia yake, kuangalia mpira na watoto na wajukuu zake na pia kupata nafasi ya kuimba kwenye kwaya ya kanisa.
Huyo ndiye Bisimba, mwanamke shujaa, jasiri, msomi, mzalendo, mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu.

*nimebold kwa aliyetaka kufahamu kama ana mume

Mungu abariki kazi ya mikono yako mama. Mungu mume wa wajane alikujua tangu mwanzo na kwakua umeshiriki mateso ya msalaba usipozimia moyo utavikwa taji katika ufalme ule uutazamiao.

Ninajivunia kuwa na mama wa jinsi yako hapa nchini!
 
Wako wapi wanawake wa jinsi ya mama Helen Kijo Bisimba? Wengi wa waliopo ni wale wenye kunyemelea viti vya dezo kupitia mfumo dume na kuudumisha huku wakikandamiza maelfu ya akina mama masikini wanaokufa kila dakika kwakukosa huduma huku wao wakipiga makofi ya ndiyo Bungeni kupitisha hoja za wanyonyaji wa mfumo dume wenye kutoa kipaumbele cha kutembelea VX huku mahospitali yakiwa hayana dawa wala vitanda vya kutosha. Na wanapokosolewa wanaita huko kukosolewa vurugu wakiitumia dola kwa faida yao binafsi kuulinda mfumo dhalili dume!

Mumekataluwa duniani na mbinguni enyi kizazi cha nyoka na tazama mauti i milangoni mwenu kuwameza!
 
Back
Top Bottom