Kauli ya Mwisho ya Mwalimu kuhusu Mzee Mtei pale nyumbani kwake Msasani..

zaidi ya kumfaham ka mwasisi wa cdm sina info zozote za mzee wetu mtei!mwenye historia,cv zake na mikasa na info zake zaid atujuze tafadhali kwa manufaa ya 2siomfaham kiundan!

Mkuu nenda duka la vitabu ulizia kitabu alichoandika mzee Mtei kuhusu maisha yake. Utakuta kila kitu hapo.
 
Wakuu sisi wengine tupo kwenye game siku nyingi. Nakumbuka kuna siku baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba CHADEMA ndicho chama cheenye SERA zinazoeleweka. Kama.mmesahau au mlikuwa bado wachanga basi fuatilieni.

Ni kweli kabisa, baada ya kusoma katiba ya chadema alikisifia na kubaki na katiba ile.
 
zaidi ya kumfaham ka mwasisi wa cdm sina info zozote za mzee wetu mtei!mwenye historia,cv zake na mikasa na info zake zaid atujuze tafadhali kwa manufaa ya 2siomfaham kiundan!
Alikuwa Gavana wa kwanza Mtanzania mweusi..badaye akaja kuwa waziri wa fedha mpaka 1984 alipojiuzulu baada ya kotofatiana na Mwl. kuhusu TZ kuwa member wa IMF & wolrd bank.
Kwa ufupi ndio nimjuavyo..wanaomjua zaidi wanaweza kukupa full CV.
 
Tatizo ni kwamba kuna watu siku zote hawapendi mabadiliko hasa kama wanafaidika na hali iliyopo kwa namna moja ama nyingine. lkn ukweli ni kwamba mabadiloko hayazuiliki. CCm ni nani mpaka iongoze milele. Time for positive change has come. Others have done it, why not us??? CCM sio Tanzania, ni chama tu. Hata mwl. Nyerere alijua hilo ndo maana alisema CCM sio mama yake wala baba yake akimaanisha 'huwezi kubadilisha wazazi lkn chama kinakuja na kupita. Parties will come and go but Tanzania is there to stay!!!!
 
japo mwalimu Nyerere alitutendea mengi mazuri,si kila kitu sasa awe ndio wa kumrejea,yatupasa kuchukuwa yale mazuri tu tena yawe modified kulingana na wakati huu

Kweli kabisa yeye mwenyewe alisema anatushangaa, tunaacha mazuri, tunachukua mabaya.
 
Wakuu sisi wengine tupo kwenye game siku nyingi. Nakumbuka kuna siku baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba CHADEMA ndicho chama cheenye SERA zinazoeleweka. Kama.mmesahau au mlikuwa bado wachanga basi fuatilieni.
Hii inawezekana wengi wakawa hawana kumbukumbu ya haya maneno japo mimi mwenyewe sikumbuki aliyasema wapi. Lakini alisema enzi hizo wakati cdm sio wala chama tishio kama ilivyo leo.
 
Naona Wooote mmechangia kadri mlivyoilewa post hii,Ila kama upo DSM siku moja moja jitahidi upite Pale Msasani kwa Mama yetu,Mama Maria Nyerere umuombe japo dakika kumi akuelezee kuhusu hii kauli...

Kila la Kheri......
Sasa mimi niko Urusi mama Nyerere ntamwonea wapi?

Wewe tueleze "nia ya Mtei" aliyoizungumzia mwalimu ni ipi?

Maana unajuwa ukisema ni urais utaonekana mrongo.
 
alianzia kazi Kenya baada ya kutoka Makerere, ameoa mtoto wa ndugu wa Mtemi Mareale akawa Gavana wa kwanza, akawa Katibu Mkuu wa Jumuia ya A. Mashariki (E.A.C.) mpaka ilivyovunjika akaenda huko USA navyofahamu sasa ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kahawa TZ haya katika Siasa ndio mwanzilishi wa CDM
 
Hatubezi kauli za mwalimu,naye pia ni binadamu ana mapungufu yake kinachotokea katika CCM aliyoipenda ni unafiki ndo maana wamechukua yale mabaya yaliyofanya na mwalimu ambayo hata mwalimu ana yakiri na kuacha yale mazuri.Mwalimu hakupenda rushwa,hakupenda ubinafsi,hakupenda ukabila lakini leo CCM yake ina thubutu kusema rais wa 2015 kamwe hawezi toka KASkazini wapi tuna kwenda.Mwalimu aliwahi kukataa kumnadi mwana CCM mwenzake kwa kukosa sifa za kuwa kiongozi kutokana na tuthuma alizokuwa ana tuhumiwa wakati wa uchaguzi wa vyama vingi 1995,nani leo anaweza.Mwenyekiti anashiriki kupitisha jina la mgombea aliye washinda wenzake kwa kutoa rushwa,una tegemea serikali itapinga ufisadi!Mwalimu hakuwa mnafiki aliweka mambo wazi leo kuna nani kama mwalimu ndani ya CCM?
 
Sasa mimi niko Urusi mama Nyerere ntamwonea wapi?

Wewe tueleze "nia ya Mtei" aliyoizungumzia mwalimu ni ipi?

Maana unajuwa ukisema ni urais utaonekana mrongo.

Mkuu jmushi heshima Mbele

Yaani Ma-Great Thinkers wanaleta habari zisizo na kichwa wala miguu, wanaleta habari kana kwamba watu wako chumbani wanaongea, thread kama hizi hazina tija kabisa, unasoma mpaka page ya nne hakuna unachoelewa, ni mafumbo mafumbo tu kama watoto wa kike

unamuuliza mtu anakujibu nenda kwa Mama Maria, ni ujinga kabisa, humu ndani kuna member wangapi? kwa hiyo wote waende kwa Mama Maria kuuliza kitu ambacho mtoa Hoja anakijua?

Tupo humu kujifunza, kuelimika, kupata ustaharabu, kukosolewa, lakini kwa thread kama hii tunajifunza umbea wa kikekike tu
 
Hii kauli ya kila la heri
Ina maanisha nini kwa mtazamo wako?
Inawezekana mi sijakuelewa, ebu tulia uelezee acha kukimbiakimbia.
 
Nyerere alimshanggaa Mtei kwa uroho wake wa madaraka na si alitoa baraka kwao
 
Mwalimu pia aliwashangaa sana watu wa Arusha wakipomchagua mwanae Makongoro wakati huo yuko NCCR kuwa mbunge wao na kumuacha Mtei wa Chadema!!
 
Ya nyerere yametimia kwani hakuna mtz anaeipenda ccm iliyodanganya watz vizazi na vizazi.
 
japo mwalimu Nyerere alitutendea mengi mazuri,si kila kitu sasa awe ndio wa kumrejea,yatupasa kuchukuwa yale mazuri tu tena yawe modified kulingana na wakati huu.sasa kama alisem hivyo kuna shida gani?laiti angelikuwepo leo na kuona kazi inayo fanywa na CHADEMA angelikuwa wa kwanza kumpongeza Mzee Mtei.

kila la kheri maana yake alimtakia mema na si kwamba alipinga. Jamani hata kiswahili kinatuchanganya kiasi hicho kweli?
 
kuhusu kauli ya Mwl Nyerere ambayo naweza kukumbuka kuhusu upinzani nakumbuka tu pale aliposema kwamba CCM itaangushwa na wana ccm wenyewe akiwa na maana makundi ndani ya chama hicho ndiyo chanzo cha ufa na ndio tunayoyaona hv sasa na ndio hayo yaliyokifanya kushindwa Arumeru na ndio hayo hayo yatafanya kushindwa kwa Chama hicho mwaka 2015.
 
556963_203851959717193_100002771708114_247011_356469526_n.jpg
 
Mwlimu Nyerere aliwahi kumpigia kura ya Ndiyo balozi Paul Ndobho wa CHADEMA akiwania ubunge Musoma mjini 1995 kwa hiyo alikikubali.

mkuu, p ndobho alikuwa anagombea kwa tikiti ya nccr mageuzi sio cdm kipindi kile.
 
zaidi ya kumfaham ka mwasisi wa cdm sina info zozote za mzee wetu mtei!mwenye historia,cv zake na mikasa na info zake zaid atujuze tafadhali kwa manufaa ya 2siomfaham kiundan!

Nenda bookshop pale Mlimani City tafuta kitabu kinachoitwa From Goatherd to Governer by Edwin Mtei, Ni kizuri sana kwa kweli, kinauzwa sh elfu 15,000 tuu!
Nimejifunza mengi sana kuhusi hiko kitabu, enzi zao walikuwa ni miaka 25 tuu ndio waliochukua top position za govenment, Ilikuwa governer akiwa na miaka 32 tuu. Kitabu ni kuzuri sana
 
Mwlimu Nyerere aliwahi kumpigia kura ya Ndiyo balozi Paul Ndobho wa CHADEMA akiwania ubunge Musoma mjini 1995 kwa hiyo alikikubali.

Jamani tusipotoshe historia. Balozi Paul Ndobho hakuwahi kuwa Mwanachama wa Chadema. Alishinda kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi Musoma Vijijini 1995 na aliisharudi CCM miaka mingi sasa.Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Mjini ni Marehemu Dr. Emmanuel Changalawe Magoti (Nyongeza tu ni kuwa Jimbo la Musoma Mjini halina historia ya wabunge kukaa zaidi ya miaka 5, aliyeweza ni Marehemu Abel Kyagunya Mwanga -angalau vipindi vitatu lakini Magoti,Wakanga Marwa na Mathayo Manyinyi ni only five years each)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom