Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Kimsingi chama cha siasa kinaweza kuwa yakinifu kwa kuamini moyoni na kutekeleza sera zake kwa vitendo. Nyerere alishaona mambo mengi yaliyomo katika miongozo ya CCM hazitekelezeki na imeshatupwa, hasa kule zenji. Kwa mtazamo wa kitabu cha animal farm, falsafa hizo za kirusi zilitabiriwa kushindwa na ikawa hivyo. Siasa za Mrango wa kati ndio ambazo zinalengwa na wote, wale waliokuwa WA-cummunist na Mabepari. Mtei alijua hayo mapema sana, ndio maana alikuwa anakwaruzana na Mwalimu hasa katika mambo ya uchumi. Laiti mwalimu angemsikilize kwa makini Mzee Mtei (Genius economist) basi tungekuwa mbali. Kwa sisi tunaomfahamu Mzee mtei na historia yake, si ajabu kwa mwalimu kuona kwamba CDM itaja chukua nchi. Kwa kweli falsafa ya chadema imeandikwa ikaandikika.