Kauli ya Mufti juu ya katiba mpya

Kauli ya Mufti juu ya katiba mpya

Hilo ndio Tamko la Bakwata kwa Waislam, waislam watamfuata maana wengi wanaipenda Bakwata isipokuwa imani kali wachache ndio wanaichukia Bakwata

Siyo kweli waislamu wengi wanaipenda BAKWATA. Wasomi wa kiislamu hawaitaki...wenyewe hawafuati
Katiba yao.....na kuna ufisadi kibao.Hawafuati sheria za serikali..ukiiba Bakwata hupelekwi mahakamani wala hukatwi mkono..unaachishwa kazi tu.
 
Pengo na mufti simba wanamanufaa makubwa na mafisad huwa wanawagawia mshiko,wakina vijisent wakipiga mzigo huwa wanawakatia ganji kusikia,hivyo lazima watetee ulaji bila kujali mali ya nch inatafunwa na mafisadi/pengo na simba hao yao ni jehanamu tu inawasubili
 
Kijana usihukumu kama unaushaidi na hao watumishi wa Mungu wasije wakukupa rahana bure
 
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.

Kwa sababu wameongea yale yanayoipendeza ccm?
 
Ile picha ya Mufti akiwa anapokea fedha kutoka kwa Lowassa iko wapi?
 
chief72

Tamko zuri kwetu waislamu...serikali ilituahidi mahakama ya kadhi itakuwepo ktk katiba lakini kwa katiba hii pendekezwa haipo...kwahiyo mimi naomba waislamu wote wa Tanzania bila kubaguana, tuipigie kura ya HAPANA hii katiba...! Nawasilisha...
 
Last edited by a moderator:
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.

Unasemaje kuhusu upeo wa viongozi wa chama (CCM) wanaosema tuipigie kura ya ndio ina maana wao hawana upeo?
 
Mbona huyu nae amechelewa, inakuwa kama ndio anaamka toka usingizini. Mambo ya katiba mpya yameahirishwa ndio anajitokeza leo. Sasa hayo anamwambia nani? _manina!!

Kusoma kwenyewe hajui atajulia wapi mambo haya..mufti mpiga ramli ..
 
....siwaambii waisilamu na wasio kuwa waisilamu wakapigie Ndio au Hapana ila kila mtu akatumie akili yake mwenyewe kwa kuona ina mfaa au hai mfai, hapo ndipo aamue mwenyewe kupiga Ndio au Hapana.

Kwa upande wangu sioni kama kauli ya Mufti inaweza fananishwa na kauli ya Kardinali Pengo. Sikukiona kipindi hicho na ninaamini kilichoandikwa hapa ni nukuu ya alichokisema hivyo ameonesha mfano wa kile ambacho viongozi wa nchi yetu walipaswa kukisema hapo mwanzo. Hivi, kama mkuu wa nchi na wakubwa wengine wangetumia kauli hiyo ya "kila mtu akatumie akili yake...hapo ndipo aamue mwenyewe..." badala ya ile kauli ya "katiba pendekezwa ni nzuri, ina mambo mengi, brah brah brah, ipigieni kura ya NDIYO" ni nani mwenye akili timamu angeanzisha kampeni ya kura ya HAPANA???

Kampeni zilianza mapema kwa wakubwa wetu hawa kudhani hakuna wa HAPANA kitu ambacho kingeifanya jamii yetu kuwa ya wendawazimu kwa wote kusema NDIYO. Kardinali Pengo ajifunze kwa Sheikh Mkuu kwani kauli zake zililalia upande wa kuwalaumu wanao hamasisha kura ya HAPANA na kuwasahau wale wanaohamasihsa NDIYO. Kama kosa lilifanyika wakati wa kukabidhiwa katiba pendekezwa kwa viongozi wetu wakubwa wa nchi basi tuendelee hivyo mpaka mwisho. Kwanini tusijifunze kwa wenzetu SCOTLAND waliokuwa na the YES and the NO VOTE na mambo yakaenda kulingana na kile wananchi walichokiona??

Sisi kila kitu ni kuagizwa tufanye na mnasahau kuwa tunauwezo wa kufanya maamuzi kikubwa, TUACHIENI MUDA TUIELEWE KATIBA HIYO PENDEKEZWA. Mmelalia kwenye hizo pande mbili na mnasahau kuwa wapo AMBAO HAWATAPIGA KWANI HAWATAIELEWA NA HATA WAKIIELEWA WANAWEZA WAKASEMA LIWALO NA LIWE...
 
Tamko zuri kwetu waislamu...serikali ilituahidi mahakama ya kadhi itakuwepo ktk katiba lakini kwa katiba hii pendekezwa haipo...kwahiyo mimi naomba waislamu wote wa Tanzania bila kubaguana, tuipigie kura ya HAPANA hii katiba...! Nawasilisha...

Kwa hiyo Katiba ya sasa ina hiyo Mahakama ya Kupiga watu mawe?
 
Hiyo katiba wanayotakiwa kuisoma iko wapi?maana kila kata wanapeleka nakala 3000,sasa je kata moja ina watu 3000 tu?si kila mtu atapata hii katiba pendekezwa

Mkuu mimi sijaona nakala 3000 katika kata yetu.
 
chief72

Naomba kwa nia nzuri tu, Mheshimiwa Mufti CV yake ikoje?
 
Last edited by a moderator:
Kwi kwi kwi kwi lol! wewe bado kweli! Wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia ni wale ambao hawawaambii waumini wao namna ya kupiga kura ila wale wanaowaambia waumini wao wapike kura ya HAPANA kwako wewe wana upeo na akili finyu!!!! Na MACCM nao wanaopigia debe kura ya NDIYO badala ya kuacha Watanzania tupige kura ile ambayo tunaona itafaa nao wana upeo na akili finyu?

Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.
 
Ngoja Gwajima apone aje kumpa vipande vyake....lazima sasa hivi Gwajima itakuwa hamuheshimu tena huyo mufti

#Zitto
 
Ngoja Gwajima apone aje kumpa vipande vyake....lazima sasa hivi Gwajima itakuwa hamuheshimu tena huyo mufti

#Zitto

Mufti nae alikuwepo kwenye kikao cha maasikofu, au alipewa waraka juu ya maazimio ya maasikofu, akakubaliana nao na kusaini?
 
Hilo ndio Tamko la Bakwata kwa Waislam, waislam watamfuata maana wengi wanaipenda Bakwata isipokuwa imani kali wachache ndio wanaichukia Bakwata

Sioni tatizo na bakwata, hata August HIJA waislam wote huwangukia, hao ndo waislam wengine wana roho za kigaidi.
 
Back
Top Bottom