Kauli ya Mnyika, Inakatisha tamaa...

Kauli ya Mnyika, Inakatisha tamaa...

Rabboni

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
1,193
Reaction score
1,731
John Mnyika, Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema jana alitoa kauli ambayo kidogo ilitufanya wachache tufikirie tofauti na dhamira kuu ya UKAWA kuwaondoa CCM.

Mnyika alisema, wananchi wa Ubungo na Kibamba wafikirie juu ya uwepo wake na Kubenea ndani ya bunge utakavyoitikisa serikali...
Kwa kauli hii inamaanisha kuwa Mnyika haamini kama Ukawa watachukua nchi!!
Au alimaanisha wataitikisa serikali yao wenyewe watakaoiunda?

It means hawaamini kama Serikali ya CCM itatoka madarakani, wakati sisi wananchi wa kawaida tushaliona anguko kubwa la Chama cha Mapinduzi.
 
sasa cha ajabu ni nini mimi naona amemanisha wote majembe na tunataka watu kama hao bungeni
 
Yaweza kuwa hukuelewa au huelewi kazi za mbunge. Kazi kubwa ya mbunge ni kuisimamia serikali....Hata kama ni serikali ya chama chako lazima isimamiwe. Kwa hali hiyo wakiingia bungeni wataisimamia vizuri serikali yao chini ya CDM kwa mwamvuli wa UKAWA hivyo kuleta ufanisi
 
Yaweza kuwa hukuelewa au huelewi kazi za mbunge. Kazi kubwa ya mbunge ni kuisimamia serikali....Hata kama ni serikali ya chama chako lazima isimamiwe. Kwa hali hiyo wakiingia bungeni wataisimamia vizuri serikali yao chini ya CDM kwa mwamvuli wa UKAWA hivyo kuleta ufanisi

Yaap, ndo hivyo
 
Pole sana jamaa yangu, na wewe ni miongoni mwa wengi walio athirika na mfumo mbovu wa utawala wa CCM. Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali iliyopo madarakani na kutunga sheria. Lakini kwa miaka yote ya utawala mbovu wa CCM, kazi ya bunge (ukiondoa wapinzani) imekua ni kuitetea serikali na kukandamiza wananchi kwa kupitishia sheria mbovu na kandamizi kwa Taifa.
 
Mihimili itabaki separate bila kujali ni serikali ya nani. Yeye kama mbunge ataisimamia serikali ya Ukawa bila kupepesa macho.
 
Tatizo watu walishalemazwa na mfumo wa CCM. Wanadhani muhimili wa bunge ni kutetea chama chao. Bunge ni Bunge na Serikali ni serikali, Bunge linatakiwa kuisimamia serikali. Labda kama wakiteuliwa kuwa mawaziri.

kitufe cha like kimepotea, anyway chukua tano
 
Back
Top Bottom