iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Kila mara mkuu anapopata fursa ya kuhutubia,na Kaimu Jaji Mkuu akawa eneo hilo, basi utasikia "Kaimu Jaji Mkuu tunaomba utusaidie.
Hii hunifanya nitafakari sana,anataka msaada gani? Kesi huwa na pande mbili Jamhuri(serikali)dhidi ya mtuhumiwa,na kazi ya mahakama ni kutenda haki kwa pande zote mbili,kwa nini upande mmoja unaomba msaada tena hadharani? Ni msaada gani? Wa kupendelewa ili mtuhumiwa afungwe?
Ni vizuri anayeomba msaada aweke wazi,lengo la kuomba msaada ni nini,kama lengo ni kuharakisha nashauri yaishe,aseme,kama lengo ni kupata upendeleo,pia aseme.
Je, watuhumiwa pia wana fursa ya kuomba msaada wa Kaimu Jaji Mkuu?
Kuna zile kesi za kodi,aliyekuwa Jaji Mkuu pia " aliombwa msaada" na akapewa ka ahadi.
Kwa mustakabali wa haki sawa,mkuu ajiepushe "kuomba msaada kwa Kaimu Jaji Mkuu"
Mkuu ajielekeze kuiambia mahakama itende haki kwa wakati,na yasiwepo maombi ya "msaada". Hii itafanya wale wanaofungwa wahisi walifungwa kwa kuwa mahakama ilisikiliza " ombi la msaada" kutoka kwa mkuu