Halafu hii tabia ya kuanza kumuwekea mshindani wako vizingiti mlangoni ili asiingie ulingoni mpambane kwa maoni yangu ni woga uliopitiliza, hasa ikizingatiwa kwamba wewe mwenyewe unajinasibu kwamba umefanya mengi na makubwa. Ningekuwa na uwezo sheria au vikwazo vinavyowekwa ili kum disqualify mgombea vingefutiliwa mbali, hata kama amekosea kujaza fomu aitwe na aelekezwe, ili mwisho wa siku wagombea wakutane uso kwa uso mwenyewe na wapiga kura wao. Pia kwenye kupigiwa kura kwenye masanduku ya kura nyuma yake iwekwe picha ya anayeomba kuchaguliwa na masanduku yapangwe mstari ili kila mpiga kura aende moja kwa moja kwenye mstari wa boksi analomtaka kumpigia kura na iwe live au waandishi waruhusiwe kuchukua matukio moja kwa moja, kama ilivyokuwa uchaguzi wa wajumbe wa CCM.
Unataka aaibike😁 hilo swala hataki sikia kabisa