Kauli ya Mbowe: UKAWA kutoka bungeni

Kauli ya Mbowe: UKAWA kutoka bungeni

na huu mkakati wa serikali tatu unaelekea una ufadhili mrefu sana na ndani na nje kiasi cha jamaa hawataki kusikiliza wenzao kwa hoja bali kwa nguvu na wakizidiwa wanatoka nje.

Hapana, nadhani viongozi wa nchi hii hawna akili wala aibu. Wanafikiri hii nchi ni mali yao na sisi ni mifugo yao!
 
Baada ya kusaini posho ndiyo ukawa wakatoka.kumbukeni posho ni zaidi ya taifa kajengeni hoja acheni uoga au rudisheni posho
 
Aisee hawa jamaaa hatuwaelewi kabisa kila kukicha wanakuja na sababu zao mara hili mara lile sasa sisi wananchi tuwaeleweje?
Walisema kama hati haitaretwa wanalisusia bunge imeletwa, kama hawatapitisha aina ya kura wanazotaka wanasusia bunge zikapitishwa,
Kama hawatamtoa prof Lipumba kwenye uenyekiti wanajitoa wakamtoa,
Kama hawatapewa muda wa kufafanua hoja za wachache bungeni wajitoa wakapewa muda.
Binafsi sisi wananchi tulikuwa tunajua tatizo ni hati imeletwa na wameona wameumbuka wameamua kujitoa bila sababu za msingi tena wakiwa wamekwisha chukua mamilion ya watanzania.
Jamani mnatuchanganya sana sasa tunakosa imani na nyie ndugu zetu
 
Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi. Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .
o
Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya
kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali hii ?

Hata sielewi mnazungumzia nini . Hivi katiba inanisaidia nini mimi mlalahoi. Hii iliopo ni kama haipo hiyo ijayo ya nini sisi tungebaki bila katiba. Kama ni kitabu cha kutuongoza mbona wachache wako juu yake? Wengi tunaumia. Wanaishi kama wako peponi wanafanya makosa jela hawaendi tunakwenda sisi wenzangu na mie. Hakuna haja ya kuwa na kati Iba jamani?
 
Inaonekana huu Muundo wa serikali 2 ulifanyiwa zindiko kubwa sana. Kwanini unang'ang'aniwa namna hii ni kama vile ni Biblia au kurani ambazo haziwezi kubadilishwa kabisa?
Mkuu, zindiko ni MSLAHI binafsi tu hapa. Walahi hata mfumo wa vyama vingi usingerejeshwa kama baba wa taifa angekuwa katangulia mbele ya haki!!!!!!!!!!!
 
Aisee hawa jamaaa hatuwaelewi kabisa kila kukicha wanakuja na sababu zao mara hili mara lile sasa sisi wananchi tuwaeleweje?
Walisema kama hati haitaretwa wanalisusia bunge imeletwa, kama hawatapitisha aina ya kura wanazotaka wanasusia bunge zikapitishwa,
Kama hawatamtoa prof Lipumba kwenye uenyekiti wanajitoa wakamtoa,
Kama hawatapewa muda wa kufafanua hoja za wachache bungeni wajitoa wakapewa muda.
Binafsi sisi wananchi tulikuwa tunajua tatizo ni hati imeletwa na wameona wameumbuka wameamua kujitoa bila sababu za msingi tena wakiwa wamekwisha chukua mamilion ya watanzania.
Jamani mnatuchanganya sana sasa tunakosa imani na nyie ndugu zetu

we nawe kilaza kweli una acha kukosa imani na ccm walio kunyonya mpka utumbo na sasa wana enda kuharibu mchakato wa katiba.
 
Mbowe hana hoja atafute sababu zingine za kusingizia kwanza matusi alianza Lisu baadaye jusa mbowe naye akaja kutukana matusi kibao sasa nini anachoongea bora akae kimywa kwanza yeye ndiye anaongoza pia kwa ubaguzi rejea walivyombagua zitto.
Mbowe, Lisu na Jusa walitoa matusi gani mkuu?
 
Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.

Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali h

Mbowe anaweza kuwa sahihi kwa tafsiri yake juu ya kauli ya Lukuvi, lakini Mbowe huyu huyu amesahau kwamba yeye na katibu wake Dr Slaa waliwahi kutamka kwamba inchi hii haitatawalika???? maneno haya yanatafsiri gani kwake ?
 
Mbowe, Lisu na Jusa walitoa matusi gani mkuu?

Jusa alimwambia mjumbe mwenzie Ndugu Mpanju alipoomba mwongozo wa spika juu ya kauli ya Jusa, yeye akamjibu kwa kusema kwanza hoja yake naipuuza na yeye mwenyewe nampuuza, ukichukulia kwamba Ndugu Mpanju yeye ni mlemavu ina maana lugha ya Jusa ilikuwa ni ya kumtusi mjumbe mwenzie.
 
Eti leo CCm wanadai kuwa serikali tatu ni mzigo kwa wananchi, leo ndio wanamfikiria huyu mwananchi wakati muda wote wanamdhoofisha na sera mbovu za kiuchumi, miundominu,afya, elimu na mengineyo. Hiyo huruma ya CCM inatoka wapi? Wazandiki, mafisadi na wahuni wakubwa wanaoendelea kuliibia taifa letu na wananchi wake kwa kuwadanganya eti kuendelea kudumisha amani iliyopo. Amani ipi iliyoko Tanzania? muda wenu umeisha nyie CCM na soon u will realize.

Ni kweli inchi ina matatizo mengi ya kiuchumi, ajira na mengineyo lakini sidhani kama matatizo hayo yote yamesababishwa na muundo wa serikali 2 kwani zipo inchi nyingi tu katika bara letu la Afrika ambazo zenyewe hazina muungano wowote lakini bado zina matatizo yanayofanana na ya kwetu.

Sasa hivi ni kweli kabisa mamtizo waliyonayo wananchi huku Katavi mpanda, Sumbawanga ni idadi ya serikali? matatizo yao ya maji, barabara, kilimo kisicho na tija soluhisho lake ni idadi ya serikali kuongezeka?

Labda UKAWA watuambie kwamba hii ni strategy yao ya kupunguza nguvu za CCM kwa nia ya kupata shortcut kupata mamlaka ya inchi, wengi wanadai kwamba serikali 3 ndio maoni ya walio wengi, Napata shida kidogo katika hoja hii kama alivyokuwa anahoji Prof Remmy, mbona idadi kubwa ya waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano ni kutoka mikoa 2 kigoma na Dar, sasa inawezaje mikoa 2 katika mikoa zaidi ya 25 Tanzania bara iwakilishe inchi nzima?.

Jambo jingine ambalo nalo ni kwa nia njema tu najiuliza Tanzania imeshaingia mikataba mingi ya kimataifa,kwa jina Tanzania pamoja na kukopa kwa dhamana ya inchi Tanzania, sasa itakapotokea tukabadili muundo wetu na tukawa Tanganyika nini hatima ya mikataba ile ? ikiwa kupata kanuni za kuliongoza bunge maalumu tu la katiba ilichukua 40days, hivi kufikia maridhiano ya kugawana mali na madeni tumeshawahi kufikilia itakuwaje?.achilia mbali Tanganyika kujipanga upya sasa kupata muundo wa kiutawala.

Tumeshawahi kujiuliza hii serikali ya 3 ambayo ni ya shirikisho kwa mfumo wetu tulionao ikitokea Tanganyika CDM wameshika dola, Zanzibar CCM wameshika dola alafu serikali ya shirikisho CUF ikapata mamlaka huyu amiri jeshi mkuu ambaye yeye hana maslahi Tanganyika kwa maana sio chama tawala atakuwaje anatenda usawa.? najiuliza tu lakini sijapata jibu waungwana labda tusaidiane katika hili.
 
Tangu mwanzo mchakato mzima wa Katiba Mpya ulishaonekana kuwa na ubabaishaji usioelezeka. Rais ameyumbishwa sana na chama chake.Hata hivyo Mungu hakuiacha Tanzania na akamuongoza Rais wake na kumwezesha kutetua CRC ambayo kwa wastani ilikubalika. Tumshukuru Mungu kwa hilo. CRC ilifanya kazi nzuri yenye lengo la kupatanisha makundi mbalimbali katika jamii yetu. Bahati mbaya sana wakajitokeza wenye roho mbaya ambao wanaona wao wameshika mpini na wana nguvu hivyo hawahitaji kupatanishwa na mtu yeyote; wanajitosheleza na wanao uwezo wa kupata kile wanachotaka. Jirani zetu waliita "tyranny of numbers". Lakini ona nchi hiyo ilivyogawanyika sasa kutokana na uroho wa wanasiasa. Kila hatua ya mchakato wa katiba mpya ikawa na mizengwe na matumizi ya nguvu nyingi kuhakikisha kuwa mchakato wote unahodhiwa na serikali hali iliyoonyesha kuwa nia haikuwa njema tangu mwanzo. Hitimisho la yote haya ni pale Rais alipoaminishwa kuwa hata kwenye uteuzi wa CRC alikuwa amepotoka! Akaamishwa kuwa kwa sababu ni yeye ndiye aliyetua CRC isiyofaa basi analo jukumu la kusaidia katika kusambaratisha Rasimu ya Katiba Mpya. Zikaanza juhudi za kusambaratisha rasimu ya kwanza ya katiba katika mabaraza ya wilaya. Kwa bahati nzuri CRC ilikuwa na madaraka na ilijua hayo yote, hivyo ikajizatiti kuzuia mabaraza kutumika isivyostahili kutengua maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu. Hilo liliposhindikana mapambano yakahamia kwenye CA. Hapa, kwa bahati mbaya hata Rais wetu akaendelea kupotoshwa na kuingizwa katika mtego wa kushiriki kuvuruga rasimu ya pili na CA kwa ujumla. Kimsingi mtafaruku uliopo sasa umeanzishwa na hotuba ya Mheshimiwa Rais pale alipotamka maneno ambayo hayakustahili kutamkwa na yeye; maneno ambayo yamewaacha wengi wakijiuliza kama kweli yametoka kwa Rais wao. Kauli yake ya Jeshi kupindua serikali sasa imekuwa wimbo wa kuimbwa hata makanisani kama siyo hirizi nyingine. Kimsingi, baada ya hotuba ile ya Rais na kwa kuzingatia jinsi CA yenyewe ilivyoundwa, kila mwenye akili na uelewa wa kutosha alijua kuwa Katiba Mpya itakayoandikwa ni ile inayokidhi sera ya chama tawala na siyo maoni ya wananchi yaliyotolewa CRC. Nilimuona mjumbe mmoja wa CA kutoka chama tawala akiwashauri wenzao wa UKAWA kwamba wajenge hoja ili angalau wakubaliwe kuambulia kitu wasitoke patupu!. Kila mjumbe wa CA mwenye mawazo tofatuti na yale ya chama tawala alikuwa na mtihani wa kuchagua moja kati ya mambo mawili: kutelekeza maoni ya wananchi na kushiriki kubariki katiba mbadala ya chama tawala au kutoshiriki. Hili lilikuwa limeshaandikwa wazi ukutani tangu pale CA ilipofunguliwa na Mheshimiwa Rais. Lakini kama vile Mungu alivyomuongoza Rais wetu kuteua CRC nzuri, kisha akaiongoza CRC kufanya kazi nzuri ndivyo tunavyopswa kuendelea kuamini kuwa yu pamoja na Tanzania na atatenda miujiza yake ambayo ametuonyesha kupitia CRC. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hebu tueleze huo utaratibu sahihi waliopaswa kuufuata kama walikuwa na nia ya kutoka?

Mlango wa spika na waziri mkuu kama viongozi bungeni uko wazi kupokea malalamiko yeyote kuhusiana na bunge hilo. Nimemsikia spika wa bunge akisema hana taarifa yeyote juu ya kuondoka kwa UKAWA.
 
CCM ni chama dume kitaendelea kupeta daima,Mbowe na wenzake wamekosa hoja ndiyo maana wameamu kutoka bungeni maana wameona walichokuwa wanakitegemea hakitakuwa na hivyo watashindwa cha kuwaeleza wafuasi wao wanywa viloba.
Na wewe ni mfuasi Jike sio?
 
CCM ni chama dume kitaendelea kupeta daima,Mbowe na wenzake wamekosa hoja ndiyo maana wameamu kutoka bungeni maana wameona walichokuwa wanakitegemea hakitakuwa na hivyo watashindwa cha kuwaeleza wafuasi wao wanywa viloba.

Unaongea kwasababu baba yako ni kada wa ccm na wachumia tumbo. Sikulaumu koz siku ccm iking'oka mnakufa kwa presha, ccm ndio maisha yenu. Ila nakuoneeni huruma sana anzeni kutafuta shughuli za kufanya ili muwe na uhakika wa maisha yenu ya badae ccm itabwagwa siku c nyingi. Angalia kenya, Libya, Misri na kwingineko hakuna ufalme uliwahi kudumu. Fuatilia pia historia ya utawala wa RUMI usikae na kujipa matumaini
 
Eti leo CCm wanadai kuwa serikali tatu ni mzigo kwa wananchi, leo ndio wanamfikiria huyu mwananchi wakati muda wote wanamdhoofisha na sera mbovu za kiuchumi, miundominu,afya, elimu na mengineyo. Hiyo huruma ya CCM inatoka wapi? Wazandiki, mafisadi na wahuni wakubwa wanaoendelea kuliibia taifa letu na wananchi wake kwa kuwadanganya eti kuendelea kudumisha amani iliyopo. Amani ipi iliyoko Tanzania? muda wenu umeisha nyie CCM na soon u will realize.

Watetezi na waumini wa serikali 2 wanasema kuwa na serikali tatu kutaongeza gharama na Serikali ya Muungano haitakuwa na mapato hivyo Muungano kufa, Je, Muungano wa serikali mbili uliopo sasa nani anaugharimia?

Serikali ya Muungano inaendeshwa kwa mapato gani na yanatolewa na Nchi gani au zipi Zanzibar au Tanganyika mfu? hapa sina jibu sahihi.. na sitaki kuendelea kuishi bila kuwa na majibu sahihi. Watetezi na waumini wa serikali 2 weka majibu hapa.
 
Back
Top Bottom