Kauli ya Mbowe: UKAWA kutoka bungeni

Kauli ya Mbowe: UKAWA kutoka bungeni

sem2708

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,820
Reaction score
4,968
Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.

Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali h
 
Tuliwahi kufundishwa ili nchi ipate maendeleo inahitaji WATU,ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Tatizo liko hapo kwenye UONGOZI BORA. Tunawatu ambao hawastahili kuwa hata wakuu wa kaya zao lakini wananafasi za uongozi wa kitaifa. Kama kuna pa kurekebisha ni kwenye namna ya kupata viongozi bora maana hawa tulio nao (m.f Nape na Mwigulu) kutokana na kukosa kwao sifa stahili wanachafua siasa na kurudisha nyuma maendeleo
 
Mbowe hana hoja atafute sababu zingine za kusingizia kwanza matusi alianza Lisu baadaye jusa mbowe naye akaja kutukana matusi kibao sasa nini anachoongea bora akae kimywa kwanza yeye ndiye anaongoza pia kwa ubaguzi rejea walivyombagua zitto.
 
ccm wanalazimisha kitu ambacho sio realistic
Kipi kinacholazimishwa leo wajumbe wote wapo bungeni wanaendelea na mijadala wametoka chadema na cuf pamoja na mbatia ila naona huelewi unachosema.
 
CCM ni chama dume kitaendelea kupeta daima,Mbowe na wenzake wamekosa hoja ndiyo maana wameamu kutoka bungeni maana wameona walichokuwa wanakitegemea hakitakuwa na hivyo watashindwa cha kuwaeleza wafuasi wao wanywa viloba.
 
Kumbe CCM walidumaza elimu ili watuburuze watakavyo? Watanzania wa leo hatudanganyiki! Boresheni daftari la wapiga kura tukutane vituoni.
 
Sasa kifuatacho tunasubiri nguvu ya wanaich. Katiba mpya itapatikana. Hata kwa kutumia nguvu. Ccm wanafikir wao wana nguvu za kumtawala kila mtu. Lakin hawajui kuwa wananch wana nguvu kuliko serikali. Waulize mini kilichotokea misri
 
CCM ni chama dume kitaendelea kupeta daima,Mbowe na wenzake wamekosa hoja ndiyo maana wameamu kutoka bungeni maana wameona walichokuwa wanakitegemea hakitakuwa na hivyo watashindwa cha kuwaeleza wafuasi wao wanywa viloba.
Naam.
Lakini nje ya nchi (kimataifa) Tanzania inazidi kuchuja.
 
CCM, mna hakika gani kuhusu maoni yenu ya serikali mbili kwa wananchi hasa wa Zanzibar? Fumbueni macho. Kuweni na utashi!
 
Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi. Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali hii ?
 
Kama Makamu na Mwenyekiti wake wangekuwa FIRM kuhusu hali ilivyokuwa BUNGENI haya yote yasingetokea.Hata leo badala ya kujadili Rasimu wanajadili watu,sasa sielewi kama kwenye hansard za bunge yanaingia na yale matusi,kama yanaingia basi watoto na wajukuu zetu watatucheka.
 
Tuliwahi kufundishwa ili nchi ipate maendeleo inahitaji WATU,ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Tatizo liko hapo kwenye UONGOZI BORA. Tunawatu ambao hawastahili kuwa hata wakuu wa kaya zao lakini wananafasi za uongozi wa kitaifa. Kama kuna pa kurekebisha ni kwenye namna ya kupata viongozi bora maana hawa tulio nao (m.f Nape na Mwigulu) kutokana na kukosa kwao sifa stahili wanachafua siasa na kurudisha nyuma maendeleo
Hao wawili mlaumu aliewapa hizo nafasi,inawezekana na yeye ni wa style hiyohiyo,(show me your friend and i will tell who you are)
 
Inafaa washitakiwe hawa ccm tangu Rais hadi wote wanaoathiri mchakato wa kupata katiba mpya. Maana wametumia kodi za wananchi kuendesha mchakato wa katiba wenye hila na kiini macho. Maana walikuwa tayari wana katiba yao ya serikali mbili. Sasa ya nini kupoteza mapesa yetu. Huu ni unafiki mkubwa na kiini macho!
 
Wanaotakiwa kushtakiwa kwa kuathiri mchakato wa Katiba ni hawa waliotoka nje ya bunge kinyume na utaratibu.
 
Mbowe amevurugwa, akumbuke matusi ya wehu anaowaongoza akina nassari, sugu na msigwa kila waliposimama kuchangia bungeni. Wamelianzisha wenyewe
 
Back
Top Bottom