Kauli ya Lugola kuhusu watanzania wasiende kufanya kazi nchi za nje na akili ya Mwafrika chini ya Jangwa na Sahara

Ndiyo. Kama huna contract hakuna kwenda. Mnakuja kuanza kusumbua mabalozi hapa
 
Inawezekana kabisa agizo na utekelezaji vikawa vitu tofauti kabisa, agizo kama agizo ni la nia njema, kulinda utu wa ndugu zetu wanaoenda ingia matatizoni. Umuhimu upo kwa hao watekelezaji wa hili agizo.
Mkuu,hali iko hivyo katika Airport ya Daressalam,imekuwa sio rahisi kwa vijana wa Kitanzania kusafiri kwa kupitia hapo,juzi tu vijana hao hao walikwenda kuishangalia Dreamliner....kwa kweli sifahamu kwanini serikali iwatese vijana wake,kisa kusafiri kwenda nje

Kuna message nyingi sana zimesambaa mitandaoni kwa njia za Whatsapp na nyenginezo vijana wakilalamika haya mateso wanayoyapata wakitaka kusafiri kupitia Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere,nafikri CCM mjiandae vizuri 2020,kumbukeni vijana ndio taifa la kesho,mnaifanya nchi iwe kama North Korea,inasikitisha
 
Ndiyo. Kama huna contract hakuna kwenda. Mnakuja kuanza kusumbua mabalozi hapa
:eek: unataka ukae kwenye kiti cha kuzunguka usisumbuliwe, Mkuu..usichukulie kuwasaidia wenzako waliopata matatizo ni usumbufu chukulia kuwa ni moja katika kazi yako...
 
Tatizo langu mimi na watu kama Kangi Lugola na Magufuli hata kama si la kitu cha msingi wanachotaka kufanya, ni jinsi wanavyotaka kufanya kitu hicho.

Watu wa PR wanajua presentation is part of the message.

Yani hata kama wanataka kufanya kitu kizuri, kitafanywa kwa ubabe ubabe usio na lazima, kauli za ajabu ajabu zisizo lazima, mpaka mtu akisikiliza inakuwa rahisi sana kusikia kitu tofauti, au mpinzani anayetaka kupindisha maana anakuwa na kazi ndogo tu.

Mimi napenda kuwa nuanced, sitaki kuwa simpleton.

Katika ulimwengu wa leo ambao wafanyakazi wa ndani wanafanyiwa mambo mabaya sana Urabuni, sex trafficking ipo sana, watu wanakwenda Ulaya kwa njia za panya na kuhatarisha maisha yao, wahamiaji wasio na shughuli hawatakiwi nchi karibu zote etc, kuna sehemu serikali ina wajibu wa kuhakikisha watu wake wanapokwenda nje, wana sababu za kueleweka na mikataba inayotambulika.

Hilo mimi sina mjadala nalo sana.

Tatizo linakuja pale waziri anapotumia habari hii kusema kwa vitisho kiasi cha kufanya baadhi ya watu walio nje kuanza kuulizana, hivi leo tukirudi Tanzania likizo, tutahitaji turudi na mikataba yetu ya kazi, ili tukimaliza likizo zetu tuwaoneshe uhamiaji kwamba tunaporudi tena makazini nchi za nje, tuna kazi zinatusubiri na hatuendi kubangaiza?

Kuna watu hata wanapofanya kitu kizuri, wanakifanya vibaya kinapoteza maana yote.

Kangi Lugola na bosi wake Magufuli ni watu wa aina hii.

Zaidi, serikali kandamizi, hususan zisizo usimamizi wa kueleweka kama kwetu huko Tanzania, mara nyingi sana zinajua kutumia sheria halali zenye mantiki (kama sheria za kuzuia sex trafficking etc) katika mambo yasiyo angukia katika habari hizo (kuzuia vijana wanaoamua kupiga kura kwa miguu yao kuondoka Tanzania kutafuta kazi, biashara na maisha nje ya Tanzania kama mimi).Sasa, waziri anapohemuka na kumaka kuhusu hizi habari, hususan waziri mwenye track record ya kuhemuka, mtu akiwa concerned kwamba hizi habari zitakuwa mtego wa panya unasao wanaotakiwa na wasiotakiwa, atakuwa na uhalali wa kufikiri hivyo.
 
kuzungumzia watanzania pekee wasiende kufanyakazi nje ya nchi bila kugusia wageni wasije kufanyakazi nchini kwa utaratibu uleule aliopiga marufuku watanzania sio sahihi, wapo wafanyakazi wa kigeni wapo nchini kwa zaidi ya miaka kumi na tunashangaa wanapataje vibali vya kufanyakazi nchini huku wakiwanyanyasa watanzania wenye elimu kwa kuwapa mishahara duni mazingira yasiyokuwa rafiki ya kazi.

Juzi tuliona Raia wa kigeni akipewa nafasi ya juu katika shirika lenye watanzania wana hisa wengi pasipokuwa na sifa stahiki lakini hatukusikia waziri akitoa kauli wala kulizungumzia hilo.

ifike sehemu tufikiri kama watu wenye akili timamu badala ya kuweka akili pembeni na kutumia njia zisizo sahihi kufikiri kama marehemu didas masaburi alivyosema.
 
:eek: unataka ukae kwenye kiti cha kuzunguka usisumbuliwe, Mkuu..usichukulie kuwasaidia wenzako waliopata matatizo ni usumbufu chukulia kuwa ni moja katika kazi yako...
hiyo ndiyo perception ya watumishi wa umma walio wengi, ni miungu watu wanawaona wananchi ni bugudha, wanadhani ipo kada fulani ndio wanapaswa kuihudumia.
 
Habari wana jamvi … naona waziri hajakurupuka yupo sahihi … na ndio anaonyesha makucha halisi ya tawala yetu … kawaida hata kabla hajatamka haya … kupata passport kwa mtanzania wa kawaida ni kitu kigumu sana!! .. wengine wenu humu mnaweza kuwa mashahidi ! mtazamo wangu binafsi ni kwamba .. utawala huu ata iliyopita sera yao ya uhamiaji imekaa kuminya watu wasitoke nje Zaidi . maana ukienda kuomba passport kihalali tu mlolongo ni mrefu kweli $$ …. labda uonge ndio inaweza kuwa kama shortcut au ukitokea ndani ya mfumo ni fasta zaidi ….bila hivyo inahitaji maelezo mengi sana … umeongelea Kenya mleta mada …asilimia 25 % ya wakenya wapo ughaibuni na wanaleta hela nyingi sana kwao kila mwaka kwa ndugu na jamaa zao hivyo kusaidia uchumi wa nchi na watu wake !!! hitimisho niii mfumo wetu unadumu kutawala kutokana na watu wake kukosa elimu au maarifa , umaskini wetu na pia kukosa exposure …...
 
Huyu Mh. anafanya watu wote wenye miili mikubwa na vitambi waonekane wapuuzi, Inalilah wainailayhi rajiun.
 
Nadhani tamko la Waziri linakuja baada ya malalamiko ya watanzania vijana wanaonyanyaswa huko ughaibuni wanakofanyia kazi husani nchi za waarabu na india
 
Ninja kakurupuka, katika hili nasema kakurupuka hasa! Hivi hawa viongozi wetu wanashauriwa na nani? ni kweli kwamba hafahamu au hana taarifa ya hali ya ajira na mazingira ya kujiajiri Kwa vijana yalivyo magumu Kwa sasa hapa nchini?
Nitafurahi sana kama utaweka walau moja ambalo hakukurupuka ili tubalance stori
 
Nadhani tamko la Waziri linakuja baada ya malalamiko ya watanzania vijana wanaonyanyaswa huko ughaibuni wanakofanyia kazi husani nchi za waarabu na india
njia sahihi sio kuwazuia kwenda ni kuangalia namna gani haki zao zitakavyopatikana watakapo kuwa huko ikiwemo kufungua madawati ya kupokea malalamiko katika balozi husika.
 
Ni kweli huyu waziri amekuwa ni mtu wa kukurupuka lakini hiyo habari umeipotosha sana kwani alizungumzia ajira haramu kama za watoto kuchukuliwa mikoani na kuja kutumikishwa, pia watu kuahidiwa ajira nje lakini wakifika huko wanatumikishwa ama kwa ngono au kunyanyaswa.
Mara ngapi watu wametoa post hapa kuonyesha watanzania wanavyonyanyaswa uarabuni wakifika wananyang'anya pasiport na kutendewa vibaya

ulitakiwa uweke habari yote
 
NImeona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha waziri wa ndani akihutubia,na kumuagiza Kamishina General wa uhamiaji kuwa asiwaruhusu vijana wa kitanzania wanaotaka kwenda nje kufanya kazi kama hawajakamilisha vigezo vya kufanya kazi nje..,Mwisho akamalizia kuwa vijana wa Kitanzania wasiende kufanya kazi nje..

Nimekaa na kujiuliza kwanini Waziri amekuja na kauli kama hii,kwanini kaona aweke marufuku kwa vijana wa kitanzania kwenda kufanya kazi nje,.Tunaona nchi jirani ya Kenya vipi inavyowapeleka vijana wake kwenda kufanya kazi Ughaibuni,kwa wale waliopata bahati ya kufika nchi za UAE,Dubai na Qatar,hapo utawakuta Wakenya wengi sana wanafanyankazi mbali mbali pale Airport...Kenya tukitaka tusitake wametushinda Kiuchumi,kwanini wao wawaruhusu raia wao wakafanye kazi nchi,watanzania wakataze raia wake kufanya hivyo???

Sote tunajua,dunia inajua kuwa nchi za Afrika chini ya jangwa na Sahara(Nchi za waafrika weusi) ni nchi masikini sana lakini ni nchi tajiri sana kwa rasiimali,kwanini hasa iwe hivyo,..??Majuzi tu tumeona nchi za Morokko wakicheza kombe Dunia,..Kwa kweli wachezaji takribani wote wa Morokko hakuna hata mmoja aliezaliwa Morokko,wote wamezaliwa nchi za Ulaya ya Magharibi...!!!

Sasa utajiuliza kwanini Morokko imefanya hivyo?Ukweli Morokko imeizidi sana Kiuchumi Tanzania,lakini maamuzi ya serikali ya Morokkko imekuwa hivyo kuhusu vijana waliokwenda kuiwakilisha Morokko kwenye "World Cup".Wamokko ni wafrika waliokuweopo juu ya Jangwa la Sahara(Waafrika weupe,waafrika wenye asili ya Kiarabu)..kwanini maamuzi ya waafrika wenye asili ya Kiarabu na waafrika wenye asili ya Ubantu wawe tafauti kimawazo...!??

Nilivyoona mimi hawa wafrika walioko juu ya jangwa la Sahara(weupe) hawafikiri kama waafrika walioko chini ya jangwa la sahara(weusi),Wafrika tuliko chini ya jangwa la sahara(weusi) tunaelekeza hisia kwenye maamuzi yetu kuliko uhalisia,Wamoroko wanalijilipa kwa yale yote waliyofanyiwa na Wafaransa,Morokko ilitawaliwa na Ufaransa,Morokko haiwezi kulipiza kisasi kwa Ufaransa kwa kupigana nao,..lakini wanaweza kulipiza kisasi kwa kupeleka vijana wakafanye kazi Ufaransa na kuleta pesa na mali nyengine Morroko,hayo nimawazo ya mwafrika mweupe...!!,huu ni mfano wa nchi moja tu,kuna nchi kama ya Philipines,takriban pesa za kigeni zinazoingia Philipinies chanzo chake ni wafilipini wanaofanya kazi nchi za nje..

Kwa mwafrika mweusi kama sisi watanzania, mawazo na fikra zetu ziko tafauti,kwasababu tunaelekeza hisia kuliko uhalisia kwa kila tunachokifanya na kwa kila maamuzi yetu,tunaona kuwa kama tutawaruhusu vijana wa Kitanzania kwenda kufanya kazi nchi za nje ni kuitia aibu Tanzania,Wazungu walipokuja afrika kututawala hawakuja wazee serikali zao walileta vijana wengi sana ili waje kuchukua kila wanachoweza kuchukua katika bara la Afrika,wakati huo kulikuwa hakuna usafiri wa anga Wazungu walikuwa wanakuja Afrika kwa majahazi ya tanga,wanategemea upepo kuja Afrika,unajua majahazi mangapi yalizama,vijana wangapi walikufa,mbona hawakuona aibu!!??

Bahari ya Atlatic ni bahari chafu sana,kuliko bahari zote duniani,mawimbi yake makubwa sana ukifanananisha na bahari nyengine,..Christopher Columbus alivyovumbua "dunia mpya",mamimia kwa mamia ya wazungu wa nchi za Ulaya Mgharibi walipanda majahazi na kwenye kutafuta bahati zao kwenye "Dunia mpya"(Amerika),unajua majahazi mangapi yalizama,unajua vijana wangapi wa kizungu walikufa!!?mbona wazungu hawaoni aibu..!!?

Tuige nchi ya Japani,walipooona hawawezi kupigana na kuwashinda Wazungu waliamua kuwachia vijana wao kwenda nchiza Magharibi na Marekani kusoma na kuiga yaleyanayofanywa huko,hvi sasa Japan ni nchi peke yake Dunia ambayo sio ya Wazungu inayoweza kuleta ushindani mkubwa wa kiteknologia kwa nchi za Wazungu..

Mh Waziri wa mambo ya ndani waache vijana wa kitantanzani wakatafute Maisha katika "Dunia Mpya",fanya iwe rahisi kwa vijana kwenda kutafuta maisha popote wanapotaka,wageni walikuja na kututawala,nasi acha twende tukawatawale kivyetu...,si dhambi kwa mtanzania kusafiri na kuona dunia na yale mazuri aliyoyaona huko alikokwenda kuja nayo nyumbani na kuchangina na watanzania wengine...
We jamaa hivi unaelewa kilichosemwa au, huko nje waafrica wananyanyaswa, mi kuna jamaa alienda qatar kupiga kazi ya viwandani na wengine mabek 3 ila hizo alizokuta huko alirudi na hakuna kitu alichopata na hadi leo yupo mtaani anasema hata bure haendi uarabuni, sasa ww unafyokoa ushuzi huko wakati kule hawana haki wakileta kulalamika wanaambiwa watarudishwa kwao, mabalozi hawawez kuwasaidia maana hawana mikataba ya kazi ya kuwatetea wao, fikiria vizuri mkuu, kwani wakipewa mikataba ni dhambi, maana kama una nia nzuri ya wananchi wako na ili wasikuletee malalamiko baadae basi mbane mwajiri wake ili mwajiriwa akilia basi tumbane mwajiri atoe haki yake sio unawarusha kule afu wanaonewa afu wanaenda kujazana ubalozini hawana hata hela za kurudia, we jamaa wale waarabu, wazungu sio ndugu zako hawana hata huruma na wewe, kule mwenyeji wako anayeweza kukutetea ni balozi wako tu, wengine wanakuangalia km mshkaki wanakumeza tu hawapotezi hata usingizi
 
Chief, hujaeleza vya kutosha kuhusu hilo katazo la waziri, kulinga na maelezo yako hapo juu Sioni katazo naona ruhusa yenye kuzingatia vigezo! Embu eleza vizuri taarifa yako hii ieleweke.
Hajajua alichosema anaropoka tu, mimi binafsi naona waziri anajaribu kutetea haki ya msafiri na kumlinda dhidi ya mwajiri wake, wale wazungu na especially waarabu hawana haki wale, nnao washkaji walienda walikaa miaka miwili walirudishwa na ndege hadi hapo JNIA wana pocket money tu
 
njia sahihi sio kuwazuia kwenda ni kuangalia namna gani haki zao zitakavyopatikana watakapo kuwa huko ikiwemo kufungua madawati ya kupokea malalamiko katika balozi husika.
Wale waarabu hawajui mambo ya kumtetea mwajiriwa wao ni kazi km huwez sepa, huna wa kumlilia kule, usipoenda ww ataenda mhindi, mfilipino etc hilo dawati utalipeleka shule wakakalie wanafunzi
 
kuzungumzia watanzania pekee wasiende kufanyakazi nje ya nchi bila kugusia wageni wasije kufanyakazi nchini kwa utaratibu uleule aliopiga marufuku watanzania sio sahihi, wapo wafanyakazi wa kigeni wapo nchini kwa zaidi ya miaka kumi na tunashangaa wanapataje vibali vya kufanyakazi nchini huku wakiwanyanyasa watanzania wenye elimu kwa kuwapa mishahara duni mazingira yasiyokuwa rafiki ya kazi.

Juzi tuliona Raia wa kigeni akipewa nafasi ya juu katika shirika lenye watanzania wana hisa wengi pasipokuwa na sifa stahiki lakini hatukusikia waziri akitoa kauli wala kulizungumzia hilo.

ifike sehemu tufikiri kama watu wenye akili timamu badala ya kuweka akili pembeni na kutumia njia zisizo sahihi kufikiri kama marehemu didas masaburi alivyosema.
Sio kweli mkuu
 
Wale waarabu hawajui mambo ya kumtetea mwajiriwa wao ni kazi km huwez sepa, huna wa kumlilia kule, usipoenda ww ataenda mhindi, mfilipino etc hilo dawati utalipeleka shule wakakalie wanafunzi
tunae balozi kule na wasaidizi wakutosha iweje watanzania wanyanyasike, mmarekani anapokuja nchini hata kama kaja kufanya utalii wa ngono ubalozi unajua na wanafatilia na chochote kibaya kikitokea wanachukua hatua iweje sie balozi anayelipwa kwa kodi za wazazi wa hao vijana ashindwe kuchukua hatua stahiki?
 
tunae balozi kule na wasaidizi wakutosha iweje watanzania wanyanyasike, mmarekani anapokuja nchini hata kama kaja kufanya utalii wa ngono ubalozi unajua na wanafatilia na chochote kibaya kikitokea wanachukua hatua iweje sie balozi anayelipwa kwa kodi za wazazi wa hao vijana ashindwe kuchukua hatua stahiki?
Hatua stahiki ndo wanakusanywa kwenye ndege wanarudi home, mkuu mi situngi stori nayosema ni real nimehadithiwa na bro ambaye kaenda kufanya kazi kiwandani qatar, miaka iliyopita km mi4 hv, sahv yupo kitaa anafanya kilimo, anasema kule kazi zipo ila ukisikia watu wanarudishwa ujue kumeshindikana, hamna mtu anayelalamika kwenye raha mkuu
 
Back
Top Bottom