Nimekuja kwenu leo, si kwa hasira, bali kwa msimamo wa mtu ambaye ametafuta ukweli katika Biblia na pia katika Qur’ani.
Swali hili linaibua mjadala wa kina kuhusu uungu wa Yesu kulingana na Maandiko ya Kikristo. Kama Yesu ni Mungu, basi ni kwa nani alikuwa anaomba?
Katika Biblia tunasoma: Yesu alianguka kifudifudi na kuomba katika Gethsemane (Mathayo 26:39).
Alilia na kusihi kwa machozi akimwomba Yule aliyeweza kumuokoa na mauti (Waebrania 5:7).
Alipokuwa msalabani, alipaza sauti: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?” (Mathayo 27:46).
Ikiwa Yesu ni Mungu, alikuwa anaomba kwa nani? Je, Mungu anaweza kuomba kwa Mungu mwingine? Au haya ni ishara kwamba Yesu alikuwa mtumishi wa Mungu, si Mungu Mwenyewe?
Katika Kurani Tukufu, Allah haombi, haliombi, wala hahitaji. Yeye ni Mwenye Kujitosheleza daima. Hili ni swali lenye uzito kwa waumini wa Kikristo: Kwa nini Mungu wa Biblia anaomba, wakati Mungu wa Uislamu hahitaji kuomba?
Ikiwa Yesu ni Mungu, basi alikuwa anamuomba nani? Je, Mungu anajiombea mwenyewe? Au Yesu alikuwa anaonesha kwamba yeye ni mtumishi, si Mwenyezi?
Kwa nini aseme, “Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28), na tena, “Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu” (Yohana 20:17)?
Kwa nini Paulo atangaze: “kichwa cha Kristo ni Mungu” (1 Wakorintho 11:3)?
Kauli hii inaonesha wazi kuwa Yesu Kristo yuko chini ya mamlaka ya Mungu, akimtambua Mungu kuwa juu yake — jambo ambalo lingekuwa gumu kueleweka ikiwa Yesu angekuwa Mungu.
Tanbihi
Tujikite kwenye Mada sio kutumia jaziba mihemuko chuki gadhabu matusi nk, tuko hapa kujifunza, leteni utetexi wa ushsahidi plz