Kauli ya kweli: Je, Mungu huomba?

Kauli ya kweli: Je, Mungu huomba?

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,674
Reaction score
41,114
Nimekuja kwenu leo, si kwa hasira, bali kwa msimamo wa mtu ambaye ametafuta ukweli katika Biblia na pia katika Qur’ani.

Swali hili linaibua mjadala wa kina kuhusu uungu wa Yesu kulingana na Maandiko ya Kikristo. Kama Yesu ni Mungu, basi ni kwa nani alikuwa anaomba?

Katika Biblia tunasoma: Yesu alianguka kifudifudi na kuomba katika Gethsemane (Mathayo 26:39).

Alilia na kusihi kwa machozi akimwomba Yule aliyeweza kumuokoa na mauti (Waebrania 5:7).

Alipokuwa msalabani, alipaza sauti: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?” (Mathayo 27:46).

Ikiwa Yesu ni Mungu, alikuwa anaomba kwa nani? Je, Mungu anaweza kuomba kwa Mungu mwingine? Au haya ni ishara kwamba Yesu alikuwa mtumishi wa Mungu, si Mungu Mwenyewe?

Katika Kurani Tukufu, Allah haombi, haliombi, wala hahitaji. Yeye ni Mwenye Kujitosheleza daima. Hili ni swali lenye uzito kwa waumini wa Kikristo: Kwa nini Mungu wa Biblia anaomba, wakati Mungu wa Uislamu hahitaji kuomba?

Ikiwa Yesu ni Mungu, basi alikuwa anamuomba nani? Je, Mungu anajiombea mwenyewe? Au Yesu alikuwa anaonesha kwamba yeye ni mtumishi, si Mwenyezi?

Kwa nini aseme, “Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28), na tena, “Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu” (Yohana 20:17)?

Kwa nini Paulo atangaze: “kichwa cha Kristo ni Mungu” (1 Wakorintho 11:3)?

Kauli hii inaonesha wazi kuwa Yesu Kristo yuko chini ya mamlaka ya Mungu, akimtambua Mungu kuwa juu yake — jambo ambalo lingekuwa gumu kueleweka ikiwa Yesu angekuwa Mungu.

Tanbihi

Tujikite kwenye Mada sio kutumia jaziba mihemuko chuki gadhabu matusi nk, tuko hapa kujifunza, leteni utetexi wa ushsahidi plz
 
Mungu alikuja Katika mwili wa Mwanadamu akawa kama Mwanadamu. (Wafilipi 2:7-9)., John Chapter 1:1-3).

Mwili ni mwanadamu,

Roho ni Mungu,

Sasa akivaa mwili lazima aombe Ili kutimiza sifa za mwili ambao ni dhaifu,

Lakini Katika Roho ni Mungu huyo huyo mmoja.

Mungu ni mmoja tu na jina lake personal tullilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ni Yesu Kristo/Yeshua Hamashiach
 
Mungu alikuja Katika mwili wa Mwanadamu akawa kama Mwanadamu.

Tunaomba ututenganishie lini alikua Mungu na wakati gani alikua binaadamu?
 
Tunaomba ututenganishie lini alikua Mungu na wakati gani alikua binaadamu?
1.Alikuwa Mungu milele kabla hajavaa mwili .

2. Alipokuja Katika mwili wa Mwanadamu akaendelea kuwa Mungu Katika Roho, mwili wa Mwanadamu.

3. Alipofufuka na kupaa mbinguni, amerudi Tena Katika mwili wa Roho ndiye Mungu huyo huyo aketiye kiti Cha Enzi.

Ndio maana mabaki ya mwili wa Yesu hayapo popote.

Ni Mungu huyo.
 
Mkuu bado hujaja na hoja mada ni kuomba sio kupaa je Mungu huomba? Alikua anaomba kwanani?
Alipovaa mwili akawa mfano wa mwanadamu aliomba kwa Yeye mwenyewe,

Sifa kuu ya Mungu ni kuwappo everywhere at once,

Alimba akiwa na mwili duniani, hapo hapo Ni Mungu mbinguni Katika Roho.

Aliomba Ili kuonyesha kujishusha sababu ya kuvaa mwili.

Ndio maana kuna wakati alisema, ninajua umenisikia, ila mapenzi Yako yatimizwe.

Hata WEWE kuna time unasema na kubishana na nafsi yako, lakini wewe ni yule yule mmoja.
 
1.Alikuwa Mungu milele kabla hajavaa mwili .

2. Alipokuja Katika mwili wa Mwanadamu akaendelea kuwa Mungu Katika Roho, mwili wa Mwanadamu.

3. Alipofufuka na kupaa mbinguni, amerudi Tena Katika mwili wa Roho ndiye Mungu huyo huyo aketiye kiti Cha Enzi.

Ndio maana mabaki ya mwili wa Yesu hayapo popote.

Ni Mungu huyo.
3.huko mbinguni baada ya kupaa tunaambiwa ameketi kuume kwa Mungu baba mwenyezi
 
Hata Allah pia anaswali sasa huwa najiuliza na yeye anaswali kwa nani??
Innallah wamalikatahu yuswalluuuna ala nnabiiy
 
Mungu alikuja Katika mwili wa Mwanadamu akawa kama Mwanadamu.

Mwili ni mwanadamu,

Roho ni Mungu,

Sasa akivaa mwili lazima aombe Ili kutimiza sifa za mwili ambao ni dhaifu,

Lakini Katika Roho ni Mungu huyo huyo mmoja.

Mungu ni mmoja tu na jina lake personal tullilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ni Yesu Kristo/Yeshua Hamashiach
Unanichanganya zaidi,kwaiyo Mungu alikuwa anajiomba yeye mwenyewe.
 
1.Alikuwa Mungu milele kabla hajavaa mwili .

2. Alipokuja Katika mwili wa Mwanadamu akaendelea kuwa Mungu Katika Roho, mwili wa Mwanadamu.

3. Alipofufuka na kupaa mbinguni, amerudi Tena Katika mwili wa Roho ndiye Mungu huyo huyo aketiye kiti Cha Enzi.

Ndio maana mabaki ya mwili wa Yesu hayapo popote.

Ni Mungu huyo.
Mbona unajigonga gonga jitahidi uwe sitaiti:
Kilicho fufuka ni mwili au Roho?
Alivo paa ilikua roho au mwili?
Mungu as Nahitaji mwili wa binaadamu wa kazi gani?

Acha kujificha kwenye roho, roho ya binaadamu inatenganishwa na kifo tu.
 
Hiyo Haina tofauti na ile ya Allah anapoungana na malaika zake wanapanga muda wanakutana kumswalia Muhammad.
 
Kila siku tunawaambia muachane na hizo ngano za kirumi hamuelewi. Nyie wenyewe yanawachanganya ila kwa neno la Kuamini na kuogopa ukihoji utakufuru basi mnabaki ka wendawazimu tu. Ukombozi hata hivyo u karibu, mtaelewa tu siku sio nyingi.
 
Hata Allah pia anaswali sasa huwa najiuliza na yeye anaswali kwa nani??
Innallah wamalikatahu yuswalluuuna ala nnabiiy
Qur'an 33:56:

"Hakika Allah na Malaika wake wanamswalia (wanamtukuza, kumheshimu na kumrehemu) Mtume. Enyi mlioamini! Mswalieni naye na mumsalimu kwa salamu ya amani."

Tafsiri ya maelezo hayo:

Allah anapotajwa kuwa "anaswali" juu ya Mtume, haimaanishi kwamba anasali kama binadamu wanavyosali au kuabudu. Kwa Kiarabu, neno "ṣalāh" (صلاة) linapohusishwa na Allah linamaanisha kutoa baraka, heshima, na rehema. Si tendo la kuabudu au kuomba kwa hofu kama wanadamu.

Watafsiri wakubwa wa Kiislamu kama Ibn Kathir, Al-Tabari na hata wasomi wa Kikristo wanaojua Kiarabu wanaelewa kwamba

"Swala ya Allah" kwa Mtume ni heshima na baraka, si ibada au kujinyenyekeza kwa nguvu ya juu zaidi.

Katika Qur’an, Allah hajawahi kusujudu, kuinama au kumuomba mungu mwingine. Yeye ni wa pekee na hajahitaji kitu chochote.

Mjifunze Quran kwa kina acheni kukurupuka bila kua na elimu ya kitu.
 
Kukaa .kono wa kiume,

Ni kuonyesha mamlaka, utendaji,

SI kwamba kuna kiti kulia.

Elewa.
Amekaa mkono wa kuume, na akaambiwa kaa hadi atakapopewa mamlaka. Acha kuleta tafsiri zako mwenyewe ili kuhalalisha unachotaka tuamini.

Mie naona confusion yote inakuja kutaka kulazimisha kuwa Yesu ndio huyohuyo Mungu. Yaani Mungu kuna wakati alikufa halafu akajifufua. Na Mungu wakati akikaribia kuteswa anajiomba kikombe kimwepuke. Kama Yesu alikuwa Mungu akafa, kwa nini Shetani hakuchukua mamlaka? Na kwa nini Yesu amjibu shetani ni Mungu pekee apaswa kuabudiwa?

Tanguliza akili zako mwenyewe, badala ya yale ya kuambiwa, na utagundua Yesu na Mungu ni watu wawili tofauti. Yesu ni mwana wa Mungu sio Mungu.

Kwanza kusema Yesu ni Mungu ni sawa na kusema Shetani alimjaribu Mungu. Mungu hajaribiwi na kiumbe chochote
 
Amekaa mkono wa kuume, na akaambiwa kaa hadi atakapopewa mamlaka. Acha kuleta tafsiri zako mwenyewe ili kuhalalisha unachotaka tuamini.

Mie naona confusion yote inakuja kutaka kulazimisha kuwa Yesu ndio huyohuyo Mungu. Yaani Mungu kuna wakati alikufa halafu akajifufua. Na Mungu wakati akikaribia kuteswa anajiomba kikombe kimwepuke. Kama Yesu alikuwa Mungu akafa, kwa nini Shetani hakuchukua mamlaka? Na kwa nini Yesu amjibu shetani ni Mungu pekee apaswa kuabudiwa?

Tanguliza akili zako mwenyewe, badala ya yale ya kuambiwa, na utagundua Yesu na Mungu ni watu wawili tofauti. Yesu ni mwana wa Mongu sio Mungu.

Kwanza kusema Yesu ni Mungu ni sawa na kusema Shetani alimjaribu Mungu. Mungu hajaribiwi na kiumbe chochote
Leo umekua analytical sana ahsante kwa mchango wako nzuri, hao watu hawataki kuelewa wanajitoa akili na logic
 
Back
Top Bottom