Kauli ya kweli: Je, Mungu huomba?

Kauli ya kweli: Je, Mungu huomba?

Nimekuja kwenu leo, si kwa hasira, bali kwa msimamo wa mtu ambaye ametafuta ukweli katika Biblia na pia katika Qur’ani.

Swali hili linaibua mjadala wa kina kuhusu uungu wa Yesu kulingana na Maandiko ya Kikristo. Kama Yesu ni Mungu, basi ni kwa nani alikuwa anaomba?

Katika Biblia tunasoma: Yesu alianguka kifudifudi na kuomba katika Gethsemane (Mathayo 26:39).

Alilia na kusihi kwa machozi akimwomba Yule aliyeweza kumuokoa na mauti (Waebrania 5:7).

Alipokuwa msalabani, alipaza sauti: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?” (Mathayo 27:46).

Ikiwa Yesu ni Mungu, alikuwa anaomba kwa nani? Je, Mungu anaweza kuomba kwa Mungu mwingine? Au haya ni ishara kwamba Yesu alikuwa mtumishi wa Mungu, si Mungu Mwenyewe?

Katika Kurani Tukufu, Allah haombi, haliombi, wala hahitaji. Yeye ni Mwenye Kujitosheleza daima. Hili ni swali lenye uzito kwa waumini wa Kikristo: Kwa nini Mungu wa Biblia anaomba, wakati Mungu wa Uislamu hahitaji kuomba?

Ikiwa Yesu ni Mungu, basi alikuwa anamuomba nani? Je, Mungu anajiombea mwenyewe? Au Yesu alikuwa anaonesha kwamba yeye ni mtumishi, si Mwenyezi?

Kwa nini aseme, “Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28), na tena, “Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu” (Yohana 20:17)?

Kwa nini Paulo atangaze: “kichwa cha Kristo ni Mungu” (1 Wakorintho 11:3)?

Kauli hii inaonesha wazi kuwa Yesu Kristo yuko chini ya mamlaka ya Mungu, akimtambua Mungu kuwa juu yake — jambo ambalo lingekuwa gumu kueleweka ikiwa Yesu angekuwa Mungu.

Tanbihi

Tujikite kwenye Mada sio kutumia jaziba mihemuko chuki gadhabu matusi nk, tuko hapa kujifunza, leteni utetexi wa ushsahidi plz
UUNGU wa YESU ni siri kubwa sana ambayo ni ngumu kuielewa ukiitafakari katika hali ya kawaida, (1Timotheo 3:16) lakini pia ni miongoni mwa mambo yanayodhihirisha ukuu na uweza wa MUNGU, ni ngumu kuchunguza uwezo au akili za MUNGU (Isaya 40:28).
YESU aliomba kwa sababu alipokuja duniani alichukua mwili wa damu na nyama (Wafilipi 2:6-8)
Yote ambayo yanahojiwa kuhusu UUNGU wa YESU akiwa hapa duniani jua kwamba aliyafanya kama mwanadamu, mfano aliona njaa, alilia nk.
Ukisoma kwa tafakari ya rohoni hayo maandiko niliyokupa nina hakika utakuwa umeelewa.
 
If you can't convice them confuse them .......ndo unacho tumia mkushindwa kueleza umungu wS Yesu kawaida yenu ni kusaingizia neno ugumu au masuala ya roho.........Yesu kuja duniani alitokea wapi? Au alizaliwa tu?
 
Amekaa mkono wa kuume, na akaambiwa kaa hadi atakapopewa mamlaka. Acha kuleta tafsiri zako mwenyewe ili kuhalalisha unachotaka tuamini.

Mie naona confusion yote inakuja kutaka kulazimisha kuwa Yesu ndio huyohuyo Mungu. Yaani Mungu kuna wakati alikufa halafu akajifufua. Na Mungu wakati akikaribia kuteswa anajiomba kikombe kimwepuke. Kama Yesu alikuwa Mungu akafa, kwa nini Shetani hakuchukua mamlaka? Na kwa nini Yesu amjibu shetani ni Mungu pekee apaswa kuabudiwa?

Tanguliza akili zako mwenyewe, badala ya yale ya kuambiwa, na utagundua Yesu na Mungu ni watu wawili tofauti. Yesu ni mwana wa Mongu sio Mungu.

Kwanza kusema Yesu ni Mungu ni sawa na kusema Shetani alimjaribu Mungu. Mungu hajaribiwi na kiumbe chochote
Umenena vyema mkuu.
Kwa kuongezea kidogo naomba niseme kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, basi kama ni mwana wa Mungu basi na yeye ni Mungu.
Wakati wa ubatizo wake,
“na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye." Mathayo 3:17

Pia walipomtokea Musa na Eliya
“Alipokuwa katika kusema (na wanafunzi wake), tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. "Mathayo 17:5
Basi kama hiyo sauti ilikuwa ya Mungu baba na ikasema "msikieni yeye" , maana yake Mungu ataka tumsikie yeye na kumwamini kwa kila atakachosema.
Kwa hiyo aliposema

“Mimi na Baba tu umoja." Yohana 10:30 na
Yohana 14:7- 10 aliposema
"⁷ Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
⁸ Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
⁹ Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
¹⁰ Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake." Mungu kasema tumsikie asemacho.

Hivyo basi kwakuwa Mungu ni roho, na huyo roho alifanyika mwili, huo mwili kama wa mwanadamu mwenye sura ya Mungu baba.
Na Mungu anamshuhudia kwa kusema ni mwnangu, mpendwa wangu, tunatakiwa kutambua ya kwamba yeye ni MUNGU MWANA.
 
Mbona unajigonga gonga jitahidi uwe sitaiti:
Kilicho fufuka ni mwili au Roho?
Alivo paa ilikua roho au mwili?
Mungu as Nahitaji mwili wa binaadamu wa kazi gani?

Acha kujificha kwenye roho, roho ya binaadamu inatenganishwa na kifo tu.
Unaniuliza alifufuka mwili au Roho,NAMI nikuulize,

Mabaki ya mwili wa Yesu ya wapi?

Ndipo ujue, Ni Mungu ndiye aliyevaa mwili wa Mwanadamu akawa kama Mwanadamu wakati huo huo akiwa Mbinguni Katika utukufu akiitwa BABA.
 
Mkuu unakuepa masuali muhimu, katika maisaha ya kiroho mwili ulikua na kazi gani kupaa nao?
 
Mkuu unakuepa masuali muhimu, katika maisaha ya kiroho mwili ulikua na kazi gani kupaa nao?
Ndipo ujue aliyekuwa na mwili wa Mwanadamu ndiye huyo huyo Mungu mmoja.

Ndio maana mwili wa Yesu, mifupa wala mabaki ya fuvu yayapo popote.

Sasa usishangae akisema BABA YANGU ilhali Yeye huyo huyo ndiye BABA Katika Roho,

Unaelewa?
 
Mungu ana mwili wa binaadamu nasomba jibu?
 
YESU ni mwana WA MUNGU Kwa hio uungu wake ni Kwa sababu ya asili ya Baba yake.Kwa kuwa Baba yake ni MUNGU na yeye ni MUNGU asilimia Mia.Ila nafasi yake ni mwana.Mkuu kushinda yeye ni Baba alieumba vitu vyote
 
YESU ni mwana WA MUNGU Kwa hio Mungu wake ni Kwa sababu ya ajili ya Baba yake.Kwa kuwa Baba yake ni MUNGU na yeye ni MUNGU asilimia Mia.Ila nafasi yake ni mwana.Mkuu kushinda yeye ni Baba alieumba vitu vyote
Mkuu wewe umekua muwazi kuliko wengine kwa kauli hiyo Yesu na Baba yake wote ni Mungu au sio? Nirekebishe kama nimekosea.
 
Amekaa mkono wa kuume, na akaambiwa kaa hadi atakapopewa mamlaka. Acha kuleta tafsiri zako mwenyewe ili kuhalalisha unachotaka tuamini.

Mie naona confusion yote inakuja kutaka kulazimisha kuwa Yesu ndio huyohuyo Mungu. Yaani Mungu kuna wakati alikufa halafu akajifufua. Na Mungu wakati akikaribia kuteswa anajiomba kikombe kimwepuke. Kama Yesu alikuwa Mungu akafa, kwa nini Shetani hakuchukua mamlaka? Na kwa nini Yesu amjibu shetani ni Mungu pekee apaswa kuabudiwa?

Tanguliza akili zako mwenyewe, badala ya yale ya kuambiwa, na utagundua Yesu na Mungu ni watu wawili tofauti. Yesu ni mwana wa Mongu sio Mungu.

Kwanza kusema Yesu ni Mungu ni sawa na kusema Shetani alimjaribu Mungu. Mungu hajaribiwi na kiumbe chochote
Ndio,

Shetani alimjaribu Mungu Katika mwili wa Mwanadamu,

Rejea majibu ya YESU akimjibu shetani, alimwambia,

"Imeandikwa, Usimjaribu BWANA Mungu wako".

Sasa shetani amjaribu Yesu, Yesu amjibu, Mungu hajaribiwi.

Bado hujui Yesu ndiye Mungu?

Mungu ni mmoja tu,

Ndiye huyo Mungu Baba aketiye kitini pa Enzi,

Ndiye huyo huyo Mungu mwana.

Ndiye huyo huyo Mungu Roho mtakatifu.

Ni kama tu WEWE, Ukiwa job unaitwa Mwajiriwa, ukiwa nyumbani waitwa baba, ukiwa safarini waitwa msafiri lakini ni WEWE yule yule mtu mmoja.

Sasa tofauti yako WEWE mtu na Mungu / Yesu, Yeye aweza kuwapo Mbinguni kitini pa Enzi wakati huo huo akawapo duniani amevaa mwili wa Mwanadamu wakati mmoja.

Mungu ni mmoja tu, hakuna Mungu wawili au watatu!

Sijui unaelewa?
 
Huwezi kuupata ukweli wa Biblia kwenye Quran, ila unaweza kuupata ukweli wa Quran kwenye Biblia.

Kama unataka kumjua Yesu ni nañi Biblia Ina majibu yote, ila Muombe Roho wa Mungu akusaidie kukufunulis Siri zilizofichwa na kukusaidia kuelewa kabla hujaanza kusoma, hufanyi hivyo unataka kusoma tu kama unavyosoma Kitabu Cha Willy Gamba, then ungeendelea tu kusoma Quran.
 
YESU ni mwana WA MUNGU Kwa hio uungu wake ni Kwa sababu ya asili ya Baba yake.Kwa kuwa Baba yake ni MUNGU na yeye ni MUNGU asilimia Mia.Ila nafasi yake ni mwana.Mkuu kushinda yeye ni Baba alieumba vitu vyote
Mungu ni mmoja tu.

Akiwa kitini pa Enzi anaitwa Baba,

Akiwa Katika kazi ya ukombozi, kazini, hujifunua kama Mungu mwana, au Neno,

Akiwa ndani ya wanadamu wamwaminio aitwa Mungu Roho mtakatifu,

Mungu anabaki kuwa mmoja,sababu Yeye ni Mungu, hana limit Katika utendaji kazi wake.
 
Mungu ana mwili wa binaadamu nasomba jibu?
Na tuumbe mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu.

Hujui mtu ni mfano wa Mungu,

Hujui kuwa Mungu ana macho, masikio, mikono, miguu nk nk?

Husomi maandiko kuwa Yeye aketiye kiti Cha Enzi mbinguni, ana mikono na mikono yake ina matundu ya misumari?

Mungu ni mmoja tu.

Ndiye Yesu.

Ngoja nikutag kwenye Uzi ulioelezea Mungu alionekana kama mtu mbinguni.
 
Mungu ni mmoja tu.

Hakuna Mungu wawili.
Naelewa Wewe unaelewa vizuri.. Level yako ni TOFAUTI na watu WA mataifa..Kuna level ya kumuelewesha mtu stage flani ya uungu na akaelewa kirahisi..Take into account ni Nani unaemuelewesha.
 
Naelewa Wewe unaelewa vizuri.. Level yako ni TOFAUTI na watu WA mataifa..Kuna level ya kumuelewesha mtu stage flani ya uungu na akaelewa kirahisi..Take into account ni Nani unaemuelewesha.
Ukimwelewesha kama ulivyomuelewesha atakuuliza kuna Mungu wangapi, utakosa JIBU.

Biblia Iko wazi Mungu ni mmoja nafsi moja tu.

Yesu ndiye huyo huyo Mungu mmoja aliyevaa mwili na kuonekana kama Mwanadamu, lakini Roho yake ni Mungu.
 
Back
Top Bottom