Kauli ya Jana Morogoro naomba ufafanuzi

Kauli ya Jana Morogoro naomba ufafanuzi

Mkombozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2008
Posts
844
Reaction score
477
Hii nchi tumeitoa mbali na kuifikisha hapa ilipo,namwamini sana kijana wetu hata akichukua nchi,mie nitalala usingizi.Mgombea anapanda juukwaani na amekuwa akitamka mara kadhaa walitufikisha hapa ni mafisadi na atambambana nao kwa kujenga jela,yaani kazi tu.Naomba kueleweshwa wakuu
 
Hawezi kupambana na ufisadi maana anaogelea mlemle.Mwenzie JK alianzia Ngurudoto kwa semina nyingi elekezi zikiwa na lengo la kuleta "maisha bora" lakini tumeambulia bora maisha.Watanzania tuna hitaji MABADILIKO
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.
 
Wanajichanganya sana na kauli zao,bila kujua wanapigana madongo wao kwa wao kifupi hawaeliwi ni kipi waongee na mahali gani
 
Maana yake Magufuli atawashughulikia mafisadi. Haijalishi ni nani bt wote watashughulikiwa.
 
Hivi inamana jk na huyo makufuli pamoja na tim yao wametuona sisi ni malofa na wajinga kiasi gani?hvi hatakama sisi ni malofa hatuna akili hata za kufikiri vitu vidogo kama hivi na kupata majibu?kwa mfano makufuli akajenga kweli hizo jela za mafisadi alafu aanze kuchunguzwa mojamoja ndani ya ccm na viongozi wake nani atabaki salama?si mwisho na yeye atakua mfungwa?hivi nikweli anaweza kuwafunga maboss wake wanaompa chapuo?
 
Maana yake Magufuli atawashughulikia mafisadi. Haijalishi ni nani bt wote watashughulikiwa.

hata jk alitoa ahadi za kufanana na hizo alipopewa kijiti na mkapa akasema anaenda kuvunja mikataba hewa yote na bahati mbaya mingi aliitaja.lakin matokeo tumeyaona ndo kaongea balaa zaidi.hadanganyiki mtu awamu hii
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.

Mşomi hata wa la saba ataelewa.Ni hv,kuna maeneo tena mengi tu ambayo taifa limepga hatua kubwa, mfano swala la umoja na mshikamano.Kuna maeneo tumedorola sana mf,mapambano dhidi ya mafisadı na ufışadi na umasikini wa kipato kwa individuals.
 
Ccm mambo yamekua magumu sana,ni wazi wanakosa sera za kutuambia,chama kikishakua na uswahili uswahili ndo matokeo yake,
 
tena ni watoto mmoja aliyefariki ana miaka 12 maskini alienda kuona wasanii
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.

Jamani msiogope. Hayo ndio maneno murua kabisa. Hakuna mwenye kosa hapo. Kule Moshi, Kinana katibu mkuu wa chama chetu kitukufu kesha fafanua vizuri kasema; CCM imejaa Majambazi, Wezi, Wanafiki na kiila aina ya uozo. Sasa kama kawaona, na M/kiti naye kawaona, na rais mtarajiwa kayaona, ndo maana kasema atajenga jela, wajipeleke huko wenyewe. Uchaguzi mkuu utafanyika ghafla tena majela hayo yakiwa tiyari kwani miaka yoote hayo majizi ndio yaliongoza. Haya ni maneno ya rais sio yangu jamani. Nimejaribu tuu kufafanua vile nlivyo elewa
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.

Ni utovu wa 'nidhamu' kuwaacha watu wenye fikra kama hizi kutuongoza !
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.

utaelewa tu. anayeomba uraisi ni magufuli. hivyo kauli zake ndizo za kuzingatiwa kuliko yeyote.
 
Kaka ccm kwa sasa ni kama MNARA WA BABELI.....KILA MTU AMEKUWA NA LUGHA TOFAUTI ZINAZOWAFUNGA WAO KWA WAO
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.

huelewi wakat katutoa kwenye mdomo wa mamba Lowassa na kakubali kuvunja urafiki nae ili kutuokoa na Fisad mkubwa huyo
 
Duh kumbe kikwete anajua kuwa atafungwa kwa ufisadi alioufanya yeye na mtoto wake ..tumuweke lowasa ili tujue madhambi ya huyu jamaa
 
Kwanini sijasikia tena MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?Natamani kusikia tena hiyo phrase kwenye kampeni,
 
amini usiamini kama wakufungwa basi alikuwa ni lowasa. Kikwete kamvumilia sana kwa sababu ya uswahiba wake. pamoja na kutofautiana kwenye siasa na kutia doa kwenye uongozi wake kwa kuliingiza taifa kwenye kashfa ya richmond bado amemvumilia kwa sababu ya uswahiba wake.
wasikilizi akina Dr. Mwakyembe, Dr. Slaa. Prof. Lipumba, H. Polepole, Mh. Sita, Akina butiku na wengine utanielewa nasema nini. hata hivyo uwezo wa lowasa kuongoza nchi hii haupo kwa hali ninayoiona.

Anaogopa kufungwa ndo maana anasema akistaafu na makufuli akapewa nchi atapata usingizi,kwa kuwa atalidwa,lkn akija mamvi atakua macho segerea.
 
Back
Top Bottom