Uchaguzi 2020 Kauli ya Jaji Kaijage na yanayopangwa kufanywa na NEC kwa wagombea Urais

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Kauli iliyotolewa jana na Jaji Kaijage ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuvitaka vyama kuteua Wagombea makini ili baadaye Tume isilaumiwe siyo ya bahati mbaya.

Taarifa za uhakika nilizopata toka ndani ya NEC ni kuwaengua Lissu na Membe kwa technicalities. CHADEMA NA ACT Wazalendo waangalie hizo technicalities mapema wajiandae kisaikolojia.

Uongozi wa juu uliopo hautaki kabisa kampeni hasa kwenye nafasi ya juu ya uongozi. Wangependa kubaki na akina shibuda na lipumba ili kampeni zisiwe na msisimko.

Lissu ana hoja ya maadili ya kuvuliwa ubunge, Nyalandu na Membe wana hoja za kufukuzwa uanachama wa chama chao. Wanasheria wanahaha kutafsiri hoja hizo katika misingi ya kikatiba ili kuwaengua ulingoni na malaika mkuu apite kimya.

Tahadhari kubwa ifanyike na sauti zipazwe.
 
Kama haya ni ya kweli, hivi hii tume ni kuengua au kusimamia uchaguzi? Wanataka kuwa chanzo cha machafuko huko mbeleni maana vijana wa 1980 kwao jambo la kuchomoa betri ni rahisi sana.

Mataifa ya nje sijui yanaionaje nchi yetu na democrasia ya kuengua watu.

Chondechonde tume, msigeuke kuwa mahakama na kuanza kutafsiri sheria... kuwa na mkuu wenu ex judge hakuwapi legitimacy ya kuchukua nafasi ya mahakama...acheni.

inajulikana wazi huko chato, JPM tangu akiwa mbuge anapenda sana hizi mambo za kupita bila kupingwa... kuwatoa watu kwa technicalities..ifike mwisho sasa.

Ingefaa pia kuwepo na mapingamizi ya wanaoanza kampeni kabla ya Muda au kuwachafuwa wabunge... mf chagueni ccm Iwaletee maendeleo... tume kuweni fair play tafadharini sana.
 
Mnajitekenya wenywewe na kucheka wenyewe
Mnajidanganya wenyewe na kujijibu wenywe sio
 
Kama haya ni ya kweli, hivi hii tume ni kuengua au kusimamia uchaguzi? Wanataka kuwa chanzo cha machafuko huko mbeleni maana vijana wa 1980 kwao jambo la kuchomoa betri ni rahisi sana...
Mataifa ya nje sijui yanaionaje nchi yetu na democrasia ya kuengua watu...
Chondechonde tume, msigeuke kuwa mahakama na kuanza kutafsiri sheria... kuwa na mkuu wenu ex judge hakuwapi legitimacy ya kuchukua nafasi ya mahakama...acheni...

inajulikana wazi huko chato, JPM tangu akiwa mbuge anapenda sana hizi mambo za kupita bila kupingwa... kuwatoa watu kwa technicalities..ifike mwisho sasa...

Ingefaa pia kuwepo na mapingamizi ya wanaoanza kampeni kabla ya Muda au kuwachafuwa wabunge... mf chagueni ccm Iwaletee maendeleo... tume kuweni fair play tafadharini sana ...
Uraisi siyo ubunge. One mistake you perish. Watu kama Nyalandu na Lisu hawawezi kuvaa viatu vya Uraisi hata wakipata kura 100%
Hawana sifa kuu zifuatazo
1. Uzalendo (wanajiuza kwa maadui wa nchi mfano MIGA etc)
2. Misimamo ( wepesi kununulika na kuhamishwa )
3. Wasaliti wa maadili na mila za mtanzania (mfano Ushoga)
4. Hawana economic plan zaidi ya kujaza watu huruma
5. Record zao ni mbaya.
6. Maadili ya kiongozi mkuu( Raisi was nchi ) wamepishana nayo.
 
Uraisi siyo ubunge. One mistake you perish. Watu kama Nyalandu na Lisu hawawezi kuvaa viatu vya Uraisi hata wakipata kura 100%
Hawana sifa kuu zifuatazo
1. Uzalendo (wanajiuza kwa maadui wa nchi mfano MIGA etc)
2. Misimamo ( wepesi kununulika na kuhamishwa )
3. Wasaliti wa maadili na mila za mtanzania (mfano Ushoga)
4. Hawana economic plan zaidi ya kujaza watu huruma
5. Record zao ni mbaya.
Tupe sifa za Mafgufuli Kikwete,Mkapa ilo tuweze kulinganisha
 
Uraisi siyo ubunge. One mistake you perish. Watu kama Nyalandu na Lisu hawawezi kuvaa viatu vya Uraisi hata wakipata kura 100%
Hawana sifa kuu zifuatazo
1. Uzalendo (wanajiuza kwa maadui wa nchi mfano MIGA etc)
2. Misimamo ( wepesi kununulika na kuhamishwa )
3. Wasaliti wa maadili na mila za mtanzania (mfano Ushoga)
4. Hawana economic plan zaidi ya kujaza watu huruma
5. Record zao ni mbaya.

Hoja zako ni zakitoto kabisa. Yupi pale ccm ni mzalendo? Yupi pale ccm ana economic plan? Yupi hana record chafu pale ccm?. Acha ushabiki usiokuwa na maana. Wananchi ndio wanajua yupi anastahili kuchaguliwa
 
Back
Top Bottom