Kauli ya Chagonja juu ya Nassari

chagonja hajawahi kuongea kauli nzuri kuhusu wapinzani hivyo kwa kauli kama hii siwezi kumshangaa sana, suala la nassari kupigwa zilikuwa mbinu chafu za viongozi wa ccm waliochukizwa na kitendo chake cha kupita kwenye vitu vya kura na kuangalia zoezi linakwendaje na kama mawakala wa chama wote wamefika,
 
Ndio maana tunahitaji system overhaul, ni ngumu kuingia akilini kwa mtu yeyote kwamba kiongozi wa nagzi ya juu kama huyu anatoa kauli ambayo hakuipima, na yenye kumuaibisha hata yeye mwenyewe namna hii. Kuongea kunahitaji weledi na ubunifu wa hali ya juu na kupima madhara ya kile unachosema. Tunahitaji kujenga uwezo wa watawala wetu kama hawafundishiki..........
 
Sasa tunaweza kupata majibu ya mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa kwenye mikutano ya Soweto kuwa yaliwalenga kina Mbowe na wabunge wengine ambao si wa arusha.
 
Viongozi wengi wa polisi ni wale wa enzi ya chama kimoja hivyo tunachokiona sasa ni matokeo ya polisi kuwajibika kwa chama na sio kwa wananchi na sheria ya nchi.

Mungu tusaidie ili wajue mchango wao katika ustawi wa nchi yetu Tanzania
 
Duuh! Kwa hiyo ni sahihi kwa Nassari kupigwa kwa sababu alienda sehemu ambayo sio kwao. Ni maajabu ya dunia kuwa na kiongozi wa Upelelezi wa aina hii.
 

unawza ukawa rais ukakosa hekima

ukawa mkuu wa polisi ukakosa busara

ukawa na cheo cha juu sana kwenye nyanja ya uongozi ukakosa matumizi mazuri ya ulimi..


swalil kwa CHAGONJA ...Kuwa kiongozi KWENYE jamii kuna mipaka..,huko ARUSHA NI KWAKO CHAGONJA???


HIZ POMBE ZA ASUBHI ZINA TAABU KWELI.!!!!!!!!
 

Mtu anapofikiri kuwa walioko kwenye serikali hii wameshafika kwenye kilele cha kufanya ujinga wao wanavunja rekodi yao wenyewe kwa kufanya ujinga mwingine ambao mtu usingeweza kufikiria mtu mzima - tena mwenye dhamana ya kuongoza nchi - atafikiria kuufanya achilia mbali kuufanya! BWANA Mungu tuokoe wanao maana tunaangamia sasa!
 

Ndo upeo wake, so usishangae
 
hawa ndio aina ya watu tulionao kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na serikalini
 
Viongozi wengi wa polisi waliajiriwa zamani kidogo.Na kigezo cha kujiunga na polisi ni kutumia miguvu kuliko akili.Na ndo maana mtu athubutu kusema namba za bomu ziliwekwa ktk "google earth" wakatambua limetengenezwa China. Kazi ipo kwa polisi wadogo..
 

Kwa kauli hiyo na kama nchi ingekuwa inaongozwa kwa kuzingatia utawala wa sheria na haki, leo angerudi nyumbani na barua ya kustaafishwa ama kufukuzwa kazi kwa manufaa ya umma.

Lakini kwa kuwa tuna serikali inayolinda na kutetea wezi, mafisadi na viongozi wasiokuwa na uadilifu na kuzingatia sharia, sio ajabu kesho ukasikia rais amemtunuku nishani na kumpandisha cheo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…