Kauli tata Mei Mosi 2019

Kauli tata Mei Mosi 2019

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,718
Reaction score
830,771
Kama kuna mtu unapaswa kuwa makini naye sana... I mean kwa asilimia 100 basi ni mtu mwenye kuitwa Mwanasiasa... Ichunge sana kauli yake kwakuwa huitamka akiacha utata ama nafasi ya utetezi
Ndio maana kuna utani unasema Mwanasiasa akikwambia kumepambazuka usimwamini mpaka utoke nje ujiridhishe mwenyewe.... Tafsiri yake ninini hapa!? MWANASIASA HAAMINIKI...
Ishu ya kupandishwa madaraja na kuongezewa mishahara ilikuwa ni ahadi ya Mei Mosi 2018.... Subiri yavuta kheri... Lakini sometimes huja kinyume.... Kilichotarajiwa na wengi kimekuja tofauti kabisa... Picha zijazo zinajieleza
Lakini kwa umakini mkubwa kabisa imetoka kauli nyingine tata kuwa alisema ataongeza kabla hajatoka madarakani.... Ametaja mwaka wa kutoka madarakani?
Jifunze kusoma lugha za kisiasa... Utaishi maisha mengi
IMG-20190501-WA0219.jpeg
IMG-20190501-WA0218.jpeg
 
Huyo Mkuu hajawahi kuwa amini au hata kuwa na upendo na wafanyakazi.
Ni mnafki wa daraja la kwanza.

Pesa ya kufanya yote yanayo tibu kiu yake anayo lakini sio kulipa jasho la wavuja jasho. Unawaambia watu umeokoa mabilion ya wafanyakazi hewa, lete alone hizo za ambao wamepungukiwa s-fa (which was stupid nonsense), hayo mabilioni yameenda wapi?

Broods of the great liar.
 
Wafanyakazi utadhani wako msibani
Lazima wawe kwenye hali hiyo,maana wafanyakazi Leo walikuwa wana msikiliza Mh lakini walikuwa tayar kwa lolote yani ni kama mashabiki Wa Man U walipokuwa wanatizama mechi kati yao na Barcelona....
 
Halafu utashangaa wale makada wa tucta mwakani watamualika tena ili aendelee na ngonjera zake za miaka minne sasa! Ila tuongee tu ukweli, hotuba za mzee zinachosa sana maana hazivutii na mara nyingi zinatabirika. Leo amejifunza kitu kwa wafanyakazi bila shaka! Hawakuficha kabisa hisia zao pale uwanjani.
 
Jiwe mjanja amebana hivyo ili mwakani awapandishie wote wajisahau awaombe tena kura/kula zao na akipita anasgusha tena nyie mnamjua au mnamsikia
Mwakani kila kitu ni bwerere ili aanze kukusanya point za kuomba tena kura nabwatanzania walivyo wepesi wa kusahau na kura ataouta tena kwa ushindi wa ajabu
 
Sio hivyo tu,hata kakwepa kuahidi kuwa ataongeza mishahara mwakani na ni wazi hana uhakika kuwa hali itaruhusu kuongeza mishahara akaishia kutoa kauli/tungo tata kuwa ataongeza kabla hajatoka madarakani na wala msitarajien kuna siku watakuja na min budget ya kuongeza mishahara.

Huyu bwana ameshafeli na bado mtaona mengi siku zijazo(kajitishwa mzigo asiouweza na sasa umeanza kumuelemea na kuna siku atautua kwa aibu).
 
Mh ni jasiri muongoza njia ambaye pia ni kauzu sana.Kwa hii njia anayotupitisha tutaona matunda yake mbeleni tusimkwamishe.kuhusu uchaguzi ujao naona kama hakutokuwa na uchaguzi kwa vile upinzani ushapotezwa na hauna agenda yenye mshiko.Nina maanisha hata wakilibeba hili wananchi wana matumaini na mwenye nchi.
 
Back
Top Bottom