Kauli nyingine tata ya Kikwete hii hapa

Hua najiuliza mara nyingi,hivi raisi wetu hana washauri? Kwasababu kauli anazotoa zina mengi ya kujiuliza.Sina haja ya kuzirudia kwa vile kama mtu ni mfuatiliaji wa mambo ya nchi yetu vizuri,lazima atakuwa anakumbuka angalau kauli tata chache hivi.

Hii ya leo ni ile aliyotoa kule Babati jana.Katika hali ya kushangaza, Rais alisema wale wasichana wenye sifa za kwenda ualimu wamfuate Ikulu.Sasa mimi najiuliza Ikulu pamekuwa Kariakoo kiasi kwamba kila mtu anaweza kwenda?

Na kama basi ameruhusu waalimu watarajiwa waende Ikulu,kwa nini mabwana shamba watarajiwa,wafanyakazi mbalimbali wa afya nao wasimfute Ikulu?Na katika hali hiyo, Rais amesahau 'protocal' ya ajira?

Ninachojua mimi kila wizara ina ajiri watu wake,sasa tangu lini Rais akawa afisa mwajiri?Chonde chonde jamani,ninaomba wasaidizi wa Rais wafanye kazi zao inavyo paswa, kwa maana kwamba wamshauri vizuri Rais wetu.

Mkome kuchagua waswahili kuwa marais
 
Mwache awamege cha mwishomwisho

Back
Top Bottom