Kauli nyingine tata ya Kikwete hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli nyingine tata ya Kikwete hii hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 16, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hua najiuliza mara nyingi,hivi raisi wetu hana washauri? Kwasababu kauli anazotoa zina mengi ya kujiuliza.Sina haja ya kuzirudia kwa vile kama mtu ni mfuatiliaji wa mambo ya nchi yetu vizuri,lazima atakuwa anakumbuka angalau kauli tata chache hivi.

  Hii ya leo ni ile aliyotoa kule Babati jana.Katika hali ya kushangaza, Rais alisema wale wasichana wenye sifa za kwenda ualimu wamfuate Ikulu.Sasa mimi najiuliza Ikulu pamekuwa Kariakoo kiasi kwamba kila mtu anaweza kwenda?

  Na kama basi ameruhusu waalimu watarajiwa waende Ikulu,kwa nini mabwana shamba watarajiwa,wafanyakazi mbalimbali wa afya nao wasimfute Ikulu?Na katika hali hiyo, Rais amesahau 'protocal' ya ajira?

  Ninachojua mimi kila wizara ina ajiri watu wake,sasa tangu lini Rais akawa afisa mwajiri?Chonde chonde jamani,ninaomba wasaidizi wa Rais wafanye kazi zao inavyo paswa, kwa maana kwamba wamshauri vizuri Rais wetu.
   
 2. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii wala sio washauri tena ni mazezeta yake tu hayo!
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Nashukuru kwa bandiko lako, ni zuri sana isipokua jinsi ulivyomalizia.
  Hapo natofautiana na mtazamo wako. Kwa nini udhani wa kunyooshewa kidole ni washauri/wasaidizi wake?

  .
   
 4. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Yakweli haya au tetesi wajameni mimi mbona naona kama haikuji vile.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lazydog,

  Yani hilo ni moja ya tatizo la msingi, moja ya kubwa kuliko yote la wananchi wetu inapokuja kwenye kuchambua viongozi na matatizo yao. Rais anatoa hotuba anajichemshia mwenyewe jukwaani halafu tunasema hana washauri wazuri. Hapo tu ndio nachoka akili.

  Juzi bungeni kaongeza chumvi zake - na Kikwete anajulikana kwa kupenda chumvi - kaongea tofauti na alivyotaarishiwa, kadai akitaka anaweza kukamata mtu yeyote bila sababu, alipokuwa anawahutubia mainjinia kawambia "acheni ujanja ujanja," kana kwamba mainjinia wote ni wasanii, alipokuwa Ikulu Washington akatamka kwenye press conference eti amekuja Amerika kutoa shukurani, aliposhindwa kuvuka daraja Kusini huko akadai hajui kuogelea, kana kwamba kuna mtu alimtayarishia mtumbwi, kuhusu michezo akadai kazi amekamilisha na siku hizi sisi ndio tumekuwa vinyozi, eti nchi nyingine zikiwa na ratiba ya kucheza na Stars wanajiuma uma.

  Uongo mtupu.

  Halafu eti oooh, washauri wake. Kwa mtaji wa washauri basi unaweza kutetea kila kitu Rais anachofanya. Tukimlaumu kwa kuteua washauri wabaya utasema kashauriwa vibaya katika kuteua hao washauri. Na nani? Nani alimshauri katika kuchagua wale washauri waliomletea majina ya washauri waliopendekeza wale washauri walio end up kuwa washauri wa Ikulu?

  Ni kisingizio!
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mpaka leo hii hamjamzoea JK ana katabia kaa kuongea mabo jinsi anavyojisikia na ndo tabia yake.
  Na ukichukulia yeye na hao anaotaka waende ikulu damu damu basi mambo mstari.
  Apo ni tabia binafsi utamshauri nini kuna vijineneo ambavyo ni nje ya speech aliyoandaliwa huwa anavitoa tuu kimtindo.
  Tumvumilie labda 2010 atastep down tupate mwingine maanani akipenda
   
 7. M

  Mwanangurumo Member

  #7
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii imenikumbusha Kipindi nafanya kazi kule Ngara kwa wakimbizi nilikutana na mmarekani mmoja akisema hivi ( You know you Tanzanian you are very wonderful people in this world. I asked him why yuo say so. He replyed! How did you manage to stay ten years without a prestent!! Brothers we do not have a presdent, kikwete can not presdent at all
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Pals!Read between lines!Hamjamwelewa?Amesema WASICHANA maana yake yeye hao alionao hawamtoshi kabisa ndio maana anajua kule Babati kuna weupe wakuvutia!
   
 9. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...anataka kumuiga King Mswati nini???!!!!!!
   
 10. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Hivi ni mkwere au mkware...?
   
 11. M

  Mimich Member

  #11
  Mar 13, 2015
  Joined: Feb 10, 2015
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna hadithi fulani ya mfalme **** sijui ndo inafanana na hii??.. Ebu fungukeni wanajamvi..
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2015
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kichwa nazi! !
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2015
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Ni kwa sababu tatizo la kwanza limeshaeleweka na sasa tumaini la wafuatiliaji wa mambo ni plan B.
  Lakini kama mfano akina Gurumo kwao 80m hawajui hata kama zimeingia kwenye account zao, unadhani watapata muda wa kumshauri rais badala ya kusimamia miradi yao inayoingiza mabilioni!?

   
 14. m

  mashingia kuute Member

  #14
  Mar 14, 2015
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anatafuta mchumba labda ndo maana anawaita wasichana ikulu. Kwani hakuma wavulana waalimu wanaotafuta kazi?
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2015
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Natamani awasimulie wanangu hadithi maana najua kamwe hawatasinzia... Hata hivyo ameshasema anataka kwenda kulea wajukuu kule kwenye Kijiji chake
   
 16. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  ...gurumo the advicer!
   
 17. black sniper

  black sniper JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2015
  Joined: Dec 10, 2013
  Messages: 5,818
  Likes Received: 2,479
  Trophy Points: 280
  TOBAAA ulipataje kazi kwa lugha hii
   
 18. Mgoroko

  Mgoroko JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2015
  Joined: Mar 12, 2014
  Messages: 460
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Raisi kikwete kafanya mambo mengi mazuri sana,hata wewe kuwa na uhuru wa kuhoji huu utumbo wako ni moja ya mambo makubwa aliyo fanya raisi kikwete kukupa uhuru wa kutumia teknolojia.
   
 19. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2015
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  W ewe unashangaa nini hapo? Mbona nyerere alimkalisha kiti moto Paul kimiti pale Dodoma ili ajieleze kwake hela alizojengea nyumba ake pae doma alizipata wapi. Kaa io alikkera wewe basi hata hili la kikwte pia lione kama kawaida ville iwejeraisi wa nchi ahoji watu pesa zao za kujenmea walipata wai ili hal;i kuna vyombo vya usalama?
   
 20. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2015
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Mshauri mwenyewe Gurumo....Mmmmhhh
   
Loading...