Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Ni ukweli uliowazi Sasa kwamba mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ni kama amewameza wagombea wenzake na hawasikiki tena.

Tangu ateuliwe na chama chake CHADEMA na kisha kuchukua fomu za kuteuliwa kutoka tume ya uchaguzi NEC Lissu amekuwa gumzo kila kona huku akijadiliwa zaidi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Lissu amekuwa akifanya ziara mikoa mbalimbali ya kusaka wadhamini huku akilakiwa na Maelfu kwa maelfu kokote anakopita.

Mojawapo ya sababu kubwa ya kupata uungwaji mkono huo kutoka kwa wananchi hasa waliohojiwa kila anakopita ni kauli Mbiu yake ya 'Uhuru na Kazi' akimaanisha pamoja na kutakuwa kufanya kazi lakini katika serikali yake wananchi watakuwa huru hasa katika kufanya siasa, kupata habari mbalimbali bila ubaguzi, vyombo vya Habari kuwa huru bila kufungiwa hovyo, waandishi wa habari kutokunyanyaswa na watu kuwa huru kukosoa serikali yao bila kuogopa kukamatwa na kufungiwa.

Pia Lissu amekuwa akijinasibu katika serikali yake ni mwiko kuingilia Bunge na mahakama bali kuiacha mihimili hiyo kuwa huru katika maamuzi yake. Pia wananchi kuwa huru kuangalia LIVE Bunge lao.

Mgombea huyo wa Chadema anasema kutaka watu wafanye kazi tu huku ukiwanyima Uhuru wao ni dhambi kubwa ambayo kamwe serikali yake haitafanya.
Lissu anajua watanzania wanataka nini. Swala la Uhuru kila mtanzania analitaka. Mambo ta chakula sijui na madaraja kila mtu atatafuta. Kwani kodi ni za wananchi.
 
Nani kama Tundu Lissu, cheki alivyovuta nyoyo za waTanzania kudai uhuru katika kazi zao za ukulima, uvuvi, ufugaji , biashara na haki ya mlipa-kodi kupata Uhuru ndani ya Maendeleo yake ktk kila kona ya nchi

Raia wema wakimsubiri Rais wao.
 
Nani kama Tundu Lissu, cheki alivyovuta nyoyo za waTanzania kudai uhuru katika kazi zao za ukulima, uvuvi, ufugaji , biashara na haki ya mlipa-kodi kupata Uhuru ndani ya Maendeleo yake ktk kila kona ya nchi

Utadhani ni Yesu ameingia Yerusalem.
 
Uhuru upi?

Hivi mwananchi wa nanjilinji kule ukiongelea juu ya uhuru si anakushangaa?

Hilo la uhuru atawapata viongozi wenzie wa pale ufipa

Mkuu ukumbuke hao waliopigwa korosho zao ni wakijijini.
 
Hiyo kauli mbiu ndio inayofanyika sasa..mwambieni abadili kauli mbiu..

Watu wanafanya kazi kwa uhuru. Machinga, mamalishe wamejazana mabarabarani.

Watu wa mpesa, tigo pesa na wengine wanafanya kazi bila kuhofia majambazi kama zamani.

Bodaboda wapo huru, hakuna kukamatwa wala kutekwa na kuuawa kama zamani.

Mwenye hofu kwa sasa ni mwanasiasa mwenye kauli na lugha kali na chafu.

Labda angeita siasa na uhuru..kwamba akishinda atawaachia wanasiasa uhuru wa kutukana watakavyo na kutunga uongo wapendavyo. Pia ruksa kutumia lugha zenye ukakasi mfano kusema rais tundu lissu anaisaidia uganda kupambana na rwanda, au rais tundulissu amlala mke wa mnyika, au mbowe afyeka mbuga ya serengeti kujenga hotel ya kisasa, au lema waziri wa utalii atumia ndege za serikali kufanyia biashara zake za utalii. Waziri mkuu Mbowe amteua joyce mukya kuwa naibu gavana bot.
 
Upinzani imara unaifanya Serikali iliyoko madarakani kutokuwa lege lege ( By Mwalimu Nyerere).

Serikali iliyoko madarakani inafanya jambo jema sana kutokumbughudhi Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini.

Si lazima Tundu Lissu awe Rais wa Inchi ila muhimu ni yeye kuleta Uhai wa Demokrasia bila kuvunja upendo na Amani ya Inchi.

Misahafu Takatifu inasisitiza sana Amani na upendo kuliko utajiri .
Utajiri, madaraka nk. vyote vitapita lakini kiongozi anayedumisha amani na upendo jina lake halitapita kamwe..

Hata watu wako wakiwa maskini lakini wako huru na wana furaha ni bora kuliko kitu chochote.

Yesu Kristo aliweza kugeuza mikate 5 na Samaki wawili kutosha kuwalisha watu 5000 na kubaki vikapu 12.

Yesu Kristo hakuwahi kumiliki nyumba, shamba au mifugo. Hata yule punda aliyempanda wakati anaenda kuteswa hakuwa wa kwake. Sisi waumini tunajua alikoteswa na kuuwawa Yesu Kristo. Sisi waumini tunajua mahali alipozikwa Yesu Kristo.

Hadi Sasa Yesu Kristo anakumbukwa kuliko kitu chochote Duniani bila kujali imani ya mtu.
Tusitangulize sana ustawi wa uchumi ila amani,
upendo na uhuru.
 
Lisu anaweza kuwa Raisi wa nchi hii, kama magufuli alipewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom