Kauli isiyo ya kidemokrasia ya Obama!

Kauli isiyo ya kidemokrasia ya Obama!

...will never be... vs ... ...will not be...
Wajuvi wa kudhungu mtujuze!!!
 
Ana haki ya kusema ni Democratic Na Trump ni Republican. Keshaona tishio la chama cha Republican kushika dola via Trump. Ni mambo ya upinzani angekuwa Republican anamshambulia mwenzie ingeshangaza.

Ndio ilivyo ktk siasa za kimarekani.
 
Hiyo si Tanzania. Obama ni nani? anaweza kusema chochote na Trump akachaguliwa. Ingekuwa Tanzania ningeamini.
 
Alikuwa akitoa maoni yake binafsi kujibu swali la Mwandishi.

Kule sio TZ ambapo kila anachosema Rais ndo kinakuwa sheria pale pale.
aligoe na bush ;
ulikuwa ujazaliwa nn
 
Trump ni headache hata kwa NRC waliomkubalia ajitose kugombea uteuzi kupitia Republican. Ulaya usideme, hawataki kusikia jina lake! Kawachefua Waislamu hata waliomo Marekani. Tatizo mdomo wake hauna speed limit.
 
Trump ni headache hata kwa NRC waliomkubalie aingie katika kinyanyanganyiro cha uteuzi kupitia Republican. Ulaya hataki akanyage kwao. Amewachefua Waislamu karibu dunia nzima.Tatizo, Trump mdomo wake hauna speed limit!
 
Trump ni headache hata kwa NRC waliomkubalia ajitose kugombea uteuzi kupitia Republican. Ulaya usideme, hawataki kusikia jina lake! Kawachefua Waislamu hata waliomo Marekani. Tatizo mdomo wake hauna speed limit.

Republican wote tabia zao zinafanana, kama yule domo pira yeye alikuwa hajui Ku synchronize maneno yeye huweka maneno waziwazi (mzee wa war on terror)
 
...will never be... vs ... ...will not be...
Wajuvi wa kudhungu mtujuze!!!
Mpwa hapo hata kwa kizungu changu cha kuombea maji nimeshang'amua utofauti....inakuwaje mtu jiniazi kama wewe ubaki gizani......

Joke.....
 
Haijalishi Trump anasema nini au anafanya nini bali wapiga kura wa Marekani wanataka nini, na mpaka sasa hivi kura za maoni zote zinaonyesha kwamba Trump ndiye anayetakiwa na Wamarekani hivyo kwa Raisi nchi kusema kwamba hawezi KAMWE kuwa Raisi wa Marekani wakati ndiye anayeongoza kwa kupendwa na watu hilo kwangu linaacha maswali mengi klk majibu kuhusu hii inayoitwa demokrasia ya Marekani!
Siyo kweli kuwa wapiga kura wote wa Marekani wanamtaka Trump!. Sasa hivi bado wako kwenye Primary, ungesema labda wapiga kura wa chama cha Republican walio wengi wanamtaka Trump hapo ingemake sense. Lakini eti wapiga kura wa Marekani wanamtaka Trump?. Siyo kweli!.
 
Napenda Trump anavo weza ongea ukweli bila kuficha lakini hafai kuwa raisi wa nchi kama marekani yenye nguvu ya kijeshi na uchumi.... kwenye hiyo area hafai.... nayasema haya bila kuwa na furaha... ningependa sana awe raisi ili hawa hyenes wa africa awashitue kidogo ila kumpa nchi kama usa huyu jamaa kuna uwezekano ni another Hitler in the making.....
 
Udikteta anao na dharau pia. Fikiria mtu hajawa Rais anatamka kuwa akiwa Rais wa USA atamkamata Uhuru Kenyata, Rais wa Kenya na kumfunga kutokana na yeye kwenda Ufaransa na msururu wa watu akiwemo mwanae. Asipomkamata anavamia Kenya? Ya Bush na Iraq!
 
HAHAHAHA DONALD ANATAKA WAAFRICA TUTAWALIWE TENA KWA KUWA HATUWEZI KUJISIMAMIA MEANS AKIWA RAISI WA MAREKANI HEE WAAFRIKA TUNAOPENDA KUTEMBEZA BAKULI LA NJAA TUNATAWALIWA BILA KUFURUKUTA KHAAAAA HAFAI
itakua afadhali maana mmeshindwa kutatua matatizo yenu ya ndani kama zanzibar na mkishauana mnaanza kulalamikia mataifa ya magharibi
 
Japo kuwa trump anaimbiwa nyimbo nyingi na watu wengi lakini hiyo haimaniishi trump hawezi kuwa rais wa marekani na ninavyo jua trump mara nyingi ni mtu ambaye anakuwa sahihi sana katika hesabu zake kama trump angekuwa na tabia za kung'ata ng'ata maneno kama obama kisa anaogopa kukikosesha ushindi chama chake. anaona akisema ukweli ataharibu. kama trump angekuwa anafuata akili kama hizo labda hadi leo hii trump angekufa maskini. Lakini tusimlaumu sana obama kutokana na mazingira aliyo aloyotokea hadi akawa rais

Yeye alicho takiwa kufanya obama na kwaniaba ya chama chake aliatakiwa awaambie wananchi chama chake kimejipanga vipi kuwatumikia iwapo watachaguliwa tena. ili wanachi wawachague watapita njia ipi.
Kwa karne kama hii inahitaji viongozi wanao sema ukweli kama trum.
 
Si kweli kwamba Trump ndiye anayeongoza kwa kupendwa na Wamarekani. Hao wanaompenda ni sehemu tu ya wale wa mlengo wa republicans. Na anaongoza katika maoni kwa kulinganisha na wengine kama kumi sijui. Kwa hivyo basi, kwa ujumla wao siyo kwamba Trump ana majority ya wapenzi. Bali ukimlinganisha na republicans wengine, yeye anaongoza. Obama kafanya utabiri wake, na wala lisiache maswali yoyote katika mawazo yako. Na alitoa sababu zake.
Haijalishi Trump anasema nini au anafanya nini bali wapiga kura wa Marekani wanataka nini, na mpaka sasa hivi kura za maoni zote zinaonyesha kwamba Trump ndiye anayetakiwa na Wamarekani hivyo kwa Raisi nchi kusema kwamba hawezi KAMWE kuwa Raisi wa Marekani wakati ndiye anayeongoza kwa kupendwa na watu hilo kwangu linaacha maswali mengi klk majibu kuhusu hii inayoitwa demokrasia ya Marekani!
 
Mkuu mtu kama Trump anayetukana kulia na kushoto, ana kiburi, tajiri wa kupindukia, hivi umemsikia akitetea wanyonge?
Hata Marekani wanyonge ni wengi sana kuliko unavyodhani.
Kwa misingi hiyo Trump is a security threat!

Mkuu kama Trump hajali wanyonge kwa nini aliwajia juu Viongozi wa Afrika ambao wanag'ang'ania madarakani na kuminya demokrasia ya kweli?? Tatizo lake atumii lugha ya kidiplomasia anaposema ukweli - binafsi hilo halinipi shida, Dunia hivi sasa inahitaji kiongozi wa Taifa kubwa mwenye akili, msema ukweli, mpenda amani na hasiye sumbuliwa na complex za kujiona mnyonge.

Linapokuja suala la amani Duniani Obama ni janga, katika utawala wake ndiye ameruhusu majambazi wachache katika Jeshi la Merikani kutisha tisha Mataifa ya Ulaya akiyazuga kwamba Urusi ina mpango wa kuyavamia - anafanya mazoezi ya kijeshi kwenye mipaka ya Urusi, kasambaza makombola ya nuklia Italy, Ujerumani naUingereza akiwa na lengo la kuwateka akili ili wawe tegemezi kwa Merikani katika Ulinzi na masuala ya Uchumi, hii ni a well organised scheme ya kutaka nchi za Ulaya wasishirikiane na Wachina na Warusi kiuchumi na kiteknolojia - propaganda za kudai Urusi ina mpango wa kuzimshambulia ni mambo ya kutunga tu, cha ajabu baadhi ya Viongozi wa Nchi za Ulaya wanakubaliana na usanii huu wa Merikani, bahati nzuri kiongozi wa Canada aliye chaguliwa juzi juzi amekataa kuingia kwenye mitego ya Wamerikani!

Kipindi kilicho baki cha utawala wa OBAMA ni critical kweli kweli kwa tishio la usalama Duniani, kutotafakali kwake kwa kina kuhusu suala la Syria kunaweza kufumua vita ya tatu ya Dunia - binafsi namuona kama amechanganyikiwa tu hajui aseme nini na kwa wakati gani - anakurupuka tu kulahumu Asaad, Wairan na Warusi - we fikiria, analahumu Viongozi wanaopambana kufa na kupona kuhokoa Dunia dhidi ya magaidi wa ISIS/Daesh ambao ni tishio kweli kweli kwa wahumini wa Dini nyingine na wapagani. Narudia kusema kwamba kiongozi wa Taifa la Merikani mwenye uwezo wa kuleta amani ya kweli Duniani akishirikiana na Putin - kiongozi huyo ni Donald TRUMP pekee.
 
Hebu tuambie ukweli gani huo aliousema ambao wewe unauafiki? Tuorodheshee japo kwa kifupi tu. Tafadhali usilete habari za kutoka magazeti ya tashtiti (satirical magazines) yanayodai Trump kasema hili au lile kuhusu Afrika au viongozi wa Afrika. Kwa sababu hayo mambo hakuyasema. Sasa sema yale ambayo utatuambia kabisa na source zake ili tupime kwamba ni kweli.

Japo kuwa trump anaimbiwa nyimbo nyingi na watu wengi lakini hiyo haimaniishi trump hawezi kuwa rais wa marekani na ninavyo jua trump mara nyingi ni mtu ambaye anakuwa sahihi sana katika hesabu zake kama trump angekuwa na tabia za kung'ata ng'ata maneno kama obama kisa anaogopa kukikosesha ushindi chama chake. anaona akisema ukweli ataharibu. kama trump angekuwa anafuata akili kama hizo labda hadi leo hii trump angekufa maskini. Lakini tusimlaumu sana obama kutokana na mazingira aliyo aloyotokea hadi akawa rais

Yeye alicho takiwa kufanya obama na kwaniaba ya chama chake aliatakiwa awaambie wananchi chama chake kimejipanga vipi kuwatumikia iwapo watachaguliwa tena. ili wanachi wawachague watapita njia ipi.
Kwa karne kama hii inahitaji viongozi wanao sema ukweli kama trum.
 
Lete credible source ya habari kwamba Trump alisema hivyo kuhusu viongozi wa Afrika. Usiquote tu uzushi huu. Hakusema hayo mambo.
Mkuu kama Trump hajali wanyonge kwa nini aliwajia juu Viongozi wa Afrika ambao wanag'ang'ania madarakani na kuminya demokrasia ya kweli?? Tatizo lake atumii lugha ya kidiplomasia anaposema ukweli - binafsi hilo halinipi shida, Dunia hivi sasa inahitaji kiongozi wa Taifa kubwa mwenye akili, msema ukweli, mpenda amani na hasiye sumbuliwa na complex za kujiona mnyonge.

Linapokuja suala la amani Duniani Obama ni janga, katika utawala wake ndiye ameruhusu majambazi wachache katika Jeshi la Merikani kutisha tisha Mataifa ya Ulaya akiyazuga kwamba Urusi ina mpango wa kuyavamia - kasambaza makombola ya nuklia Italy, Ujerumani naUingereza akiwa na lengo la kuwateka akili wawe tegemezi kwa Merikani katika Ulinzi na masuala ya Uchumi, hii ni a well organised schme ya kutaka nchi za Ulaya zisishirikiane na Wachina na Warusi kiuchumi - propaganda za kudai Urusi ina mpango wa kuzimshambulia ni mambo ya kutunga tu, cha ajabu baadhi ya Viongozi wa Nchi za Ulaya wanakubaliana na usanii wa Merikani, bahati nzuri kiongozi wa Canada aliye chaguliwa juzi juzi amekataa kuingia kwenye mitego ya Wamerikani!

Back
Top Bottom