Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,455
- 122,734
Sidhani kama kuna mtu anazuwiwa kusema. Watu wanatukana badala ya kusema. Si haki. Watu wajifunze kukosoa constructively na si destructively. Kuna tofauti kati ya "njoo hapa ya lugha ya ukali na njoo hapa hiyo hiyo ya lugha ya kistaarabu.
Hapa kwamba watu wanatukana ndio wote wenye utetezi dhaifu dhidi yake mnapojifichia. Matusi ya hapa na pale hayawezi kukosekana kwani watu hawanafanani. Hata huko maofisini na sehemu nyingine watu wenye lugha chafu wapo lakini hatufikii mahali pa kukoseana uvumilivu kwa mapungufu yetu.
Kisha utambue watu wote hatuwezi kuwa ndio mzee, kitu ambacho mkulu hataki na pia hakubaliani na mawazo mbadala labda uyalete kwa njia ya kujipendekeza. Sasa wale ambao wanamkosoa waziwazi ndio hao wanakutana na hiyo tabia yake ya kukosa uvumilivu. Hitimisho lake ni watu hao kumuita dictator. Kwa hiyo kama ni dictator au sio kila mtu inategemea na eneo alilosimama. Kuna watu wanaona namba 6 kutokana na eneo waliposimama na wengine wanaisoma kama 9 na wote wako sahihi.