Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Hivi raisi anavyotoa maamuzi au maagizo ni kwa maslahi ya nani?
Ikiwa anaendesha nchi kwa maslahi ya watanzania basi anafaa apongezwe na ikiwa yupo kwa maslahi yake binafsi basi hatuna budi kukemea na kumwita dikteta na kila jina litakalomuudhi.
Kazi ya uraisi si rahisi, hususan katika nchi zetu za Afrika, na daima mpinzani atakuwa mpinzani tu.
Tumeshuhudia raisi jinsi alivyoweza kutatua matatizo ya wanyonge katika mikutano yake, amewaajibisha watendaji wa ovyo, amerudisha nidhamu kwenye ofisi za serikali, rushwa imepungua, viwanja vinapatikana kwa urahisi, mawaziri wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Nadhani hii kauli ya kumuita raisi dikteta ni ule msemo wa waswahili unaosema "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya".
 
Mbali na kuwa umetumia denials as a defensive mechanism kwa kutumia maneno kama "Hatumchukii" n.k, Kwa mtu mwenye akili post yako imejaa chuki binafsi kwa Magufuli binafsi na si kwa kuangalia utendaji wake.

- Hakuna hata sehemu moja umediscuss utendaji wake bali kufanya Character assassination kwa kumpa sifa mbaya ambazo nina uhakika hana.

Asante Eja kwa maoni yako.
 
Yeye mbona anaporomosha matusi? Kusema
Wastaafu wanawashwa washwa si tusi? Na kuita watoto wao wenzie vilaza?

Sidhani kama kuna mtu anazuwiwa kusema. Watu wanatukana badala ya kusema. Si haki. Watu wajifunze kukosoa constructively na si destructively. Kuna tofauti kati ya "njoo hapa ya lugha ya ukali na njoo hapa hiyo hiyo ya lugha ya kistaarabu.
 
Mkuu Paskali, hiyo clip yako hapo Mwalimu Nyerere alikuwa ana state facts, hakuwa anafanya unabiii au kuchuria, he was merely stating the known facts.

Magufuli ni dikteta, na hilo ni tatizo la John Magufuli. NUKTA.

Upande wa pili kuna tatizo la mfumo (system) ambao ni dhaifu na butu haukufanya kazi ya vetting thoroughly. Hakuna namna Magufuli angeshika hata nafasi ya 10 kati ya wagombea 11, kwa sababu track record yake Wizara "alizotawala" ilikuwa mbaya na chafu. Hizo takwimu za kukariri ambazo zilimpa umaarufu zilipaswa kupitishwa kwenye tanuru ili dhahabu ijulikane na makinikia yajulikane.

Ukitaka kujua ubaya wake sikiliza kauli zake anapotafuta sympathy au ego-satisfaction hasa kwa kutumia zile cheap and stereo-typed popular slogans zake za uzalendo, upendo, tumbua nk nk. Ule ni unafiki wa kiwango cha Hollywood. Unafiki na chuki ni tabia zake Magufuli asisingiziwe mtu mwingine awaye yote. Anatakiwa akubali huo udhaifu kisha ajirekebishe (ni process) sio kusema aombewe. Udikteta wake alianzia kwenye familia yake na maisha yake yote amekuwa uchwara, hata kwenye Wizara alizotumikia.

Tunaomkosoa Magufuli, wengi tuna point kwenye hizo facts za Mwl. Nyerere tu. Wengi hatumkosoi kwa kumchukia bali kwa kuonyesha na kuianisha bayana madhaifu yake, ila kiburi chake kimemfanya ashindwe kusikia na kujirekebisha.
Mimi nadhani Pascal Mayalla unatakiwa kuelewa wengi ya wana JF hawana upeo wa ''kuona'' logics zinazojificha kwenye threads zako. Ndugu ni hivi: Mwalimu alikuwa anawaasa wabunge (wananchi) wasiogope kwani kuogopa kwao kutawafanya waje kutawaliwa na diktekta! Lakini si kweli mwanzisha thread anaamini ujinga wa kuwa Nyerere ndie wa kulaumiwa kwa ''kumuumba dikteta'' Magufuli kwa maneno! Yeye ameonyesha tu jamani Nyerere alishasema mkiogopa viongozi mtatawaliwa na diktekata... hivyo mjadala uelekezwe kwa watanzania na wabunge wao wasiogope viongozi...

https://www.jamiiforums.com/members/pascal-mayalla.17813/
 
Hivi raisi anavyotoa maamuzi au maagizo ni kwa maslahi ya nani?
Ikiwa anaendesha nchi kwa maslahi ya watanzania basi anafaa apongezwe na ikiwa yupo kwa maslahi yake binafsi basi hatuna budi kukemea na kumwita dikteta na kila jina litakalomuudhi.
Kazi ya uraisi si rahisi, hususan katika nchi zetu za Afrika, na daima mpinzani atakuwa mpinzani tu.
Tumeshuhudia raisi jinsi alivyoweza kutatua matatizo ya wanyonge katika mikutano yake, amewaajibisha watendaji wa ovyo, amerudisha nidhamu kwenye ofisi za serikali, rushwa imepungua, viwanja vinapatikana kwa urahisi, mawaziri wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Nadhani hii kauli ya kumuita raisi dikteta ni ule msemo wa waswahili unaosema "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya".

Ubarikiwe mkuu, mmebaki wachache sana wenye ubongo mzima. According to Twaweza
 
Hata penye negative kuna kitu cha kujifunza, kulikuwa na kuna nafasi ya kuondoa udikiteta ama kuendelea nao kama tunapendezwa nao. Sasa kama Tanzania tuna udikiteta ama lah, ni suala la viongozi kulitolea mashaka ya wananchi basi. Vinginevyo tubakie na udikiteta tusio upenda.
 
Tafsiri na ufafanuzi wako kuhusu tabia ni sahihi kabisa. Hitimisho lako ndilo lenye kukosa staha, unampo mtuhumu mtu pasipo na ushahidi, na hasa kiongozi wa nchi ambaye anawakilisha Taifa, ukiwemo wewe.

Unaandika mimi naona shida kwa Mkuu wetu, nachunguza na kujiuliza je chanzo cha tatizo alilo nalo ni nini? Nagundua kuwa chanzo ni tabia yake (attitude)... Na moja ya tabia niliyoiona kwa kuangalia matendo, mwenendo na maneno yake ni kiburi (pride) kwa sababu.... Unaendelea kutoa tafsiri ya neno pride kwa kiingereza na kuacha kauli yako ikielea.

Kutuhumu au kusifia tabia ya mtu ni lazima kuwepo vigezo vya kupima au kuelezea sifa hizo. Na ni vizuri katika tafsiri yako ya kiingereza ya neno pride umegusia hivyo vigezo (maneno mazito mlalo kwenye bandiko lako). Tafadhali, tusaidie (mimi na wanaJF) pride ya huyo mtu kwa matendo, mwenendo na maneno yake

Mkuu Mwengeso sijaacha kauli yangu ikielea labda kama ulitaka pia nitafsiri maana niliyoiweka kwa Kiingereza, ambapo sioni ulazima.

Neno ambalo limekuletea mushkel (lisilo na staha) ni kiburi, hapo niko sawa?

Basi kwa ridhaa yako naomba sasa nitoe mifano michache tu kama ulivyoomba ili kuweka staha ya maoni yangu juu ya hiyo tabia.

1) "Mimi sijaribiwi...na sitajaribiwa...." - Julai 2016 (Magufuli: Sijaribiwi) - kwa maoni yangu hapakuwa na haja wala ulazima kutamka maneno hayo ukizangatia akiwa kwenye nafasi aliyoketi sasa. Watu wenye hulka au tabia fulani hukosea kwa aidha hupitiliza au kutotumia maneno stahiki kwa nafasi/vyeo vyao au matukio husika.

2) Serikali na tetemeko la Kagera - Septemba 2016 (http://www.bbc.com/swahili/habari-37405857)....kwa tabia na desturi za wanadam waliostaaribika kwenye majonzi au msiba watu huzungumza au kutenda mambo ya kufariji na kutia moyo. Watu hulazimika kuzuia hisia zao (hasa chuki au tofuati zilizoko) na/au maneno au matendo yenye kuumiza lakini ukiangalia kauli zake na matendo yaliyofuatia (kwake na wasaidizi wake) unaona wazi wazi kasoro za tabia tajwa. Ukiwa Mfariji Mkuu unapaswa kuwa na tabia na uwezo wa kufariji penye kuhitaji faraja. Huwezi kuwa na ile tabia kisha ukawa mfariji kwa sababu upendo, hekima na unyenyekevu (humbleness of heart) ni msingi wa sifa za Mfariji Mkuu (na mfariji mwingine yeyote yule).

3) Serikali haina shamba hivyo haitatoa chakula cha msaada wa wenye njaa - Jan. 2017 (Rais Magufuli: Msidanganywe patakuwa na chakula cha msaada, serikali haina shamba | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today) Nadhani sina haja ya kuelezea (i.e. no need to give my opinion on this one).

4) Sakata la Sukari 2016 mpaka sasa (Oktoba 2017) - Hili lina zaidi ya mwaka mmoja sasa na bado hataki kukukbali kuwa alikosea. Kwa nini???

- Rais Magufuli: Msidanganywe patakuwa na chakula cha msaada, serikali haina shamba | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today)
- Magufuli aahidi sukari ya bei ya chini
- Viwango vipya vya sukari vimetangazwa leo, onyo latolewa kwa watakaobainika kupandisha bei – millardayo.com
- Magufuli mchezo wa sukari hauhitaji hasira | Gazeti la Rai

Funga kazi ni pale aliposema bei ya sukari ilikuwa shs 5,000 kabla hajawa Rais!!!! Je wewe mwaka 2015 au 2014 uliwahi kununua kilo 1 ya sukari kwa shs 5,000? Na je kwa takwimu na uhalisia ukilinganisha bei ya sukari kati ya awamu ya nne yote (miaka 10 ya JK) na awamu hii ya 5 ya Mh Magufuli ni awamu ipi bei ya sukari imepanda/ghali?

Ndugu naomba niishie hapa tafadhali.
 
Kuna mambo mtu huzaliwa nayo na Kuna mambo mtu hujifunza kutokana na malengo yake..udikteta WA magufuli upo na hafundishwi na mtu bali Ni asili yake ndo maana alisema hapangiwi na mtu na wala hasahuriwi na mtu...kumbuka wakati anamuapisha Ana ngwira alitumia neno Tata ambalo watu wengi walielewa kivingine...hili neno la POWER IS POWER and now YOU HAVE POWER..ni kudhiirisha udictefa wake WA kutotaka kuambiwa na mtu na asisikilize la mtu atumie POWER aliyompa...kwani kabla ya yeye kuwa rais mbona thread nyingi Tu huku watu waliomjua wanasema huyu jamaa hashauriki?kabla ya kuwa rais tulimshuku na sasa he has POWER and no one can touch him..anachukua to uzoefu toka kwa watangulizi wake kina museveni na Paulo kagame..na tusitafute mchawi hapa sio Baba WA taifa wala Tundu lisu..MAY HE GET WELL SOON WE PRAY..
Kauli ya sipangiwi na mtu ilikuja baada ya mikelele mingi toka upinzan kushinikiza makonda haondolewe. Nafikir ni vema kuangalia kauli zake zinatolewa mda na mazingira gani.Chadema hawawez wakawa wanampangia jpm nini chakufanya,nani atumbuliwe nani aachwe tena bila taratibu zozote. ILE KAULI NILIIELEWA HIVI.Ila kwakua tumekuwa watu wa propaganda kuliko uhalisia sio ajabu leo ukisema magufuli alisema sipangiwi.
 
Mimi nadhani Pascal Mayalla unatakiwa kuelewa wengi ya wana JF hawana upeo wa ''kuona'' logics zinazojificha kwenye threads zako. Ndugu ni hivi: Mwalimu alikuwa anawaasa wabunge (wananchi) wasiogope kwani kuogopa kwao kutawafanya waje kutawaliwa na diktekta! Lakini si kweli mwanzisha thread anaamini ujinga wa kuwa Nyerere ndie wa kulaumiwa kwa ''kumuumba dikteta'' Magufuli kwa maneno! Yeye ameonyesha tu jamani Nyerere alishasema mkiogopa viongozi mtatawaliwa na diktekata... hivyo mjadala uelekezwe kwa watanzania na wabunge wao wasiogope viongozi...
Kweli kabisa mkuu, woga ni sumu mbaya sana kwa haki na maendeleo iwe ni mtu mmoja au jamii au taifa zima.
 
Mtu,
Anapotoa maoni yake katika Forum lazima aheshimiwe, inawezekana kiwango chake cha uelewa ni kidogo.
Kinachotakiwa ni kumvumilia na kumwelimisha na sio Kumtukana, kisa mmetofautiana kimtazamo,
Jamii ya kistaarabu mambo kama haya hayakubaliki hata kidogo.
Kwanza inakuwa nje ya malengo ya mada husika, pili ni kumvunjia heshima mtu ambaye hata humjui na inawezekana akawa ndugu yako wa karibu kabisa, labda baba yako au kaka.
Tatu unaharibu mtiririko wa mawazo ya watu juu ya mada husika.
Lakini kubwa zaidi unageuza Forum kuwa danguro la matusi.
Unaanzaje kumtukana mtu usiyemjua kama unasema umeelimika ?
Kuelimika si ni kustarabika ?
Au unataka wachangiaji wote watoe hoja zilizoko ktk mawazo yako tu ?
Halafu mnalilia uhuru wa kutoa maoni.
We unayetukana na huyo anayewaadhibu wanaotoa maoni yao, mnatofautiana nini? nikwamba wewe huna nguvu tu ungeweza hata kumwua kwa kutoa maoni tu.

Vijana mjifunze kujibu hoja kwa hoja. Wengine wako humu wanasikiliza tu mijadala kwa lengo la kujifunza.
 
Back
Top Bottom