Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Watu kama wewe ni wamezaji wa kila kitu mnachoambiwa. Makengeza hayawaruhusu kuona kwa Uhuru. Nchi yetu inahitaji kuboreshwa na kusogezwa mbele na siyo kuharibiwa kwa kigezo butu cha uzalendo.Paskali ndugu yangu. Una uelewa wa mambo kiupana sana tena sana. Kwa kutambua hilo, naomba nikuulize kwanza maana ya dikteta ni nini? Hili neno liko kwenye kamusi zetu? Je, haiwezi kuwa rungu la wakubwa ambalo linatumika kusambaratisha umoja wa vinchi vidogo kama haka ka kwetu?
Ni kweli sisi tunaongozwa na dikteta? Kwa dalili au vipimo vipi? Ukiwa Baba wa familia na ukaamka na kumkuta mtoto wako hapo nyumbani hajaenda shule na anachezea midoli au anaumba ng'ombe wa udongo na angalau ukatata kufahamu kwa nini hajaenda shule na akakujibu hataki utafanyaje?
Nafahamu ni lazima utatumia nguvu kwa kuwa kama mzazi utakuwa unafahamu umhimu wa shule. Hapo hujawa dikteta? Ni dhahiri utakuwa dikteta japo dhamira yako itakuwa sahihi na ya kumuokoa mwanao ili asipate madhila huko mbeleni. Lakini pia kuna mifano mingi sana hapa ninaweza kuitoa ikiwemo ya viongozi waliopachikwa majina ya udikteta na mpaka wakaondoshwa madarakani na wengine kuuwawa kama wanyama. Tanzania hatuna dikteta wala hatujampata wa kufanana nae. Mwalimu pia aliwahi kuitwa dikteta na hao hao wanaojaribu kupenyeza hii kitu sasa.
Hakika si watu wema kwetu. Wana mbinu lukuki za kutuvuta mashati. Ukitaka mkeo akuheshimu ni lazima asiwe na uwezo wa kujipatia kipato chake Paskali. Akiwa na kazi yake na akajitosheleza wewe hutoweza kumwambia akupikie ugali usiku wa manane na kama huamini jaribu utakuja unioe mrejesho. Hizi ni propaganda kama demokrasia nk.
Tuziepuke tujenge nchi yetu. Tuna kiongizi mfia nchi tumuungee mkono. Hii ni bahati hatutaiona kirahisi naamini hivyo. Nyerere aliitwa dikteta lakini angalau yeye hakuwahi kukubali hayo na yawezekana hakuwa dikteta bali ni mzazi alietaka mtoto asichezee maboksi siku ya shule badala yake aende shule akasome ili kutengeneza maisha yake ya baadae.
Tusikubali msemo wa "wenzetu" UK au USA. Hao si wenzetu maana wana utamaduni tofauti na sisi na hawatakuja kuwa wenzetu milele.
Watakusifia ukishindwa na kamwe hawatakupenda ukiwa na dalili za kushinda. Ukijiweza maana yake hawatakunyonya tena.